hakusulubiwa
Member
- Dec 23, 2012
- 37
- 22
Kutoka kwa Abdulrahman Mohamed
INAWEZA KUJITEGEMEA?
Muelekeo wa Makala ya Habari Leo ambao ni wazi Omar Ilyas anauunga mkono kama silaha yake dhidi ya mabadiliko katika muungano ni kuwa Zanzibar inafaidika na Muungano kwa kutochangia, na by implication haitaweza kujiendesha yenyewe. Ndio maana makala hiyo imepewa kichwa cha habari: SERIKALI MBILI HAZIEPUKIKI…
Kwanza nianze kuweka wazi kwamba hakuna nchi ambayo iko self sufficient kiuchumi Duniani. Kuanzia nchi zilizoendelea mpaka zinazoendelea nyingi zinakuwa na deficit katika budget, Tanzania yenyewe ambayo kwenye makala hii imesifiwa kuibeba Zanzibar ina budget deficit, negative balance of payment, high inflation, high unemployment na DGP growth rate isiyotofautiana sana na Zanzibar.
Kwa mujibu ya Hotuba ya Rais Sheni (source iko mwisho) kuhusu Zanzibar GDP growth ninanukuu "ukuaji wa uchumi ulitegemewa kufikia asilimia 7.0 mwaka 2012 kutoka asilimia 6.8 mwaka 2011" (Shein, 2013)
Na kuhusu GDP growth ya Tanzania, Nikinukuu article iliyopelekwa IMF na Waziri wa Fedha pamoja na Gavana wa BOT "MACROECONOMIC DEVELOPMENTS AND PROGRAM PERFORMANCE iliyopelekwa IMF (Iliyoandikwa na Waziri wa Fedha pamoja na Gavana wa BOT) inaeleza "Economic growth remained buoyant during 2012 with a real GDP growth of 6.9 percent, within the projected range of 6.5–7.0 percent" (sourse iko mwisho)
Hivyo basi Tanzania na Zanzibar kiuchumi (kwa mujibu wa takwimu) hakuna tofauti yoyote kubwa.
Naomba nikumbushe kuwa Growth hizi zenye kufanana ni baada ya kuwa Tanzania aka Tanganyika humo humo ina mamlaka ya kimataifa na Zanzibar haina, Tanzania inatoa leseni ya viwanda ambayo Zanzibar hakuna viwanda Bara vipo, Tanzania inachimba madini na gesi na Zanzibar haichimbi chochote…
Je hali halisi ya maisha (ukiondoaTakwimu) Zanzibar iko wapi? Ni ukweli usiopingika kuwa kuna sehemu nyingi za kiuchumi ambazo Zanzibar imedorora mno, mfano Education (Muungano) Zanzibar iko nyuma kupita kiasi na Muungano hakuna hata moja ambalo unafanya, Afya (SMZ) Zanzibar pia ipo nyuma mno na Zanzibar haijaleta mabadiliko makubwa katika eneo hili. Hivyo basi kwa hali ya sasa si Muungano wala si Zanzibar ambayo ni tija kubwa kwa Zanzibar, hali ni mbaya kwenye sekta zote bila ya kujali msimamizi ni yupi kati ya seributu (maana sio serikali) mbili hizi.
Binafsi nigeliona UMUHIMU MKUBWA WA KUENDELEA NA MUUNGANO HUU KAMA ULIVYO KAMA INGELIKUWA LABDA ZANZIBAR INA MAENDELEO KATIKA SEKTA ZA MUUNGANO na imedorora tu katika sekta Zinazoongozwa na SMZ.
Hii ingekuwa hoja tosha ya kuelekea kwenye serikali moja ya Muungano, au kubaki na serikali mbli ili ku-preserve benefit za Muungano kama ulivyo. Lakini Zanzibar imedorora katika Mambo yanayosimamiwa na Muungano na SMZ, Kwa Mfano Elimu ZANZIBAR NDIO INAONGOZA KWA FAILURES. Kwa hiyo argument kuwa serikali mbili ziendelee na ni suluhisho kwa maisha ya Wazanzibari haina nguvu yoyote, kudorora kwake kumechangiwa na seributu zote mbili iwe ni kiuchumi au kisiasa.
Zaidi kwenye mamlaka kamili Zanzibar itatoa fair share katika muungano kwa mujibu wa makubaliano ambayo yatakuwa hayana utata kama uliopo sasa hivi, sasa hivi hatuambiwi Zanzibar inatakiwa kuchangia nini na ki vipi na kwa nini ichangie. Wala hatuambiwi Bara inatumia kiasi gani (nje ya matumizi ya Muungano) Mambo ni mvurugano tu.
Anayedai kuwa Zanzibar haitaweza kujiendesha basi hana muono wa kisiasa wala wa kiuchumi, ni madai ya vitisho ya kuwafanya Wazanzibari ambao wengi wameonyesha kuvutiwa Zaidi na serikali tatu na muungano wa mkataba (kama maoni yalivyoonyesha) waogope kuendelea na ajenda ambayo tunajua wazi kuwa watawala (CCM) hawataki wanachokitaka wananchi wa Zanzibar.
Ikiwa Zanzibar inaweza kuwa ilivyo leo bila ya kuwa na vyombo vyenye kusimamia sera muhimu kama vile urari (inflation), ukosefu wa ajira, bila ya kuwa na sarafu yenye ku-reflect economic situation, bila ya kuwa na chombo cha kusimamia fiscal na monetary policiies, bila ya kuwa na international trade yenye kuinufaisha Zanzibar moja kwa moja, bila ya kuwa na mamlaka mengi muhimu ya kuendesha uchumi, iweje Zanzibar kesho ishindwe kujiendesha ikiwa na mamlaka hayo?
Na hii hapa sehemu ya Zanzibar kutoka International Grants kwa mujibu wa Gavana na Waziri wa Fedha wa serikali ya Muungano:< < Foreign grants and financing. Total grants were higher than projected due to more than- expected front-loading of general budget and basket grant disbursements. The Government contracted [US$1,363 million] in ENCB, of which US$1,165 million was for the gas pipeline, US$178 million for the Dar es Salaam water project, and US$20 million being the foreign currency component of a government-guaranteed loan for TANESCO (amounting in total to US$65 million). >> (Source iko chini)
Sidhani kama nina haja ya kueleza kuwa katika mamilioni haya ya Dola Zanzibar ilipata sifuri (ingawa wengi wanajaribu ku-play down umuhimu wa mamlaka ya kimataifa, lakini huwa hawayajui haya au wanafanya kusudi kama propagandist, pipe ya gesi haituhusu, na TANESCO ni ya Bara sio ya Muungano sisi ni wateja tu. Tunapoyasema haya kuwa wanaotaka sisi tuonekane hatuna akili, wabaguzi, hatuupendi muungano na mambo ya kipuuzi kama hayo.
Hivyo tusidanganyane kuwa kiuchumi Zanzibar inaitegemea Bara kwa asilimia kubwa na kuwa Zanzibar haitaweza kujiendesha.
KWA WASTANI WA IDADI YA WATU ZANZIBAR INAKUSANYA KODI ZAIDI YA TANZANIA/TANGANYIKA
Omar Ilyas zifuatazo ni takwimu za Makusanyo ya Kodi Zanzibar Vs Tanzania pamoja na uchambuzi wake (Nakupa jibu la zaidi ya ulivyouliza)
Kwa Mujibu wa TRA Tax Collection Statistics Makusanyo ya Kodi Tanzania nzima ni:
Tshs 1,722,728,400,000 (Source nitaiweka chini) kwa mwaka 2011/2012.
Kwa Mujibu wa Hotuba ya Rais Sheni ninanukuu "Aidha, ukusanyaji wa mapato ya ndani umeongezeka kutoka T.Shs. 181.4 bilioni mwaka wa fedha 2010/2011 na kufikia T.Shs. 212 billioni mwaka 2011/2012. Hili ni ongezeko la asilimia 17. " (Shein, 2013) Reference nitakuwekea chini.
Sasa naomba niweke hizi figure na kulinganisha na population ili kujua Zanzibar na Tanzania ni ipi inakusanya kodi zaidi.
Source mbili hizi zimeainisha kwamba:
Tanzania (including Zanzibar) kodi ni TSh 1,722,728,400,000
Zanzibar Only: TSh 212,000,000,000
Tanzania ina watu 44,928,923 (Census Result Brief Report, 2012)
Zanzibar ina watu 1,303,569 (Census Result Brief Report 2012)
Sasa hebu tuone Wazanzibari na Watanzania (Including Zanzibar) ni wepi wana uwiano mzuri wa malipo ya kodi kwa idadi ya watu.
Kwa kifupi hii hapa formula
Tanzania = Kodi iliyokusanywa Tanzania ÷ Idadi ya Watu Tanzania
Zanzibar = Kodi iliyokusanywa Zanzibar ÷ Idadi ya Watu Zanzibar
Majibu yatatoa ni ipi ina wastani mzuri wa kodi.
Tanzania >> 1,722,728,400,000 ÷ 44,928,923 = 38,343.42
Zanzibar >> 212,000,000,000 ÷ 1,303,569 = 162,630.44
Ikiwa Rais Shein, TRA na Takwimu za National Board of Statistics wako sahihi wastani wa kodi iliyolipwa na kila Mzanzibari mmoja ni TShs. 162,630.44
Na ikiwa Takwimu hizo ni sahihi pia basi Wastani wa kulipa kodi kwa kila Mtanzania ni Ths 38,343.42Pia tuangalie ni mara ngapi zaidi Mzanzibari kodi yake inaizidi Mtanzania:
162,630.44 ÷ 38,343.42 = 4.24
Hii ina maana Wazanzibari wanalipa kodi mara nne zaidi ya Watanzania kiwasatani. Omar Ilyas kama wewe ni mweledi wa hesabu nadhani utakuwa umeshajua kwamba ukiondoa mchango wa Zanzibar katika Tanzania basi Tanganyika itakuwa na mchango mdogo zaidi kiwastani. Nadhani hii ndio sababu ya msingi ya takwimu za kila upande kutokwekwa wazi, kimatumizi, ukusanyaji wa kodi na mapato, kisha tunadanywa na wewe Omar unadanganyika kama kilivyosema kichwa cha habari zilzioandikwa kwenye "Habari Leo" kwamba "UCHUMI WA ZANZIBAR UNATEGEMEA BARA"
Uzandiki na propaganda hizi zitawalevya waliokwisha kulewa sio sisi. Nasubiri majibu yangu na hasa maswali haya mawili:
1. Ni kiasi gani cha Bajeti ya Tanzania kinatumika kwenye shughuli za Muungano?
2. Ni kasi gani cha matumizi hayo kinakwenda kwenye shughuli za T Bara zisizo za Muungano?
3. Ni kiasi gani cha matumizi hayo ya Muungano yanatumika moja kwa moja kwenye shughuli za Muungano upande wa Zanzibar.
Sio tu ujue kuuliza Omar na kujibu pia.
Reference
Hotuba ya Rais Shein Katika Maadhimisho ya Muungano
http://www.google.co.uk/url?sa=t&rct=j&q=&esrc=s…😉
Tanzania: Letter of Intent, Memorandum of Economic and Financial Policies, and Technical Memorandum of Understanding (By Tanzania Minister of Finanace and Governor of BOT)
http://www.imf.org/external/np/loi/2013/tza/051713.pdf
HOTUBA YA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI,MHESHIMIWA DK. ALI MOHAMED SHEIN,KATIKA MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 49 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR,TAREHE 12 JANUARI, 2013. inapatikana
http://www.facebook.com/l.php…
TRA Website (2014), Tax Collection Statistics, available from http://www.tra.go.tz/…/Copy of TRA Quarterly…
Souece: Makala haya nimeyatoa kutoka Mzalendo.net