Serikali kwa kushirikana na Sekta Binafsi imendelea kuimarisha uzalishaji wa ndani wa mbegu bora za mazao ambao umeongezeka kutoka tani 42,096.68

Serikali kwa kushirikana na Sekta Binafsi imendelea kuimarisha uzalishaji wa ndani wa mbegu bora za mazao ambao umeongezeka kutoka tani 42,096.68

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Serikali kwa kushirikana na sekta binafsi imendelea kuimarisha uzalishaji wa ndani wa mbegu bora za mazao ambao umeongezeka kutoka tani 42,096.68 msimu wa 2022/2023 hadi kufikia tani 56,114 msimu wa 2023/2024.

Makadirio ya mahitaji ya mbegu hizo nchini kwa msimu wa 2024/2025 ni tani 80,000 ambapo upatikanaji umefikia tani 42,471.09 sawa na asilimia 53 ya makadirio ya mahitaji ambazo kati ya tani hizo, tani 29,819.57 zimezalishwa ndani ya nchi na tani 12,651.52 zimeingizwa kutoka nje ya nchi.

Serikali ya Awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imepanga kutoa ruzuku ya tani 52,000 za mbegu bora za mahindi kwa wakulima katika msimu wa 2024/2025.

Hadi kufikia Novemba 30, 2024 jumla ya tani 4,000 za mbegu bora za mahindi zenye thamani ya Shilingi bilioni 3.5 ya ruzuku zimenunuliwa na wakulima 79,335

Serikali inaendelea kuhimiza matumizi ya mbegu bora ili kuongeza tija, uzalishaji na kipato kwa wakulima.

#kaziiendelee
#tumejipatanamama

 
Umeandika Vyema -Ninashida na Mbegu ya Ufuta bora nachelewa kupanda nisaidieni
 
Back
Top Bottom