chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,969
Wadau kwema? Kumekuwa na miito ya baadhi ya watu wakitaka serikali izuie watu kuuza chakula nje ya nchi ili kukabiliana na tatizo la bei ya chakula kupanda.
Sina uhakika sana kama hilo litachangia kushusha bei ya vyakula likifanyika sasa hivi, ila nina uhakika litarudisha nyuma sekta ya kilimo kwa kiasi kikubwa.
Kwa nini? Sekta ya kilimo kwa Tanzania ipo chini sababu ya bei ya mazao mara nyingi kuwa chini na haimlipi mkulima na hata kuna kipindi hairudishi hata gharama za kilimo, sababu ni ukosefu wa masoko yanayoeleweka.
Na hii hufanya watu wengi wasite kuwekeza kwenye kilimo kwa sababu faida yake ni ndogo ukilinganisha na risk na effort anyotumia na kupelekea kilimo cha Tanzania kuwa duni ama kufanywa tu na wakulima wadogo wadogo kwa ajili ya kupata chakula na sio biashara.
Mtu akiwa na milioni zake 200 anaona ni afadhali awe anaingiza bidhaa za kichina nchini kuliko kufanya kilimo sababu kilimo hakilipi.
So matokeo yake nchi inakua ya wachuuzi zaidi kuliko wazalishaji, na ndio maana tunaona nchi imetapakaa machinga kila kona na kwa sababu hii.
Sasa mbinu pekee ya kweli kupunguza bei ya vyakula ama bei ya kitu chochote ni kuongeza supply tu na sio kudhibiti soko.
Na bei za mwaka huu kuwa juu ni mauamivu kwa baadhi ya watu lakini ni neema pia kwa sababu itawapa wakulima mapato na mtaji na nguvu zaidi kuwekeza zaidi kwenye kilimo kipindi kijacho itakayopelekea supply kuongezeka.
Pia inaweza kuwashawishi watu ambao wana mitaji ila hawataki kuwekeza kwenye kilimo kuanza kufikiria kuhusu kuingia kwenye kilimo.
Serikali inaweza kuzuia baa la njaa kwa kuwahimiza wakulima kuweka akiba na kununua kutoka kwa wakulima kwa ajili ya akiba ila sio kuzuia soko la nje.
Kilimo ndio sekta ambayo itatuingizia fedha za kigeni, itaajiri watu wengi na kouondoa umasikini kama tukitumia vizuri.