Serikali kuwabana zaidi waagizaji Magari yaliyotumika ili kulinda uzalishaji wa ndani

Ni wazo zuri. Muhimu tu hao wazalishaji wajikite kwenye uzalishaji wa magari yao kwa kuangalia consumer needs. Yaani bidhaa iendane na soko lililopo.
Siyo wazalishe magari na kuyauza kwa pesa kubwa, huku wanunuzi wengi wakiwa hawana uwezo wa kuifikia hiyo bei.

Na serikali iachane na zile kodi zake kandamizi. Haiwezekani gari liuzwe kwa mfano shilingi milioni 6 za Kitanzania, halafu serikali nayo inalitoza gari hilo hilo kodi ya shilingi milioni 6! Huu ni wizi, na pia ni dalili ya kuwakomoa wananchi.
 
Professor mwenyewe chaki ilimshinda chuo kikuu, kaingia bungeni ili aweze kupanda vx v8, atuondolee upuuuzi wake.
 
Akienda kuhojiwa kwenye luninga, I'm sure atasema.... pia wanachi wameunga mkono jambo hilo kwasababu walishirikishwa kabla ya serikali kupitisha muswada huo...😜
 
Hahaha! Vichwa vya treni na mabehewa yake vimeagizwa used tena kwa ushauri wa Rais Samia!
 
Hatuna pesa ila ikipunguza kodi sana tutayanunua mapya.

Nani anataka kuendesha gari inalingana na vijana waliozaliwa miaka ya 2000, kila mtu anapenda kitu kipya tatizo gharama.

Sijui magari ya petro na desel yakipigwa ban itakuaje.
 
usipoweka magari used kunaongezeka level ya maskini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…