Tatizo lilianza pale ambapo wananchi waliruhusiwa kutengeneza wenyewe barakao. Zile ni zana za kitabibu ni moja ya vifaa muhimu kwa wahudumu na mtu yeyote katika kujikinga na maambukizi kwa njia ya hewa ama njia zenye kufanana.
Jamii inaanza kushona vitenge kuwa barakoa tupo kimya! Ilitakiwa tenda itolewe katika viwanda vya ndani kushirikiana na wizara ya Afya ili kutengeneza bidhaa zenye ubora na zinazofaa kwa matumizi.
Wizara ya afya inahimiza barakoa iwe na matabaka 3 (layer) sasa hizi zetu zina matabaka matatu kweli?