Wakuu, hao wanaovuma kama Wazanzibari wakiongozwa na CUF, hawaitaki Tanzania. Ni sisi huku Tanganyika pamoja na CCM ndio tunaohangaika kui"save" Tanzania (JMT). Wao wanachohitaji hasa ni madaraka kamili ya serikali yao ya Zanzibar. Hii habari ya serikali tatu ni tapatapa ya CCM na baadhi ya Watanganyika ambao bado tunashindwa kukubali kuipoteza JMT. Wazanzibari hao hawahangaiki na hoja hii; wanachoangalia ni kama huo mfumo (wa serikali 3) utawakwamisha kwenye lengo lao la kushika hatamu kikamilifu. Hapo ndipo watakapoupinga kwa nguvu zote. Hawa watu wamepania madaraka ya kiserikali kwa nia moja.
Mkuu, wewe umepiga mulemule penyewe; Wazanzibari hao uliowasema ndio ambao hawautaki muungano, na sababu kubwa ni za kidini tu, ingawa wengi hawasemi wazi lakini huo ndio ukweli.
Nchi hii bado haijampata mtu jasiri kama Nyerere wa kulisema hili kwa uwazi, wengi wanalizungumza ku-"save" tu face zao, na hili ndilo tatizo kubwa kuliko yote!
Watanzania (bara na visiwani) tunashindwa sasa kujiona kama Taifa moja na badala yake tunaanza sasa kujitambulisha kwa udini kwa kisingizio cha usehemu, upuuzi mtupu!
Hata hizi serikali tatu ni panadol tu kwenye kutibu malaria, dawa ni kuondokana kabisa na Zanzibar na Tanganyika ili tubaki na Tanzania pekee. Hizi nyinginezo hatuna budi kuzitunza vizuri kwenye vitabu vya historia!
Nyerere na Karume walifanya jambo moja zuri linalotuhitaji sisi wa kizazi hiki kufanya ziada iliyobaki, badala yake sisi (kwa usomi na utaalam wetu) tumeamua kuharibu jambo jema lililoanzishwa na waasisi hawa.
Muungano ulio imara ni suala la utashi wa kisiasa na kamwe sio jambo la kisheria kama wengi wanavyojaribu kutuaminisha hapa. Sheria hufuata katika kuyaweka sawa makubaliano hayo ya kisiasa.
Nyerere na Karume kama wanasiasa wa wakati ule walifanya maamuzi yale vema; lililotakiwa kwa sasa ni wanasiasa wetu kupambanua nini dhamira yao ya kutuunganisha watanzania wote chini ya mwavuli mmoja badala ya utitiri huu wa serikali ambao nina hakika kuwa huko tuendako patachimbika tu, maana hapa tulipofika ndo tumelikoroga kabisaaa!!!!