Serikali: Magari chini ya mwaka 2010 yasiingizwe nchini

Serikali: Magari chini ya mwaka 2010 yasiingizwe nchini

analgesic

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2013
Posts
719
Reaction score
1,112
Waziri mkuu amesema magari yaliotengenezwa chini ya mwaka 2010 yasiingizwe nchini, naona tunakoelekea kumiliki gari itakuwa ujipange haswa.

Na biashara ya magari yaliondani ya nchi inaenda kukua kwa Kasi.

====================================

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema magari yaliotengenezwa chini ya mwaka 2010 yasiingizwe nchini.

“Tanzania haitakiwi kuwa dampo kwa kuleta magari yaliyopitwa na wakati, Bunge letu limeshapitisha sheria kuwa magari yote yanayoingizwa nchini yawe yametengenezwa baada ya mwaka 2010 kuja huku mbele na siyo nyuma ya hapo, huo ni wajibu wa TBS, lazima ijiridhishe na ielimishe wanaoagiza magari,” - Majaliwa.

Ameitaka Kampuni ya Kimataifa ya Kuhudumia Makontena Tanzania (TICTS) kuimarisha utendaji kazi wake ikiwemo kuacha kuchelewesha ushushaji wa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam.

 
Hii kauli tunaweza kuichukulia poa lakini Kuna magari ya maana sana Hatutayaona tena yakiingizwa Nchini..
Haya yafuatayo
images.jpg
images%20(2).jpg
images%20(3).jpg
images%20(1).jpg
images%20(5).jpg
images%20(4).jpg

Magari Yoote haya yametengenezwa 2009 kurudi nyuma....

Siyo rahisi kutekelezeka kwa hyo kauli...

Sijui kama wanamaanisha kweli walichokisema
 
Uchumi huo bado hatujaufikia na bado hawana mbadala wa kutuuzia/kukopesha gari mpya na hizo used za 2010.
South africa wanaweza kwa sababu wana viwanda vya ku assemble magari yote unayoona yapo south Africa/ Sud africa.

Je sisi tuna viwanda vingapi vya ku assemble hizo gari?

Na je kuna mikopo nafuu kwa wananchi kuweza kumiliki hayo magari?.
 
Muhimu kuwe na mindset, mentality mpya. Kwamba gari ni kitu muhimu sana kwa kuchochea maendeleo karibu kwenye kila sekta hapa TZ. Siyo anasa.

Ni muhimu kama barabara, simu, hospitali, masoko, kazi, biashara. Kiungo muhimu sana kwa mkulima, mfanyakazi, mfanyabiashara, mgonjwa, mwanafunzi, kuchochea biashara, wagonjwa kuwawahisha hospitalini, ufanisi.

Hakuna haja ya kuyapiga marufuku, just ongeza kodi. Kuna wengi wanayapenda na wako tayari kulipia pesa yoyote kuyapata. Kutokana na kodi kubwa hayatakuwa mengi. Wanaweza kutoza kodi 150%- 200% magari ya zamani na magari ya kuanzia 2010- 2022 kama 25%.

Wakifanya hivyo tutapata gari nyingi imara, rafiki kwa mazingira, tutapunguza ajali, kuongeza ufanisi, ajira, mapato serikalini.
 
Back
Top Bottom