informer 06
Member
- May 11, 2024
- 66
- 49
Afisa kutoka Wizara ya Afya, Asnath Mpelo amesema kuwa Serikali ipo katika hatua za mwisho kuanza kutoa mafunzo ya shahada ya juu ya uuguzi wa afya ya akili, ikiwa lengo ni kufikisha huduma hizo za kibobezi katika ngazi chini kwenye jamii.
Ameyasema hayo leo June 20, 2024 wakati wa utoaji wa taarifa kwa umma kuhusu maandalizi maadhimisho ya kumbukuzi ya kifo cha hayati Benjamin Mkapa aliyewai kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya Tatu, maadhimisho ambayo yanaratibiwa na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation kwa kushirikiana na Serikali.
"Kama Wizara tuna mpango, tupo kwenye hatua za mwisho kabisa ambapo tutaanza kutoa mafunzo ya diploma ya juu kwenye fani zenye upungufu mkubwa, kwa mfano tatizo la huduma ya afya ya akili, tutaenda kuanza mafunzo rasmi kwa shahada ya juu au diploma ya juu ya uuguzi katika eneo la afya ya akili" amesema Asnath
Ameongeza kuwa wataalamu hao watawezesha mpango kushushwa huduma za kibobezi katika ngazi za chini hali ambayo itasaidia wananchi kuepuka gharama za kwenda kupata huduma hizo kwenye hospitali za ngazi ya juu ikiwemo Rufaa na ngazi ya Taifa.
"Ambapo tunategemea watumishi hao watashuka chini kuweza kutoa huduma za afya ya akili za kibobezi katika ngazi za msingi kabisa kabla ya kukimbilia na kupata usumbufu wa gharama kubwa kufuata huduma hizi kwenye hospitali za Rufaa na mikoa na za juu zaidi."amesema Asnath
Akizungumza akiwa Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya amesema kuwa kumekuwepo na upungufu wa watumishi katika sekta ya Afya lakini jitihada mbalimbali zimekuwa zikifanywa na Serikali kwa kushirikiana na wadau ikiwemo taasisi ya Benjamin Mkapa katika kuleta ufumbuzi.
"Tunashukuru Serikali kupitia Rais Samia Suluhu Hassan kwa mwaka wa fedha 2023/2024 tumeweza kupata kibali cha ajira cha watumishi takribani elfu 13,187 wameajiriwa ili kuweza kuziba pengo hilo (uhaba wa wahudumu wa afya ) lakini ajira za mikataba zaidi ya watumishi elfu nne wameweza kuajiriwa. Na ninaweza nikasema juhudi hizi zimefanywa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wa sekta wakiwemo Mkapa Foundation"amesema Asnath
Mwakilishi huyo amesema kuwa kulingana na kauli ya Waziri mwenye dhamana anayeiongoza Wizara ya Afya, Ummy Mwalimu ni kuwa wanakabiliwa na uhaba wa watumishi wa Afya kwa asilimia 65.
Aidha akizungumzia mchango wa taasisi ya Mkapa Foundation kwenye sekta ya afya sambamba na maandalizi kuelekea maadhimisho ya kumbukuzi hiyo , Afisa Mtendaji Mkuu, Benjamin Mkapa Foundation (BMF), Dr. Ellen Mkondya Senkoro amesema kuwa tokea kuanzishwa kwa taasisi hiyo wamekuwa wakishirikiana na Serikali kutoa ajira za mikataba kwa watumishi wa afya katika ngazi mbalimbali.
"Kwa miaka 18 tokea tumeanza tumeishaajiri wataalamu kwa ajili ya vituo, takribani 7,000 ingawa pia tumeongeza jitihada za kuajiri watumishi wa afya ngazi ya jamii takribani 600 kwa ujumla wake ni elfu 13,000 tumeshatoa hizo ajira."amesema Dr. Ellen
Ameongeza "Na kwa mwaka huu tu tumetoa ajira za mkataba karibia 2097 za wataalamu wa afya kwa maana kuna wauguzi kuna madaktari, matabibu na wataalamu wengine wa maabara na vilevile wahudumu wa afya ngazi ya jamii karibia 500 na bado tunaendelea kutoa hizo ajira kadri tunavyopata fedha"
Ambapo amesema kuwa katika kuadhimisha kumbukuzi hayati Benjamin Mkapa watafanya mijadala ya kitaalumu ambayo itajadili sera na masuala ya kitaalumu pamoja na kuwaleta pamoja baadhi ya wadau wa sekta ya afya huku msingi wa mjadala ikiwa ni rasilimali watu.
Vilevile Mkurugenzi wa Program wa BMF, Rahel Sheiza amesema kuwa kmbukizi hiyo yenye jina la Mkapa Legacy Summit inategemewa kufanyika kwa siku tatu mfululizo, Julai 29-31, 2024 ambapo kauli mbiu ni “Kuchagiza Uendelevu wa Ndani Kuelekea Upeo Mpya”.
Ameeleza kwamba kumbukizi itaanza kwa Kongamano la Rasilimali Watu wa Sekta ya afya litakaloshirikisha wadau wakiwemo wataalamu wa afya ngazi zote, na kufanyika tarehe 29-30 Julai. Ambapo ashiriki takribani 500 wanategemewa kuhudhuria huku Rais Samia akitegenewa kuwa mgeni rasmi katika kumbukuzi hiyo itakayofanyika katika ukumbi mikutano wa kimataifa Mwl. Julius Nyerere (JNICC), Dar Es Salaam.
Rahel Sheiza akifafanua kauli mbiu ya kumbukizi ya mwaka huu isemayo “Kuchagiza Uendelevu wa Ndani kuelekea kwenye Upeo Mpya” (Mkapa’s Legacy: Taking Local Sustainability to New Horizons”), amesema kuwa inaangazia maono na kazi mbalimbali za Hayati Benjamin Mkapa katika kuongeza chachu ya maendeleo ya ndani ya nchi, kwa kutumia raslimali, sera na mifumo ya ndani katika kuleta maendeleo.
Kumbukizi hiyo ya Hayati Benjamin William Mkapa itakuwa ni ya tatu kufanyika tangu kufariki kwake 23 Julai, 2020. Ambapo Kumbukizi ya kwanza ilifanyika Julai 2021 jijini Dar es Salaam, na ya pili ilifanyika Julai 2022, Zanzibar.
Itakumbukwa Taasisi ya Mkapa Foundation imekuwa ikitekeleza miradi ya afya nchini, hususani kuanzia ngazi ya Taifa hadi kwenye ngazi za chini kwenye jamii nchini kwa Tanzania Bara na Zanzibar. Ambapo mpaka sasa ina miaka 18 tokea ilipoanzishwa.