waheshimiwa salaam. kuna kila dalili ya serikali, kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kuvunja kwa makusudi vifungu vya katiba, sheria za nchi na sheria za haki za binadamu za kimataifa, hii ni kutokana na kupandisha mara dufu ada za kufungulia madai ya ardhi au makazi. Ukisoma Gazeti la Tanzania Daima la tarehe 5 January,ni kuwa serikali imepandisha kwa kiwango kikubwa mno ada za kufungulia madai hayo. hiki ni kilio na mwiba mwingine kwa Mkulima wa nchi hii ambaye mlo wake mmoja wa siku anaupata kwa shida. mathalani Kwa mujibu wa gharama mpya, fomu ya maombi itapanda kutoka sh 500 hadi 4,000 wakati kufungua madai ya mali isiyozidi sh milioni 10 mwananchi atapaswa kulipia sh 40,000 badala ya 5,000 ya awali. Kufungua madai ya mali inayozidi sh milioni 10, mhusika sasa atagharimika sh 120,000 badala ya sh 15,000 za awali, huku kupeleka hati ya utetezi kwa maandishi malipo yake yamepanda kutoka sh 2,500 hadi sh 20,000. Gharama hizo zinaonesha kuwa, wale wanaotaka kufungua maombi madogo watalipia sh 40,000 badala ya sh 5,000 na kupeleka hati ya kiapo itakuwa sh 12,000 badala ya sh 1,500 za awali. ukiangalia hali halisi ya nchi hii ,ardhi na mali za masikini zanachukuliwa na matajiri wasokuwa na utu wala upendo kwa binadamu wenzao,sasa kama mdai ndo huyo masikini,atapata wapi fedha hizo?. Ikumbukwe kuwa gharama hizo zitakuwa zinakinzana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 24 (1) ambayo inamruhusu kila mtu kuwa na haki ya kumiliki mali, na haki ya hifadhi kwa mali aliyonayo. sasa niwaombe wale wote wenye dhamana ya kutetea wanyonge hawa,wasifumbie macho jambo hili. hapa kuna asasi za dini,na asasi zingine zisizo za kiserikali na wale ambao wanaitwa vyama vya upinzani kama kweli wanataka kupigania masilahi ya wanyonge.