Kakke
JF-Expert Member
- Dec 4, 2010
- 1,883
- 1,482
[h=1][/h]
Muhariri wetu Joseph Mihangwa
KATIKA sehemu ya kwanza ya makala haya, tuliona misingi mikuu inayopaswa kufuatwa katika kutunga Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuzingatia na kuongozwa na Mkataba wa Muungano wa 1964, ambao Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Jaji Joseph Sinde Warioba imejitahidi kuzingatia.
Aidha tuliona pia kazi ya Bunge la Katiba, ambapo kwa mujibu wa Sheria ya Muungano Namba 22 ya 1964, kifungu cha 9 (1) ni Kuridhia (rasimu) na kukubali (to ratify and adopt) Katiba ya Serikali ya Jumhuri ya Muungano.
Tuliona pia aina ya muundo uliokusudiwa na jinsi, kwa kutumia wanasheria wa nchi za Magharibi (Roland Brown, Fifoot), matakwa ya Mkataba huo yalivyopindishwa kwa kufifisha uhuru (autonomy) na sura au utambulisho (identity) wa Zanzibar uliokusudiwa chini ya Mkataba, na hivyo kumfanya Rais wa Kwanza wa Zanzibar, hayati Abeid Amani Karume acharuke kutaka kususia Muungano.
Sababu kubwa ni kwamba, Karume alitia sahihi Mkataba wa Muungano (kwa kutegeshewa?) bila kujua maudhui na yaliyokuwamo kwenye Mkataba. Upo ushahidi kwamba, aliwaonesha Mkataba huo baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi baada ya kueleweshwa vyema na Dounado kuhusu yaliyokuwamo nao hawakuridhika; kisha akasema, Kama hamuutaki (Mkataba huu), nitaurudisha kwake (Nyerere). Licha ya kutoridhiwa na Baraza hakupata kuurudisha.
Na baada ya kubaini jinsi alivyochengwa kufikia Muungano na utekelezaji kinyume na alivyotarajia, Karume alitupilia mbali kila kitu na kuwa mtu wa kujihami daima dhidi ya Muungano kutaka kufifisha mamlaka yake. Aliitawala Zanzibar kama nchi huru kwa ndani, hata kwa mambo yaliyopaswa kushughulikiwa na Muungano. Kilichoibuka ni Kero za Muungano ambazo zimedumu hadi leo.
Niharakishe kusema hapa kwamba, uhasama wa viongozi hawa wawili ulisababisha uteuzi wa Tume ya Katiba na Bunge la Katiba lililopaswa kuitishwa ndani ya mwaka mmoja kupitisha Katiba ya Muungano lisiteuliwe hadi wakati mwingine mwafaka.
Bunge hilo, kwa mujibu wa Mkataba, ndilo hili linaloendelea hivi sasa Mjini Dodoma. Ni kusema kwamba, kwa miaka 50 ya Muungano, Tanzania imetawaliwa kwa Katiba zilizopatikana kwa taratibu zisizozingatia matakwa ya Muungano.
Kero ni nyingi, lakini kero ya kwanza ya Muungano ilikuwa Mei 19, 1964 wakati aliyekuwa Waziri wa Biashara na Viwanda wa Muungano, Kassim Hanga, alipohudhuria Baraza la Huduma za pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACSO) mjini Nairobi kama Mwakilishi wa Tanzania.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, iliyosomwa na mteule wake, aliyekuwa Rais wa Kenya wa wakati huo, Jomo Kenyatta, hakuficha furaha yake kwamba, kufuatia Muungano wa Tanzania, Zanzibar haitashiriki tena kama Mtazamaji (Observer) bali kama Tanzania.
Ikumbukwe kuwa, kuanzia miaka ya 1963, wakati Mwalimu Nyerere akipigia chepuo kuundwa kwa Shirikisho la Afrika Mashariki hadi liliposhindwa Aprili 10, 1964, Zanzibar ilihudhuria vikao hivyo kama mwalikwa mtazamaji.
Hanga akagutuka, na usiku huo akampigia simu Karume kumjulisha hilo. Kwa hasira, Karume akamwagiza Hanga kurejea Zanzibar (sio Dar es Salaam iliyomtuma) mara moja kwa kile kilichoitwa Zanzibar haikuhitaji EACSO, na kuacha mkutano ukiendelea.
Pigo kubwa la pili kwa Muungano kwa mkono wa Karume ni pale alipopitisha (Amri) Sheria (Decree) kufanya ASP kuwa Chama pekee chenye mamlaka ya juu kuliko vyombo na taasisi zote Visiwani. Hiyo ilikuwa Mei 11, 1965 miezi, miwili tu kabla Tanzania kuwa nchi ya Chama kimoja. Chini ya amri hiyo, Chama cha ASP kiliunganika na Serikali kuwa ndicho Serikali na Serikali kuwa ndiyo ASP.
Chini ya amri hii pia, Karume alianzisha idara saba ambazo ni Jeshi, Polisi, Usalama, Vijana, Wafanyakazi, Wanawake na Wakulima, zikiongozwa na Wakuu wa Idara wa kuteuliwa na yeye mwenyewe, kwa kushauriana na Baraza la Mapinduzi.
Lengo lilikuwa ni kuhamisha kwa staili yake, mamlaka ya vyombo vya ulinzi Visiwani kama Jeshi, Polisi na Usalama, kutoka kwenye Muungano kuwa ndani ya mamlaka ya Wazanzibari.
Na ndivyo ilivyokuwa kwa Mahakama, pale Zanzibar ilipoanzisha muundo wake wa Mahakama na kujitoa kwenye Mahakama ya Rufani ya Afrika Mashariki, na baadaye hukumu za Mahakama za Kizanzibari kutokatiwa rufaa kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania. Kwa baadhi ya hukumu, Karume mwenyewe alikuwa na mamlaka ya mwisho.
Jambo lingine lililotikisa Muungano wakati wa Karume, lakini akashindwa kwa kunaswa kwa mtego wa kisheria, lilihusu mambo ya Benki na Fedha.
Wakati wa enzi za ukoloni, nchi za Tanganyika, Kenya, Uganda na Zanzibar ziliunda, kwa njia ya hisa, Taasisi ya sarafu Afrika Mashariki (East African Currency Board) EACB, iliyosimamia sarafu chini ya usimamizi wa Waziri wa Makoloni wa Uingereza.
Nchi wanachama zilistahili gawio la faida na haki ya kukopa kutoka EACB. Baada ya uhuru, usimamizi wa EACB uliwekwa mikononi mwa serikali za kila nchi zilizowakilishwa EACB, ikiwamo Zanzibar.
Lakini kwa Zanzibar, hata hivyo, Muungano kati yake na Tanganyika kuwa nchi moja kulibadili mambo kufanya kutokuwa na uwakilishi EACB. Japokuwa jambo ya fedha na mabenki hayakuwa ya Muungano, kama ambavyo pia Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha wa wakati ule, D. Namfua alivyokiri, katika barua yake kwa utawala wa nchi, Kumb. TYC/46/01/502 ya Juni 9, 1964, kwamba Zanzibar ingeweza kushiriki kwa mwavuli wa Ushirikiano wa kimataifa, lakini Namfua hakuelewa kwamba kwa sababu Mambo ya Nje lilikuwa jambo la Muungano, na Zanzibar haikuwa Taifa licha ya kuwa nchi isiyo dola, isingeweza kushiriki.
Kufuatia kushindwa kwa juhudi za kuunda Shirikisho la Afrika Mashariki, nchi zote tatu, isipokuwa Zanzibar ambayo sasa ilikuwa Tanzania, ziliamua kuanzisha Benki Kuu na sarafu zake.
Hapo, mgogoro wa ndani ukazuka juu ya mambo matatu: Kwanza, kama Zanzibar ilistahili kupokea na kunufaika na hisa zake za EACB baada ya kuvunjika kwa EACB; pili, nafasi na wajibu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) tarajiwa kwa mambo ya Fedha ya Zanzibar. Na tatu, nini kingezuia Zanzibar kuanzisha Benki Kuu na sarafu yake, ikizingatiwa kwamba mambo hayo hayakuwa ya Muungano?
Wakati maswali haya yakiwa bado hayajapata majibu, Karume alianza mchakato wa kuanzisha Benki Kuu ya Watu wa Zanzibar yenye mamlaka na udhibiti wa akiba ya fedha ya Zanzibar.
Na kwa kasi ya pekee, akahamisha akiba ya paundi za Uingereza 700,000 kutoka Benki Grindlays ya Uingereza kwenda Benki Norodony Moscow, tawi la London, ili fedha hiyo isiweze kufikiwa na Benki za Uingereza, nchi ambayo ilikuwa nyuma ya (hila za) Muungano, wala zisinyakuliwe na Serikali ya Muungano.
Karume ategeshewa
Kwa hili, na kutokana na ukweli kwamba Fedha halikuwa jambo la Muungano, hoja ya Zanzibar ilikuwa na mantiki nzito. Lakini Serikali ya Muungano haikutaka kuona Zanziabar ikiwa na Benki yake. Hapo tena, magwiji wa sheria wa Mwalimu Nyerere, wakiongozwa na Roland Brown, aliyepata kuandaa Mkataba na Sheria tata ya Muungano yenye makengeza ya nyoka mwenye sumu kali, wakaingia kazini kudhibiti mbio za Karume.
Ukaandaliwa Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba ya Muda, kufanya Sarafu, fedha za Kigeni na udhibiti wa ubadilishanaji fedha, kuwa mambo ya Muungano, na kuwasilishwa Bungeni Juni 10, 1965, na kupitishwa siku hiyo hiyo.
Kana kwamba alikuwa ametegeshewa ajikaange mwenyewe, Karume, wakati huo akiwa Kaimu Rais wa Jamhuri ya Muungano wakati Mwalimu akiwa nje ya nchi, alipewa Muswada huo uliopitishwa na Bunge na kuutia sahihi siku hiyo hiyo kuwa Sheria Namba 21 ya 1965, na kuanza kutumika siku hiyo hiyo.
Kama ambavyo alivyotia sahihi Mkataba wa Muungano mwaka 1964 bila kujua alichokuwa akitilia sahihi, vivyo hivyo safari hii tena, Karume hakujua nini alichokuwa akitilia sahihi. Hata wabunge wa Bunge la Muungano kutoka Zanzibar hawakubaini madhara kwa Zanzibar, kwa kile walichokuwa wakipitisha.
Baada ya kutia sahihi Muswada huo na kurejea Zanzibar, alielezwa na Dourado jinsi sheria aliyotia sahihi ilivyokuwa na athari kubwa kwa maslahi ya Zanzibar, na kwamba asingefanya lolote kwa sababu ilikwishakuwa sheria.
Bila kujali yaliyotokea, Karume aliendelea na mchakato wa kuanzisha Benki ya Watu wa Zanzibar kwa kuteua Tume ya Benki ya kupendekeza Muundo na Mamlaka ya Benki, iweze kufanya kazi za Benki Kuu na kutambuliwa hivyo na Sheria za Muungano.
Kuanzishwa kwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) mwaka 1966 kulimkata ngebe Karume na mbio za kuanzisha Benki ya watu wa Zanzibar. Wazanzibari walilowa, pale Nyerere, kwa mamlaka aliyopewa chini ya ibara ya 5 (b) ya Mkataba wa Muungano, na kifungu cha 8 (2) cha Sheria ya Muungano kama tulivyoona mwanzo, alipotoa Amri kwamba, Sheria ya Tanganyika ya Benki na Fedha za Kigeni (Cap 139) itumike pia Zanzibar.
Hoja za Wazanzibari zikaendelea kupata majibu ya uhakika. Katika waraka wake kwa uongozi wa Zanzibar, Kumb. TYC.46/01 wa Machi 22, 1966; aliyekuwa Waziri wa Fedha wa wakati huo, Amir Habib Jamal, alisema yote kwamba, kuanzia wakati huo, ni Gavana wa BOT pekee ndiye atakuwa kwenye Bodi ya EACB, na Zanzibar haitawakilishwa.
Pili, kwamba mgawo wa rasilimali na mtaji, na au faida iliyopatikana kutokana na Tanganyika na Zanzibar kuwekeza katika EACB italipwa Serikali ya Tanzania. Tatu, kwamba, michango yote pamoja na riba iliyolimbikizwa na Zanzibar italipwa na Hazina ya Tanzania.
Nne, kwamba, baada ya EACB kuvunjwa na mali kugawanywa, mali ambazo vinginevyo zingekwenda Zanzibar, zitachukuliwa na Serikali ya Muungano. Tano, ilifanywa marufuku kwa Zanzibar kuanzisha Benki Kuu, lakini ikaruhusiwa kuanzisha Benki ya kawaida kwa Sheria za Zanzibar, mradi tu benki hiyo isifanye kazi zilizo mahsusi kwa Benki Kuu.
Zanzibar haikamatiki
Ilikuwa rahisi kuidhibiti Zanzibar enzi za udikteta wa chama kimoja na hekima za mkono wa chuma za Mwalimu Nyerere na umbumbumbu wetu, kuliko enzi hizi za uamsho (re-awakening), demokrasia, sayansi na teknolojia.
Ni ujinga kuficha Mkataba wa Muungano kwa kuwaambia wanaouhitaji kwamba haupo, na eti kwamba wanaotaka kuona nakala yake waende Umoja wa Mataifa ulikohifadhiwa!
Kwa ujumla, kiburi na kejeli za hayati Karume kwa Muungano zilikuwa za msingi kama tunavyobaini sasa kutokana na lundo la kero za Muungano mbele yetu. Pamoja na udikteta wake, lakini kama kuna kitu Wazanzibari kinachofanya wamheshimu na kumtukuza mwasisi huyo wa Taifa la Zanzibar na Muungano, ni Uzanzibari na ungangari wake wa kutotaka kuburuzwa kwa mambo yaasiyo ya Muungano.
Wasomi na Serikali mbili au tatu
Wasomi wa Sheria, Sayansi ya Jamii na Siasa wanaelewa fika kwamba Muungano uliokusudiwa ni wa Shirikisho, lakinii kwa kujipendekeza kwa wanasiasa na kutojiamini, wakati mwingine wanakubali kusaliti taaluma zao kusimamia serikali mbili; huku ukweli na historia ukiwasuta.
Profesa wa Sheria, B.P. Srivastava, katika The Constitution of the United Republic of Tanzania Some Salient Features, some Riddles (East Africa Law Review 1981 83), anabainisha Muundo sahihi wa Muungano kwa kusema, Jamhuri ya Muungano iliyokusudiwa ni ya muundo wa pembe tatu, ambapo Tanganyika na Zanzibar zinaunda kona mbili za kitako, na Jamhuri ya Muungano inaunda kizingia (vortex).
Naye gwiji la Sheria na Mwanasheria Mkuu wa kwanza wa Zanzibar huru, ambaye mwaka 1964, kwa uelewa wake wa Sheria, alitupwa nje kila mara wakati wa mchakato wa Muungano, Wolfgang Dourado, katika andiko lake The Consolidation of the Union: A basic Re-appraisal (mada kwenye Semina ya Chama cha Wanasheria cha Tanganyika, 1983) anasema: Watu wengi, wakiwamo viongozi wa Chama na Serikali, wanashindwa kufahamu kwamba, Serikali ya Muungano yenye kutekeleza mamlaka juu ya mambo ya Muungano kwa eneo lote la Muungano, ni serikali tofauti na ile ya Muungano inayotekeleza mamlaka kwa mambo yasiyo ya Muungano kwa ajili ya na ndani ya Tanganyika.
Kwa mantiki hii, kuna serikali tatu, kwa maana ya Serikali ya Muungano inayotekeleza pia mambo ya Tanganyika yasiyo ya Muungano, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Muungano kwa ajili ya Mambo ya Muungano.
Profesa Issa Shivji, gwiji lingine la sheria nchini, ambaye siku za karibuni ameonekana kujichanganya kwa kutetea Muundo wa Serikali mbili, anakiri Muungano wetu ni wa Shirikisho lenye serikali tatu.
Katika kitabu chake, The Legal Foundations of the Union (uk. 37 na 39) anasema: Wakati Wazanzibari wako chini ya Serikali mbili Serikali Kuu ya Muungano na Serikali ya kikanda ya Zanzibar kama ilivyo kwa Shirikisho lolote lile, Watanganyika wao wako chini ya Serikali moja; lakini ni sehemu tu ya serikali.
Kwa kuziweka pande zote pamoja, na kwa kuitazama Sheria ya Muungano ilivyo, nawasilisha kwa uhakika kwamba, msingi wa kishirikisho unaotawala Sheria ya Muungano wetu ni aina ya Katiba ya Shirikisho.
Akimnukuu aliyekuwa Jaji Mkuu wa India, Sikri, katika kesi ya Kesavananda, Shivji anasema: Yatakuwa marekebisho haramu, kama yatafanyika (na yaliyofanyika), kubadili msingi, muundo au maudhui muhimu ya Katiba (Mkataba wa Muungano) kuhusu yafuatayo: Ukuu wa Katiba (Mkataba wa Muungano), Jamhuri na udemokrasia wa Serikali, Katiba isiyo ya kidini, mgawanyo wa madaraka kati ya Bunge, Utawala na Mahakama; na mwisho, Muundo wa kishirikisho wa Katiba.
Anasema: Muundo wa Serikali ya kishirikisho unaoainishwa katika kifungu cha 5 cha Sheria ya Muungano, ndio msingi mkuu wa watu wa Tanganyika na Zanzibar kuungana . Kamwe, upande mmoja wa Muungano hauna mamlaka kubadili mgawanyo wa madaraka na Msingi wa Muungano, na kwamba kitendo kama hicho ni batili.
Shivji anamaliza kwa kupigilia msumari (uk 45) akisema: Kuongezwa kwa mambo ya Muungano kulikofanywa kwa AMRI ya Rais na Bunge, ni kitendo haramu cha kubaka madaraka na kudhalilisha msingi mkuu wa Muungano; ni kinyume cha msingi unaotawala mfumo wa Shirikisho kuweza kubomoa msingi wa Muungano.
Wazanzibari wasaliti wa Muungano?
Mengi yamesemwa juu ya Zanzibar kuwa na Katiba yake inayotambua, pamoja na mambo mengine makuu, Zanzibar kujitambua kama nchi yenye mipaka kamili, na kwamba nchi hiyo ni miongoni mwa nchi mbili (iko wapi ya pili?) zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Na kwa mujibu wa ibara ya 132 ya Katiba hiyo, Sheria za Muungano zilizopitishwa na Bunge la Muungano sharti zijadiliwe na kuridhiwa na Baraza la wawakilishi kama njia ya kukomesha tabia iliyozoeleka ya kupanua orodha ya mambo ya Muungano.
Yote haya ni kwa Zanzibar kutaka kuona Zanzibar na Tanganyika zinakuwa nchi zenye mamlaka kamili kwa mambo yasiyo ya Muungano. Kwa hilo hatuwezi kuwabandua, piga-ua, hata kama ni kwa kura ya wazi au ya siri.
Kwa mtazamo wa juu juu, huu unaweza kuonekana kama usaliti wa Wazanzibari kwa Muungano, lakini kilichofanyika na wanachofanya ndio ukweli wenyewe, kwamba Muungano wetu ni wa kishirikisho na hauwezi kubadilika maadam Mkataba wa Muungano na Sheria ya Muungano zipo na zinataka hivyo. Mengine yote na kinyume cha hayo ni uhafidhina wa kisiasa usiopenda kutambua na kukiri ukweli.