Serikali: Mashine ya kwanza ya Kufua Umeme Bwawa la Nyerere itawashwa Mwezi Februari 2024

Serikali: Mashine ya kwanza ya Kufua Umeme Bwawa la Nyerere itawashwa Mwezi Februari 2024

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2022
Posts
9,436
Reaction score
10,944
My Take
Hongera sana Serikali ya awamu ya 6 na Tanesco Kwa sababu hii ni mapema zaidi kabla ya mwezi June ambao ulipangwa kabla.

Kufuatia uwepo wa mgao wa umeme nchin Serikali kupitia Wizara ya Nishati imeuarifu Umma kuwa Februari 25,2024 mashine namba 9 ya kufua umeme kwenye bwawa la mwalimu Nyerere itawashwa rasmi kwaajili ya uzalishaji wa umeme nchini.

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba kwenye mkutano wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Nishati uliofanyika jijini Dodoma ambapo amesema zoezi la kuwasha mashine nyingine lifuata kwa awamu .

“Tulikuwa tumedhani kwamba majaribio yangeanza mwezi wa kwanza lakini majaribio yameweza kuanza mwezi mmoja kabla yameanza mwezi Disemba kwahiyo ni hatua inayopelekea matumaini kwa watanzania kwamba sasa tunaondoka kwenye adha hii ya mgao wa umeme” Mhandisi Felchesmi Mramba Katibu Mkuu Wizara ya Nishati .

Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga ameendelea kuhimiza watendaji wa wizara hiyo kuhakiki ubora wa miundombinu ili kuruhuru upatikanaji wa umeme.

Kazi iendelee 👇


PIA SOMA

TUHUMA ZA UFISADI NA HUJUMA

HISTORIA
 
My Take
Hongera sana Serikali ya awamu ya 6 na Tanesco Kwa sababu hii ni mapema zaidi kabla ya mwezi June ambao ulipangwa kabla.

Kazi iendelee 👇

View: https://youtu.be/kfSbmmjOyfY?si=20MEji85dwI1JThE

Binafsi naamini piga ua mabeberu kote duniani mpango wao nchi zetu zisijitosheleza kwa umeme daina. Wanafaidika tukiweweseka kwa uhaba na ughali wa umeme maana wanajua kwa hali hiyo hatuwezi kuendeleza viwanda. Wanalotaka wao tuwe soko na tegemezi kwao daima kwa hivyo pamoja na juhudi kuongeza uzalishaji tutashuhudia umeme hakuna.
Inahitaji kiongozi imara sana na mwenye maona sahihi kama magufuli kupambana na hiko kisiki. Tuombe mungu 2024 tuweze kupata magufuli mwingine.
 
Binafsi naamini piga ua mabeberu kote funiani mpango wao nchi zetu zidijitodheleza kwa umeme daina. Wanafaidika tukiweweseka kwa uhaba na ughali wa umeme maana wanajua kwa hali hiyo hatuwezi kuendeleza viwanda. Wanalotaka wa o tuwe soko na tegemezi kwao daima.
Inahitaji kiongozi imara sana na mwenye maona sahihi kama magufuli kupambana na hiko kisiki. Tuombe mungu 2024 tuweze kupata magufuli mwingine.
Hizo ni hadithi za kufikirika.Makampuni makubwa Yako Afrika kuchimba Madini, unadhani yataweza kuwa na Ufanisi kama umeme ni ghali na haujitoshelezi?https://www.reuters.com/world/afric...ct-accord-with-edf-led-consortium-2023-12-13/
 
Sijui SGR itaaanza lini? Nawaza tu kwa sauti
 
Si walisema wangeanza kuingiza huo umeme kwenye gridi ya taifa mwezi huu na wakatangaza hadi kukatika kwa umeme wamebadilika tena 🤔🤔
 
Back
Top Bottom