Facts1
JF-Expert Member
- Dec 23, 2009
- 307
- 28
Wana JF mimi ni mgeni humu jamvini, katika nchi za wenzetu vyama vya upinzani huitwa a waiting Government au a Coming Government au The Next Government. Hivi vyama tiari huwa vina wasemaji vivuli kwa kila idara. Kwa mfano Uingereza kuna Conservative na Liberal Democrat vote hivi vina wasemaji wazoefu kwa kila idara au wizara.
Hapa nyumbani achilia mbali na mawaziri vivuli wa muungano wa upinzani bungeni, chama kama chama nacho kinatakiwa kiwe na muundo wa serikali yake. Katika chama cha CHADEMA nimekuwa nikiwasikia takribani wakurugenzi wawili au watatu tu wakiwa kama wasemaji wa idara zote.
Kwa mfano nimekuwa nikimsikia zaidi Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa John Mnyika, Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri Jonh Mrema, Sheria na Mambo ya Katiba Tundu Lissu.
Kuna idara nyeti kama Elimu, Afya, Kilimo nk,wako wapi wasemaji wake kama wapo mbona hatuwasikii kwenye masuala yao kama John Mnyika anavyokuwa shujaa kuhoji masuala nyeti kama Tanzania kuhusika na uuzaji wa silaha DRC? Naomba mwenye Idara zote aniletee hapa JF na wakurugenzi wake ikiwezekana na uwezo wao hata elimu zao ikiwezekana.