Serikali kuvuna 75% ya mapato kitalu cha gesi Ruvuma-Mtwara

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Serikali imeingia makubaliano ya kihistoria ya uzalishaji na ugawaji wa mapato (PSA) kitalu cha gesi cha Ruvuma-Mtwara yenye thamani ya Dola milioni 500, hiyo ikiwa ni miaka saba tangu kubadilishwa kwa sheria ya Petroli mwaka 2015.

Kupitia mkataba huo, Serikali itapata faida kwa asilimia 75 tofauti na kabla ya kufanyiwa marekebisho ya sheria hiyo ambayo sasa inaelekeza katika utekelezaji wa miradi hiyo serikali isipate faida chini ya asilimia 25.

Akizungumza leo Novemba 25,2022 Dar es Salaam kabla ya kuingia makubaliano baina ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Kampuni ya Petroli Tanzania ARA ya nchini Oman, Waziri wa Nishati January Makamba amesema, makubaliano hayo ni ya kihistoria tangu kufanyiwa mabadiliko sheria ya Petroli.

Amesema mwaka 2015 baada ya sheria ya petroli kufanyiwa mabadiliko yaliibuka maneno mengi juu ya utekelezaji wake lakini sasa Serikali inavuna matunda ya sheria hiyo.

"Sasa hivi Serikali kwenye mapato ghafi inapata faida tofauti na awali ambapo mapato yalitoka kwenye faida pekee, kwahiyo sheria hii imeweka utaratibu ambao tunatapa zaidi,"amesema.

Kupitia mkataba huo, Makamba amesema utakuwa chachu kwa wawekezaji kufika hapa nchini kutokana na mazingira salama ya uwekezaji.

Waziri Makamba aliiagiza kampuni hiyo, kuhalikisha ndani ya miezi 12 hadi 18 gesi hiyo iwe imeanza kutumika kwani hakuna sababu za mradi huo kuchelewa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dk James Mataragio amesema kupitia mkataba huo shirika hilo litanufaika kwa asilimia 15 na Serikali asilimia 45 hivyo kwa jumla serikali itajikusanyia faida ya asilimia 75.

Amesema mpaka sasa kupitia nradi huo kiasi cha futi za ujazo wa gesi futi milioni 1.6 zimegundulika na kinachofanyika ni ujenzi wa mabomba kutoka Ntorya hadi Madimba.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya ARA Ethan Saygi, ameishukuru Serikali kufuatia makubaliano hayo na kuahidi kutelekeza mradi kwa wakati.

Ugunduzi wa gesi katika kitalu cha Ruvuma-Mtwara ulifanyika mwaka 2012.

MWANANCHI
 
Hivi mimi ndio sijui hesabu au

15 + 45 ni 75?
 
  • Kicheko
Reactions: Obe
.....
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dk James Mataragio amesema kupitia mkataba huo shirika hilo litanufaika kwa asilimia 15 na Serikali asilimia 45 hivyo kwa jumla serikali itajikusanyia faida ya asilimia 75.

MWANANCHI
15+45=60 na sio 75 kama hesabu za mserikali
 
Hii imekaa ki-Megawati megawati tu..!! Maana tuliambia hadi mwaka wa kuuza umeme nje, wakati leo hii tuna mgao wa maana..!!
 
Inshu n kwamba watu wa mkoa huo wananufaika vp??
 
Back
Top Bottom