Serikali, labda tungefanya hivi juu ya ajira za ualimu

Mmea Jr

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2016
Posts
798
Reaction score
1,871
Habari zenu wakuu ,,, natumaini wote mpo salama ,, wale walioamka wakiwa wagonjwa ninawaombeni duwa ,, inshallah mtakuwa salama,, na waliofikwa na misiba na majanga ya kila namna ninawaombeni muweze kuvuka salama katika nyaka hizo ngumu zilizowafika..

Kwa kipindi sasa wengi tumeshuhudia njia mbali mbali ambazo serikali imejaribu kuzitumia lakini zote hazijaa zaa matunda ,,, tatizo bado limekuwa likionekana linazidi ukubwa kadri siku mbele zinavyoyoyomaaa ,,, toka kuajiliwa moja kwa moja mpaka leo hii kufanya usahili lakini bado serikali imegonga ukutaa

Kwa upande wangu maoni yangu labda tufanye/serikali ifanye hivi ,,,

Serikali itoe waraka ,, utakao wataka walimu woteee watakaomaliza labda katika mwaka huu wa masomo katika vyuo mbali mbali nchini wajitolee ,, na walimu hawa watapaswa kujitolea kwa muda usiopungua miaka 3 (mfano tu )

Serikali ivihimize vyuo mbali mbali vinavyotoa kozi za ualimu kutuma majina ya wanafunzi walimu wotee walio mwaka wao wa mwisho wa masomo ya ualimu kwenda tamisemi ( mfano ) ..

Tamisemi kwa kutumia ule mfumo wao wa OTEAS ,, wayaweke majina hayo ya wanafunzi wa mwaka wa mwisho yaliyotumwa na vyuo mbali mbali vitoavyo course za ualimu kwenye Mfumo wao wa OTEAS ,, afu wanafunzi wotee wanaosomea ualimu baada ya kumaliza watatakiwa kuingia kwenye huo mfumo wao TAMISEMI ( OTEAS ) kwenda ku -comfirm kama wapo tayari kujitolea asiyetaka kujitolea siyo lazima ku-comfirm ,, baada ya hapo TAMISEMI waaandae orodha itakayokuwa imetoa mchanganuo juu ya
- idadi ya wahitimu waliotayari kujitolea

- mikoa waliopo ,, vyuo walivyosoma

- mikoa ambayo wangependa kujitolea

-masomo waliyosoma pindi wakiwa chuo

Tamisemi ,, ipeleke orodha hii wizara ya elimu ambayo yenyewe itajua namna ya kufanya kuwawezesha vijana hawa pindi wawapo huko kwenye maeneo yao ya kujitolea hata kwa kuomba kuongezewa bajeti na bunge ili sehemu ya bajeti iliyoongezeka itumike kwa ajili ya kuwawezesha vijana hao wakiwa huko vituoni ( of course sioni kama wizara hii kama itashindwa kulitekejeza jambo dogo hili ),, baada ya hapo wizara iipe Tamisemi kibali cha kuwapangia vijana hawa katika maeneo mbali mbali yenye uhitaji pindi vijana watakapo maliza muda wao wa kujitolea wapewe kabisa vyeti vyenye utambulisho ambavyo watavitumia hata wakati wa kuomba kazi za ualimu huko serikalini

Kama kutilia mkazo program hii Serikali sasa iweke tamko rasmi kuwa kama hutopitia hatua hii ya kujitolea kwa miaka 2 au 3 basi hautoweza kuajiliwa kama mwalimu katika shule za serikali Tanzania

Faida yake

-Serikali itakuwa umetatua tatizo la uhaba wa walimu hasa maeneo ya vijijini

- wakati mzunguko huu unaendelea ,, serikali itumie nafasi hii kupunguza mlundikano wa waalimu uliopo mtaani

- mfumo huu utasaidia kupata wanafunzi walimu wenye nia ya dhati ya kusomea ualimu

Japo hasra za mfumo huu pia zipo

Kama vile kuiongezea gharama serikali yetu nk
Nikioandika hapo ni ushauri na mtazamo wangu

Je wewe kama mtanzania ,, unaishauri serikali ichukue hatua gani ili kukabiliana na tatizo hili la ajira hasa za ualimu ???.
 
Wewe jamaa una matatizo sio bure, kwahiyo uwezo wako wa kufikiria ndipo ulipoishia?

Hivi unajua maana ya kujitolea kweli? Kwahiyo kama wewe unajitolea unataka Kila mtu ajitolee?
 
Tatizo maokoto kwenye kinu hayatoshi.
 
Waliosomea ualimu waruhusiwe kufanya kazi sehemu zingine kama Benki, masoko , biashara na utawala. Sasa Nini maana ya kusoma BaeD ama BScE kama unalazimika kuwa mwalimu tu.
 
Yaani mtu ajitolee miaka 3
Ataishi vip, yeye na familia yake
Yaani kila siku uage mke na watoto unaenda kujitolea

Kwa hao Rais, waziri,wanajitolea Bure au wanajilipa mahela

Yaani mtu aharibu future yake ajitolee miaka 3
Hivi anaifahamu vizuri serikali huyu ujitolee miaka mitatu si serikali itajisahau mpaka kuajiri ,waendeleee kuajiri Kwa miaka vilevile
 
Wewe jamaa una matatizo sio bure, kwahiyo uwezo wako wa kufikiria ndipo ulipoishia?

Hivi unajua maana ya kujitolea kweli? Kwahiyo kama wewe unajitolea unataka Kila mtu ajitolee?
Sasa badala ya kulalamika na kutoa kashfa ,, iliendeza uje na wazo lako hapa ulitete kwa hoja ,,, hoja yenye mashiko basi ndiyo ipitie mwalimu ,,, sasa hivi ulivyofanya maana yake nini ??
 
Tatizo maokoto kwenye kinu hayatoshi.
Basi tu serikali haijaamua ,,, kama inaweza kununua v8 zaidi ya 100 kila mwaka ,, inashindwa nini kwenye ishu ndogo kama hizi ,,, kila graduate serikali ikampiga na laki 3 haita pendeza kweli ???..
 
Waliosomea ualimu waruhusiwe kufanya kazi sehemu zingine kama Benki, masoko , biashara na utawala. Sasa Nini maana ya kusoma BaeD ama BScE kama unalazimika kuwa mwalimu tu.
Hapa watakuja na hoja ya kuheshimu professionalism ,,, japo kwa walimu hichi kitu huwa hakiangaliwi maana huku wote walimu na wasio walimu tunaomba tu na maisha yanaendelea
 
Maisha y sasa hivi yanahitji kujituma na kuwa na malengo

Huo muda wa kupoteza katika kujitolea miaka 2-3 utakuwa unalipwa pesa kiasi gani.

Ina maana umekosa Kazi y kufanya hadi uamini kuwa lazima ujitolee ?

Ukiwa MTU wa kupoteza muda Kama hivi ni hatari Kwa Afya yako ya akili na uchumi.
 
Habari zenu wakuu ,,, natumaini wote mpo salama ,, wale walioamka wakiwa wagonjwa ninawaombeni duwa ,, inshallah mtakuwa salama,, na waliofikwa na misiba na majanga ya kila namna ninawaombeni muweze kuvuka salama katika nyaka hizo ngumu zilizowafika..

Kwa kipindi sasa wengi tumeshuhudia njia mbali mbali ambazo serikali imejaribu kuzitumia lakini zote hazijaa zaa matunda ,,, tatizo bado limekuwa likionekana linazidi ukubwa kadri siku mbele zinavyoyoyomaaa ,,, toka kuajiliwa moja kwa moja mpaka leo hii kufanya usahili lakini bado serikali imegonga ukutaa

Kwa upande wangu maoni yangu labda tufanye/serikali ifanye hivi ,,,

Serikali itoe waraka ,, utakao wataka walimu woteee watakaomaliza labda katika mwaka huu wa masomo katika vyuo mbali mbali nchini wajitolee ,, na walimu hawa watapaswa kujitolea kwa muda usiopungua miaka 3 (mfano tu )

Serikali ivihimize vyuo mbali mbali vinavyotoa kozi za ualimu kutuma majina ya wanafunzi walimu wotee walio mwaka wao wa mwisho wa masomo ya ualimu kwenda tamisemi ( mfano ) ..

Tamisemi kwa kutumia ule mfumo wao wa OTEAS ,, wayaweke majina hayo ya wanafunzi wa mwaka wa mwisho yaliyotumwa na vyuo mbali mbali vitoavyo course za ualimu kwenye Mfumo wao wa OTEAS ,, afu wanafunzi wotee wanaosomea ualimu baada ya kumaliza watatakiwa kuingia kwenye huo mfumo wao TAMISEMI ( OTEAS ) kwenda ku -comfirm kama wapo tayari kujitolea asiyetaka kujitolea siyo lazima ku-comfirm ,, baada ya hapo TAMISEMI waaandae orodha itakayokuwa imetoa mchanganuo juu ya
- idadi ya wahitimu waliotayari kujitolea

- mikoa waliopo ,, vyuo walivyosoma

- mikoa ambayo wangependa kujitolea

-masomo waliyosoma pindi wakiwa chuo

Tamisemi ,, ipeleke orodha hii wizara ya elimu ambayo yenyewe itajua namna ya kufanya kuwawezesha vijana hawa pindi wawapo huko kwenye maeneo yao ya kujitolea hata kwa kuomba kuongezewa bajeti na bunge ili sehemu ya bajeti iliyoongezeka itumike kwa ajili ya kuwawezesha vijana hao wakiwa huko vituoni ( of course sioni kama wizara hii kama itashindwa kulitekejeza jambo dogo hili ),, baada ya hapo wizara iipe Tamisemi kibali cha kuwapangia vijana hawa katika maeneo mbali mbali yenye uhitaji pindi vijana watakapo maliza muda wao wa kujitolea wapewe kabisa vyeti vyenye utambulisho ambavyo watavitumia hata wakati wa kuomba kazi za ualimu huko serikalini

Kama kutilia mkazo program hii Serikali sasa iweke tamko rasmi kuwa kama hutopitia hatua hii ya kujitolea kwa miaka 2 au 3 basi hautoweza kuajiliwa kama mwalimu katika shule za serikali Tanzania

Faida yake

-Serikali itakuwa umetatua tatizo la uhaba wa walimu hasa maeneo ya vijijini

- wakati mzunguko huu unaendelea ,, serikali itumie nafasi hii kupunguza mlundikano wa waalimu uliopo mtaani

- mfumo huu utasaidia kupata wanafunzi walimu wenye nia ya dhati ya kusomea ualimu

Japo hasra za mfumo huu pia zipo

Kama vile kuiongezea gharama serikali yetu nk
Nikioandika hapo ni ushauri na mtazamo wangu

Je wewe kama mtanzania ,, unaishauri serikali ichukue hatua gani ili kukabiliana na tatizo hili la ajira hasa za ualimu ???.
Ukichukua kamusi ya kiswahili sanifu ukasoma na kuelewa maana ya" kujitolea " halafu ukaangalia maisha ya mtaani yanahitaji nini plus umri kusonga mbele hili wazo litazalisha omba omba wengi mtaani na kutengeneza mzigo kwa taifa.vijana tuacheni uzembe maarifa ya ualimu plus ukijichanganya mtaani kufanya kazi unatoboa unatoboa ami nawambieni.
 
Waajili kulingana na batch ya kumaliza chuo

Waliotangulia kuhitimu waanze wao maana umri unawatupa mkono ukizidi kuwaacha hawatakuja kuanilika tena au watakaa kwenye ajila muda mfupi mno Kisha kustaafu bila kufanya chochote.
 
Sawa ,, lakin sasa ili kutoa kelele ndiyo nikaongezea wadogozao most likely they around 23 yrs the moment they graduate ,, wawapelek kama kwenye internship ili ku -buy time huku wakiendela kuwaajili kakazao ili at least watakapo reach 26 or 27 years old ndiyo waajiliwe hivyo wazo lako halipo mbali na langu mkuu
 
Habari zenu wakuu ,,, natumaini wote mpo salama ,, wale walioamka wakiwa wagonjwa ninawaombeni duwa ,, inshallah mtakuwa salama,, na waliofikwa na misiba na majanga ya kila namna ninawaombeni muweze kuvuka salama katika nyaka hizo ngumu zilizowafika..

Kwa kipindi sasa wengi tumeshuhudia njia mbali mbali ambazo serikali imejaribu kuzitumia lakini zote hazijaa zaa matunda ,,, tatizo bado limekuwa likionekana linazidi ukubwa kadri siku mbele zinavyoyoyomaaa ,,, toka kuajiliwa moja kwa moja mpaka leo hii kufanya usahili lakini bado serikali imegonga ukutaa

Kwa upande wangu maoni yangu labda tufanye/serikali ifanye hivi ,,,

Serikali itoe waraka ,, utakao wataka walimu woteee watakaomaliza labda katika mwaka huu wa masomo katika vyuo mbali mbali nchini wajitolee ,, na walimu hawa watapaswa kujitolea kwa muda usiopungua miaka 3 (mfano tu )

Serikali ivihimize vyuo mbali mbali vinavyotoa kozi za ualimu kutuma majina ya wanafunzi walimu wotee walio mwaka wao wa mwisho wa masomo ya ualimu kwenda tamisemi ( mfano ) ..

Tamisemi kwa kutumia ule mfumo wao wa OTEAS ,, wayaweke majina hayo ya wanafunzi wa mwaka wa mwisho yaliyotumwa na vyuo mbali mbali vitoavyo course za ualimu kwenye Mfumo wao wa OTEAS ,, afu wanafunzi wotee wanaosomea ualimu baada ya kumaliza watatakiwa kuingia kwenye huo mfumo wao TAMISEMI ( OTEAS ) kwenda ku -comfirm kama wapo tayari kujitolea asiyetaka kujitolea siyo lazima ku-comfirm ,, baada ya hapo TAMISEMI waaandae orodha itakayokuwa imetoa mchanganuo juu ya
- idadi ya wahitimu waliotayari kujitolea

- mikoa waliopo ,, vyuo walivyosoma

- mikoa ambayo wangependa kujitolea

-masomo waliyosoma pindi wakiwa chuo

Tamisemi ,, ipeleke orodha hii wizara ya elimu ambayo yenyewe itajua namna ya kufanya kuwawezesha vijana hawa pindi wawapo huko kwenye maeneo yao ya kujitolea hata kwa kuomba kuongezewa bajeti na bunge ili sehemu ya bajeti iliyoongezeka itumike kwa ajili ya kuwawezesha vijana hao wakiwa huko vituoni ( of course sioni kama wizara hii kama itashindwa kulitekejeza jambo dogo hili ),, baada ya hapo wizara iipe Tamisemi kibali cha kuwapangia vijana hawa katika maeneo mbali mbali yenye uhitaji pindi vijana watakapo maliza muda wao wa kujitolea wapewe kabisa vyeti vyenye utambulisho ambavyo watavitumia hata wakati wa kuomba kazi za ualimu huko serikalini

Kama kutilia mkazo program hii Serikali sasa iweke tamko rasmi kuwa kama hutopitia hatua hii ya kujitolea kwa miaka 2 au 3 basi hautoweza kuajiliwa kama mwalimu katika shule za serikali Tanzania

Faida yake

-Serikali itakuwa umetatua tatizo la uhaba wa walimu hasa maeneo ya vijijini

- wakati mzunguko huu unaendelea ,, serikali itumie nafasi hii kupunguza mlundikano wa waalimu uliopo mtaani

- mfumo huu utasaidia kupata wanafunzi walimu wenye nia ya dhati ya kusomea ualimu

Japo hasra za mfumo huu pia zipo

Kama vile kuiongezea gharama serikali yetu nk
Nikioandika hapo ni ushauri na mtazamo wangu

Je wewe kama mtanzania ,, unaishauri serikali ichukue hatua gani ili kukabiliana na tatizo hili la ajira hasa za ualimu ???.
KUJITOLEA HAKIFAI KUA KIGEZO CHA TAIFA; BADALA YAKE SERIKALI IONGEZE AJIRA.

Hoja ya Kujitolea Kama Kigezo cha Ajira Serikalini: Je, Ni Suluhisho au Tatizo?

Ni dhahiri kwamba changamoto ya ajira ni kubwa, lakini badala ya kutumia kujitolea kama kigezo, serikali inapaswa kuzingatia kuongeza ajira rasmi kwa ajili ya Watanzania wote.

1. Changamoto ya Kujitolea: Uzalendo na Gharama za Maisha

Kujitolea ni jambo la kujivunia, na wengi waliojitolea wanafanya hivyo kwa moyo wa uzalendo. Hata hivyo, kusema kuwa wanaojitolea pekee ndio wazalendo ni kudhalilisha wale ambao wangependa kujitolea lakini hawawezi kutokana na changamoto za kiuchumi. Kijana anayekabiliwa na gharama za kupanga, chakula, na mahitaji mengine ya msingi hawezi kumudu kujitolea kwa muda mrefu bila kulipwa. Hivyo, kigezo cha kujitolea kinawaweka katika nafasi ngumu wale wenye kipato cha chini, na kuwakandamiza zaidi huku wenye uwezo kifedha wakipata nafasi hizo kwa urahisi. Serikali inapaswa kuelewa kuwa uzalendo unahitaji msaada wa kifedha kwa wale ambao hawana uwezo wa kujitolea kwa muda mrefu.

2. Kujitolea Sio Katika Serikali Pekee

Wale wanaojitolea katika sekta binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali pia wanatoa mchango muhimu kwa taifa. Wanapofanya kazi kwenye miradi ya jamii, elimu, afya, na huduma nyingine, wanachangia moja kwa moja katika maendeleo ya nchi yetu. Kutambua mchango wa sekta binafsi katika suala hili ni muhimu, kwa kuwa kufanya ajira za kujitolea kuwa kigezo rasmi serikalini kunaweza kuzorotesha motisha na maana ya kujitolea kwa dhati katika sekta nyingine.

3. Haki na Usawa: Athari kwa Wale Wasio na Uwezo wa Kifedha

Kujitolea kama kigezo cha ajira serikalini kutaathiri wale wasio na uwezo wa kifedha. Wenye uwezo wa kifedha wataweza kujitolea kwa muda mrefu bila kulipwa, lakini wale walio na changamoto za kifedha, ambao hawawezi kujitolea kwa muda mrefu, wataachwa nyuma. Hii inaleta ukosefu wa usawa na unyanyapaa kwa watu wenye kipato cha chini, ambao watalazimika kujitolea kwa shida huku wakitegemea kupata ajira kupitia upendeleo. Serikali inapaswa kuzingatia kuwa ajira ni haki ya kila mtu, na kwamba nafasi hizo zinapaswa kutolewa kwa misingi ya ushindani wa wazi, si kwa upendeleo wa kifedha.

4. Ujanja na Njia za Mkato katika Kupata Ajira

Ikiwa kujitolea litakuwa kigezo rasmi cha ajira, kuna hatari ya watu kuanza kutumia njia za mkato kupata barua za kujitolea, ikiwemo kupitia ndugu na marafiki. Watu watajipatia barua za kujitolea ili tu wapate nafasi ya ajira, jambo ambalo litawathiri wale waliojitolea kwa dhati. Hatua hii itazua rushwa na upendeleo, na hata kudhoofisha mfumo mzima wa ajira katika sekta ya umma.

5. Sheria Inahitaji Ajira Kupatikana kwa Ushindani

Ajira katika serikali kuu inapaswa kutolewa kwa ushindani na kwa uwazi. Kama mtu alijitolea, bado anapaswa kufuata taratibu rasmi za kuomba aj

ira kama kila raia mwingine, kwani ajira serikalini ni haki inayotolewa kwa misingi ya usawa na ushindani. Kuweka kigezo cha kujitolea kinapunguza nafasi ya kila Mtanzania mwenye sifa kuweza kupata ajira kwa usawa na uwazi. Kujitolea kunapaswa kuwa fursa ya kujenga uzoefu, sio upendeleo wa kupata ajira. Serikali inapaswa kuhakikisha kuwa nafasi za ajira zinalenga ustadi na uwezo wa kitaaluma, ili kuendana na sheria na kanuni za ajira kwa umma.

Mapendekezo kwa Serikali: Ajira Ngazi za Mikoa kwa Wanao Jitolea

Kwa wale wanaojitolea katika ngazi za mikoa na wilaya, serikali inaweza kutoa nafasi maalum kwa wale wanaoonyesha bidii na kujitolea kwa dhati kwa muda mrefu, lakini hii iwe kwa nafasi maalum za kujaza pengo la haraka lililotokana na kustaafu, vifo, au kuondoka kwa wafanyakazi wa awali. Hii itawapa wale waliojitolea katika maeneo hayo nafasi ya ajira kulingana na mchango wao, lakini bila kupunguza haki ya raia wengine kuomba nafasi za ajira za serikali kuu ambazo zinatakiwa kuwa wazi kwa wote.

Hitimisho

Mjadala wa kujitolea kuwa kigezo cha ajira unahitaji tahadhari na tafakari ya kina. Kutumia kujitolea kama kigezo rasmi cha kuajiri serikalini kunaweza kusababisha upendeleo, ukosefu wa haki, na unyanyapaa kwa wale ambao hawana uwezo wa kifedha wa kujitolea kwa muda mrefu. Serikali inapaswa kuendelea kuweka mkazo kwenye kuunda nafasi zaidi za ajira rasmi na kushirikisha watanzania wote kwenye mchakato wa kupata ajira. Mfumo wa ajira unapaswa kuwa shirikishi na wenye uwazi, na kuzingatia viwango vya kitaaluma na sheria za kazi, ili kutoa fursa sawa kwa raia wote. Ikiwa serikali itaamua kutumia kujitolea kama sehemu ya vigezo vya ajira, basi inapaswa pia kuzingatia kuwafadhili wale wanaojitolea, ili kutoa fursa sawa kwa kila mtu anayehitaji na kuhakikisha kuwa mfumo wa ajira haupotoshwi na ushawishi wa kifedha.
 
Mimi mara nyingi huwa nashauri mtu ajitolee ili aongeze ujuzi utakaomnufaisha yeye kama yeye huko mbeleni
 
Back
Top Bottom