Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Huku mivutano kuhusu muundo wa muungano ukiendelea, nimefazifanyia tathmini ndogo kero za muungano kwa pande zote, nikajiridhisha pasi shaka, kuwa Jaji Warioba yuko very right!, muundo wa serikali mbili, licha ya kushindwa kumaliza kero za muungano kwa kipindi cha miaka 50 iliyopita!, hivyo nimejiridhisha kuwa muundo wa serikali mbili, kamwe, hauwezi kutatua kero hizo, hata zikipewa kipindi cha miaka 100 mingine!. Dawa ya kudumu ya kupunguza kero hizo, japo sio kuzimaliza kabisa ni serikali 3, ila suluhisho la kudumu, na dawa ya kutibu kwa kuzimaliza kabisa, kero za muungano, ni serikali moja! ambayo inaunda nchi moja chini ya rais mmoja!.
Naomba niwapitishe very briefly kwenye baadhi ya kero hizi.
Huku mivutano kuhusu muundo wa muungano ukiendelea, nimefazifanyia tathmini ndogo kero za muungano kwa pande zote, nikajiridhisha pasi shaka, kuwa Jaji Warioba yuko very right!, muundo wa serikali mbili, licha ya kushindwa kumaliza kero za muungano kwa kipindi cha miaka 50 iliyopita!, hivyo nimejiridhisha kuwa muundo wa serikali mbili, kamwe, hauwezi kutatua kero hizo, hata zikipewa kipindi cha miaka 100 mingine!. Dawa ya kudumu ya kupunguza kero hizo, japo sio kuzimaliza kabisa ni serikali 3, ila suluhisho la kudumu, na dawa ya kutibu kwa kuzimaliza kabisa, kero za muungano, ni serikali moja! ambayo inaunda nchi moja chini ya rais mmoja!.
Naomba niwapitishe very briefly kwenye baadhi ya kero hizi.
- Kutokuwa na Uwazi wa Mapato na Matumizi wa Fedha za Jamhuri ya Muungano, kwa sababu serikali ya Muungano pia ndio serikali ya Tanganyika!, hakuna any dividing line zipi ni gharama za Tanganyika na zipi ni gharama za muungano!, serikali mbili haziwezi kutatua hili milele!. Dawa ni ama serikali tatu hivyo gharama za Tanganyika zitajulikana, and the same applies to mapato, kwa sasa Tanganyika pekee ndio tunagharimia muungano!, Its about time sasa kila mtu aubebe mzigo wake mwenyewe!.
- Kutokuwa na Akaunti ya Pamoja. Hili lilishindikana kwa sababu fedha za Tanganyika pia ndizo pekee zimekuwa zikigharimia muungano!, uwe na account ya pamoja ya nini wakati Zanzibar haitoi single cent?. Serikali tatu ndio suluhisho la tatizo hili account itafunguliwa Serikali ya Tanganyika itatiamo fedha na Zanzibar italazimika, huu ndio utakuwa mwisho wa dezo dezo!.
- Uwepo wa Mkanganyiko wa Mapato jinsi ya kuchangia gharama uendeshaji wa Serikali zote mbili utamalizwa kwa kuinyofoa serikali ya Tanganyika ndani ya serikali ya muungano!.
- Kuwepo kwa Tume mbili zinazoshindana katika Nchi moja pia kutaondolewa kama kila mtu atakuwa kivyake vyake!.
- Zanzibar kutoshirikishwa kikamilifu na Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika mchakato wa kupata misaada kutoka kwa Nchi za nje nako pia kutamalizikia kwa sababu misaada sio jambo la muungano, kwa sasa tunawapa Zanzibar asilimia 4.5 ya misaada yote ya Tanzania!. Kila mtu atajitafutia, na huu ndio utakuwa mwisho wa watu kujivunia wasichokipanda, kujipakulia wasichokipika, na kujilia vya watu!.
- Malalamiko kuwa Viongozi Wakuu wa Zanzibar wanachaguliwa Dodoma na sio Zanzibar nako pia kutaisha, mambo yote ya Zanzibar sasa yatakuwa yao wenyewe!.
- Zanzibar kulalamika kuwa kuna baadi ya mambo yamefanywa kuwa ya Muungano kupitia kutungwa kwa Sheria ya Bunge la Jamhuri ya Muungano na baada ya hapo mambo hayo huwa katika utatanishi, hili nalo litakwisha.
- Kitendo cha Zanzibar kuwa nchi huru, inabendera yake, ina wimbo wa Taifa, Serikali yake na imebadili Katiba yake kutambuliwa kama Nchi kutamalizwa kwa serikali moja!, serikali mbili au tatu, haziwezi kutatua hili, huwezi kuwa na muungano wa nchi mbili halafu bado zikabaki nchi mbili!.
- Kitendo cha Zanzibar kubadili masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ambayo inasema Sheria za Muungano zinazotungwa na Bunge hilo,zitumike sehemu zote, badala yake Katiba ya Zanzibar inaelekeza kuwa ili Sheria
- itumike Zanzibar Sharti ipelekwe kwenye Baraza la Muungano ni lazima kikemewe na kuadabishwa!. Katiba ya JMT ndio supreme!. Hili pia haliwezi kumalizwa na serikali mbili wala tatu, bali dawa ya hili ni serikali moja!.
- Hili la Zanzibar kutunga Sheria kuhusu Fedha, ambalo ni suala lililopo kwenye Katiba ya Muungano pia litamalizwa na serikali moja!.
- Hili la Zanzibar kutunga Katiba ambayo imechukua Madaraka ya Rais yaliyopo kwenye Jamhuri ya Muungano,inaeleza kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano anamadaraka ya kugawa Nchi katika maeneo ya Kiutawala, mabadiliko ya kumi ya Katiba ya Zanzibar ya 1984 yametambua kuwa Zanzibar ni Nchi na yamempatia Rais wa Zanzibar mamlaka ya Kuigawa Nchi katika meneo ya Muungano litamalizwa kwa serikali tatu!.
- Hili la Katiba ya Zanzibar inaeleza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi mbili lakini Katiba ya Jamhuri inaeleza kuwa Tanzania ni Nchi moja haliwezi kumalizwa kwa serikali mbili, bali serikali moja, nchi moja!.
- Masharti ya Katiba yaliyowekwa kwenye Katiba ya Zanzibar kuhusu Mchango wa Zanzibar katika mambo ya Muungano yamepingana na masharti ya Muungano, hili linaweza kumalizwa kwa serikali 3, kila nchi kuchangia serikali ya muungano, na kiwekwe kipengele expressly kuwa kuchangia muungano ni lazima!, sio favour na hakuna options wala kugomea!.
- Muundo wa Muungano uliopo umepoteza kutambulisho Kihistoria Tanganyika kuhusu watu wa Tanganyika kupitia maslahi yao, hili dawa yake ni serikali tatu.
- Hili la Wananchi wa Tanzania Bara, kutokuwa na haki ya kumiliki Ardhi,wakati wenzano wa upande wa Zanzibar wanahaki ya kumiliki Ardhi Tanzania Bara linaweza kumalizwa kwa serikali moja ila its very unfortunately, mbia mmoja ni landless, wakati mwingine ana ample land!.
- Hili la Wabunge wa Zanzibar huchangia mijadala ya Muungano na ambayo kwa uhakika wake ni mambo ya Tanganyika na kwamba Wabunge wa Tanganyika hawana nafasi ya kuchangia katika Baraza la Wawakilishi.
- Kwa mujibu wa Sheria ya Mzanzibari ya mwaka 1985 Watanzania ambao ni Watanzania wa Bara kutakiwa kutimiza masharti Maalum ili kupata haki ya kiraia wakati Mzanzibari hutakiwi kupata haki hiyo bila masharti yeyote,haki hiyo ni pamoja na kugombea Uongozi, litamalizwa kwa serikali 3!.
- Kitendo cha selfishness Zanzibar kuendelea kuushikilia utaifa wake, wakati Tanganyika tuliupoteza, kutamalizwa kwa serikali moja, hivyo kuwakata kabisa vilimilimi, ghubu na makelele kibao kuhusu muungano.
- Sambamba na hizi kero kubwa kubwa, kuna vikero vingine vidogo vidogo, vyote vitamalizika kwa nchi moja, serikali mmoja, rais mmoja!.