Serikali Kutumia Trilioni 6.7 Kusambaza Umeme Kwenye Vitongoji

Serikali Kutumia Trilioni 6.7 Kusambaza Umeme Kwenye Vitongoji

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

SERIKALI KUTUMIA TRILIONI 6.7 KUSAMBAZA UMEME KWENYE VITONGOJI

Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba amesema Serikali imetenga kiasi cha shilingi Trilioni 6.7 kwa ajili ya miradi ya kusambaza umeme kwenye Vitongoji 36,101 hapa nchini ambavyo havijapata huduma umeme.

Makamba amesema hayo wakati wa kujadili taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu utekelezaji wa Miradi ya maendeleo inayotokana na fedha za mkopo wa ECF kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF), kwa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Jijini Dodoma, Aprili 14, 2023.

"Tanzania Bara ina jumla ya vitongoji 64,760 na kati ya hivyo, 28,659 vimepata umeme kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ambapo vitongoji 36,101 bado havijafikiwa na huduma ya umeme," amesema Makamba.

Amefafanua kuwa katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali imetenga Shilingi bilioni 100 kupitia mkopo kutoka IMF kwa ajili ya kuanza kutekeleza mradi wa kusambaza umeme kwenye Vitongoji vilivyopo katika Mkoa wa Songwe na Kigoma.

Makamba amesema Wakala amepanga kutumia fedha za IMF, kutekeleza mradi wa kusambaza umeme katika Vijiji 654 vya Mikoa ya Kigoma na Songwe, ambapo kuna jumla ya vitongoji 1,821 ambavyo havifakiwa na miundombinu ya umeme.

"Uchaguzi wa Mikoa ya Songwe na Kigoma umezingatia hali ya upatikanaji wa Nishati ya umeme uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa mwaka 2020 na kuonyesha kuwa mikoa hiyo ina kiwango cha chini zaidi cha umeme kwa upande wa Tanzania Bara," amesema Makamba.

Waziri Makamba, ameeleza kuwa Mawanda ya mradi kwa Mkoa wa Kigoma ni ujenzi wa njia za umeme wa msongo wa kati zenye urefu wa kilomita 321, ujenzi wa njia ya umeme wa msongo mdogo zenye urefu wa Kilomita 700, kufunga mashineumba 350 na kuunganisha wateja wa awali 7,664 katika vitongoji 350 kati ya 905 ambavyo havijapata umeme.

Pia, amefafanua kuwa Mkoa wa Songwe, Mawanda ya mradi ni ujenzi wa njia za umeme wa msongo wa kati zenye urefu wa kilomita 420, ujenzi wa njia ya umeme wa msongo mdogo zenye urefu wa kilomita 608, kufunga mashineumba 304 na kuunganisha wateja wa awali 6,688 katika vitongoji 304 kati ya 916 ambavyo havijapata umeme.​

 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-04-15 at 16.01.31.jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-15 at 16.01.31.jpeg
    32.4 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-04-15 at 16.01.31(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-15 at 16.01.31(1).jpeg
    26.4 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-04-15 at 16.01.30(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-15 at 16.01.30(1).jpeg
    47.4 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-04-15 at 10.44.22.jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-15 at 10.44.22.jpeg
    50.3 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-04-15 at 16.01.30.jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-15 at 16.01.30.jpeg
    35.5 KB · Views: 1
Waambieni watu ukweli. Mradi wa REA umefadhiliwa na SIDA bado hela nyingi mmezipiga na kufanikisha kwa asilimia 52 tu.
Hivi mnadhani watanzania wataendelea kukaa gizani?
Sasa hivi mawaziri wawili au watatu wanashindana kupiga pesa kwa ajili ya urais.
Tumewastukia......na wewe kipara huna muda mrefu hapo wizarani pamoja na kubebwa unakobebwa.
 
Back
Top Bottom