Serikali, matumizi ya nguvu sana ni ishara ya kupoteza uhalali wa kuongoza

El Roi

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2020
Posts
297
Reaction score
537
Katika falisafa ya Uongozi Matumizi ya nguvu sana huwa siyo jambo linalopewq kipaumbele.

Mwanafalsafa mmoja aliwahi kufananisha Matumizi ya nguvu na Sabuni.

Unajua kadiri unavyoitumia sana sabuni ndivyo inavyoishia na Mwisho kwa sababu unaitumia sana utajikuta imeisha.

Ninapoitazama nchi yetu naona kabisa dalili zote za kuingia katika dimbwi hili la utawala kupoteza uhalali wa kuongoza

Kumbuka siseme uhalali wa kutawala. Kutawala na kuongoza ni mambo mawili yenye utofauti.

Kutawala ni kulazimisha na Kuisukuma mambo kwa nguvu. Kuongoza ni ushawishi ambao kundi la wanaoongoza wanauweka juu ya waongozwa.

Kumezuka kasumba Sasa katika nchi yetu, ambapo ukiwa na jicho la utambuzi, utaona Matumizi ya nguvu ya vyombo vya Dola, na walioko katika serikali, chama tawala nk wanavyofanya.

Ebu fikiria tuko mahali ambapo ukitoa maoni kinyume na watawwala unakamatwa na kushughulikiwa na Kila mtu aliyeko kwenye mfumo wa kutawala. Je haya siyo Matumizi mabaya ya sabuni? Kwa Nini kutumia nguvu kwa Kila kitu na Kila jambo?

Chalamila nae na Dar yake ni vitisho Kila siku. Iko wapi ile nguvu ya ushawishi ya viongozi??

Kwa Nini hatuna viongozi Tena wanaopendwa kwa mguso wao?

Wako wapi viongozi ambao hotuba zao tu kwa sababu ya ushawishi na siyo maguvu zinawafanya watu watulie na kufurahi? Waovu wengine waache uovu wao hata bila nguvu?

Nashauri Matumizi ya nguvu, yasiwapotoshe watawala kudhani Wana nchi nzuri yenye amani kumbe ni uzuri wa bandia (cosmetic beauty).

Nenda wapi Tanzania kama siyo vitisho tu? Iko wapi nguvu ya hoja na upendo wa viongozi kwa wanaowaongoza?

Familia yoyote ambayo inaendeshwa kwa mabavu ndo familia mbovu kabisa mahali popote Duniani.

Familia ya namna hiyo inajenga nidhamu ya woga, Utumishi wa kuonwa (eye service), na afya mbovu ya uhusiano.

Familia nzuri yenye afya hukua katika miongozo ya kidemokrasia na nguvu kidogo sana. Nguvu sawa, lakini isizidi majadiliano, upendo, na kutendeana haki.

Moyo wangu unauma sana na sioni hatima ya maana kwa nchi yetu ninaposikia, " hata watu wasio na sifa za kuandikishwa kupiga kura, wanaandikwq na lazima wapige kura. Haya ni Matumizi ya nguvu Sasa. Yaani hata aibu ya kawaida tu imetutoka?. Kwa sababu tu ya maguvu unafanya chochote?

Vipigo kwa watu wanaoonekana kuwa na mawazo tofauti nasi. Kwa Nini? Ina maana tumepoteza nguvu ya ushawishi hata wa hoja?

Na kama hata ushawishi wa hoja umeisha, tunaongozaje sasa?

Nimalizie kwa kujiasa Mimi pamoja na wenzangu tunaoongoza, acheni kuyapa kipaumbele Matumizi ya nguvu kwa Kila jambo kwa sababu ni dalili kwamba "we are becoming irrelevant to matters Leadership.

Unajua Nini? Pole pole, tunaanza kujenga jamii ambayo itazoea mateso, na suluba na Mwisho jamii hiyo itajitafutia namna ya kutoka katika shida hiyo ikifika at the boiling point.

Kiongozi yeyote mzuri, awe wa familia, ukoo, serikali, na hata msikiti au kabisa, hakimbiliii kutumia nguvu bali nguvu ya ushawishi.

Ushawishi ambao ni zao la haki, upendo, kuthamini watu wako, kuishi ktk viatu vyao (Emphacy), kujiheshimu nk ndo mambo yatayosaidia jamii kurudi kwenye mstari wa kuongozwa, nje ya hapo tunatafuta fujo na kujenga usugu kwa waongozwa kuishi bila loyalty kwa wanaoongoza.

Let us come back to our senses, if not, we are going to lead people illegimately that can result into making people rebellious both eternal and external.
 
Kupoteza ni mara moja tu, na tayari huo uhalali ulishaga potea!
 
sasa kwa mfano kwa malalamiko tu kila uchwao utamshawishi nani aungane nawe kulalamikia?

mawazo mapya na fikra mbdala ndiyo chimbuko mahususi la msingi la wa kuchochea ushawishi wa kuvutia wananchi wengi zaidi na sio malalamiko ambayo ni ishara ya wazi ya kukata tamaa.

ni jambo la kawaida kutumia nguvu kadiri ya resistance ya kaidi mwenye kiburi katika kumdhibiti na kumdoofisha.

kutumia nguvu ni kitua ambacho hakiepukiki katika kutuliza vurugu na fujo miongoni mwa wenye amani na utulivu 🐒
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…