Serikali mbona mna huruma wakati biashara za utapeli zinafanyika kwenye majengo yenu hapa Kahama

Serikali mbona mna huruma wakati biashara za utapeli zinafanyika kwenye majengo yenu hapa Kahama

chizcom

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
8,680
Reaction score
18,035
Narudia tena kueleza haya yaliyopo Kahama japo nilishakuwa mwizi nikakoswa koswa ila huu wizi kama Serikali mnatoa baraka mkisubiri vilio ndio mjifanye kutoa pole.

Hapa Kahama kuna hii kampuni sijui Alliance tena imekodi jengo la NSSF na humo ndani kuna TRA na NSSF na pia ikitazamana na Halmashauri, Mkuu wa Wilaya pamoja na kila Taasisi za Serikali.

Kiukweli hii kampuni inadanganya vijana kwa kiingilio cha laki sita alafu atafute ng'ombe mwenzake ili kurudisha pesa.

Ina maana Serikali mnabariki wizi ili kesho mjifanye kutoa pole?
 
Serikali haijui iwafanyie nini vijana ambao wengi ni graduates 🎓 sasa wanapokuja majizi kama hayo yakihaidi ajiri na kwakua watu wameyaamini serikali imeamua kukumbatia huu utapeli.
 
Unatarajia serikali hapo ifanye nini wakati jiografia ya Kahama inapakana na maeneo mengi ya wilaya zenye vijana wengi waliomaliza kidato cha nne na hata hawajui wafanye nini licha ya kuwa na ardhi nzuri, mifugo mingi, misitu, na madini ya kutosha. Ikiwa hakuna mipango endelevu juu ya rasilimali watu za taifa hili tutegemee kutoona hatua zozote zikichukuliwa
 
Serikali haijui iwafanyie nini vijana ambao wengi ni graduates [emoji310] sasa wanapokuja majizi kama hayo yakihaidi ajiri na kwakua watu wameyaamini serikali imeamua kukumbatia huu utapeli.
Serikali yenyewe imejaa matapeli Sana!
 
Back
Top Bottom