Serikali: Kwa sasa Tanzania ina wagonjwa 66 wa Corona nchi nzima ndani ya mikoa 10 na mikoa 16 haina wagonjwa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,885

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema hadi kufikia leo mchana, kulikuwa na wagonjwa 66 wa #COVID19 katika mikoa 10 hapa nchini.

Akihutubia Bunge JijinI Dodoma, Waziri Majaliwa amesema mikoa 16 ikiwemo Arusha, Pwani, Manyara, Katavi, Rukwa na Kagera haina mgonjwa wa Corona.

Ameongeza kuwa, licha ya mlipuko wa #CoronaVirus wameweza kukaa Dodoma kwa takribani miezi miwili na nusu, na wameweza kutekeleza majukumu mbalimbali ya Bunge.

Amempongeza Rais Magufuli kwa msimamo wake uliofanya Tanzania kuwa mfano wa kuigwa duniani kwa namna aliyoshughulikia ugonjwa huo.
 
Alice in wonderland .tutaelewa SOMO tu na hizi siasa za bongo. Na si walisema mashine zinadanganya?😥
Na si kuna kiongozi alisema tusali tumeshinda corona Yaani hakuna tena covid?
Na pia ...... Anyway nisije kupanik bure.
 
Kwa hiyo wameongezeka kutoka wagonjwa 4 hadi wagonjwa 66 ndani ya wiki moja?

Kweli wanasiasa ni waongo!
 
Alice in wonderland .tutaelewa SOMO tu na hizi siasa za bongo. Na si walisema mashine zinadanganya?😥
Na si kuna kiongozi alisema tusali tumeshinda corona Yaani hakuna tena covid?
Na pia ...... Anyway nisije kupanik bure.
Alice in wonderland .tutaelewa SOMO tu na hizi siasa za bongo. Na si walisema mashine zinadanganya?😥
Na si kuna kiongozi alisema tusali tumeshinda corona Yaani hakuna tena covid?
Na pia ...... Anyway nisije kupanik bure.
Utakuwa ni mjinga kumwamimi mvutabangi
 
Alice in wonderland .tutaelewa SOMO tu na hizi siasa za bongo. Na si walisema mashine zinadanganya?😥
Na si kuna kiongozi alisema tusali tumeshinda corona Yaani hakuna tena covid?
Na pia ...... Anyway nisije kupanik bure.
Aisee, umenikumbusha mbali. Umekisoma kitabu cha Alice ? Basi mimi nimekisoma nikiwa darasa la nne mwaka 1985, swahili version. Kinavutia balaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…