Serikali kuwabana zaidi waagizaji Magari yaliyotumika ili kulinda uzalishaji wa ndani

Watanzania wajiandae kuanza kununua magari mapya baada ya serikali kukamilisha kuandaa sera mpya ambayo itapiga marufuku Watanzania kununua magari yaliyotumika...
Hii Itapelekea kupungua kwa idadi ya wamiliki wa magari na hatimaye kupelekea kupungua kwa mapato ya serikali yatokanayo na vituo vya mafuta na tozo nyingine zinazohusiana nayo.
 
Nasikia Mahindra wanakuja kuwekeza au wameishafika?

Bolero sio mbaya ila sijui bei itakuwaje.

Walete magari mapya sawa ila na used wasisitishe bali yaje kwa wasioweza kumudu mapya

Hivi hawa viongozi mbona hawabadiliki na kuwa na maarifa hata kidogo.

Kuna ajira gani ya vijana take home ya 2m kuweza kumudu hata kawasaki?
 
Serikalini mawaziri na wabunge waanze kutumia mahindra na wao, sio kutubana sisi pekee, waache v8, la sivyo tunaendelea na toyota zetu za 2005 new model.

Tuache kudanganyana, hakuna kiongozi ataacha utamu wa LC 300 V6 eti akatumie mahindra.
 
Watunga sera ndiyo haohao wavunja sera nambari one
 
Serikalini mawaziri na wabunge waanze kutumia mahindra na wao, sio kutubana sisi pekee, waache v8, la sivyo tunaendelea na toyota zetu za 2005 new model.

Tuache kudanganyana, hakuna kiongozi ataacha utamu wa LC 300 V6 eti akatumie mahindra.
Mkuu mtanunua tu mahindra mpya ina cc 800 ukubwa wa duet na itauzwa kati ya mil 5 hadi 6 .milage 0
 
Mahindra tayari wamekuja kuokoa jahazi!
 

Hujui tu kuwa kitu chochote cha rahisi madhara yake ni makubwa? Nunua gari jipya!
 
Serikali yenyewe ndo mnunuzi mkubwa wa magari mapya kwa kodi zetu.
 
Hawa hawa mapopoma ndio walisemaga enzi za Mwendazake "tutaacha kuvaa mitumba, tutaunda viwanda tuwauzie wazungu mitumba". Kimba kweli hawa jamaa.
 
Yan mtu mmoja tu kutaka kuwekeza hela ndogo hvyo ndo atusababishie adha watu ote wanaoagiza gari used kwa bei za vipato vyetu? Wakati hapa watu wemewekeza zaid ya bilioni 200 kwa mwaka kwa kununua magari nje mfano mzuri hafidh Aficarries.

Nyie kurupukeni tu hayo magari yenu mapya mtakuwa mnauziana wenyewe na kuyaweka kwenye window shop
 
Wakitembea kwenye ma V8 yao mapya huwa akili zinakwenda kwenye kalio zao. Nchi ambayo toothpicks inaagizwa nje, leo wanataka magari mapya 😁
 
Hiyo hoja yako elekeza kwa Kitila!
 
Magari ya mhindi hamna kitu...

Ni heri kununua Toyota RAV4 ya mwaka 1998 kuliko kununua Mahindra mpya isiyo na shape ya shoo wala ubora wa kiwango cha Toyota..

Tunataka Toyota, Honda, Nissan, Pajero, Suzuki, Mercedes Benz, Peugeot, Ford wajenge viwanda vyao hapa na hapo ndipo mje na hiyo sera yenu ya ajabu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…