Serikali: Mkopo tuliopewa na IMF tutautumia kujenga madarasa na kuimarisha Huduma za Jamii vijijini

Naomba kujua hayo masharti nafuu maana haluna aliyewahi kukopa alasema hajapewa madharti nafuu zaidi tunaona deni la taifa likipaa tu tangu kwa magufuli na sasa kwa samia.

Masharti hayo ni yapi?
Kukopa kawaida ,ukitaka masharti Kaombe mkataba
 
"mkopo wa zaidi ya dola za Marekani 500m" We msemaje wa Serikali, Hiyo uliyosema ndio kiasi gani? Kwanini hutoi takwimu iliyokamilika? Au ndio upenyo wa kupiga? Hembu uwe unautaabarisha Umma, kwa habari zilizokamilika.
 
Miundombinu ya madarasa kwanza ndio mengine yatafuata, watoto wako wako private wa kwetu wanarundikana chini kwa hiyo tulia
 
Unaweza Jenga miundombinu kwa mkopo ila ajira haitolewi kwa pesa ya mkopo,toa upumbavu wako hapa.
 
Mambo ya ajabu kabisa kuwahi kutokea! Yani pesa yote hio ndio ikajenge madarasa 1000 tu? These guys must be kidding us!

Kama tozo ya 50B inajenga madarasa 500+ hio trillion 1.2 ndio ijenge madarasa 1000 tu? Kazi ipo kwa kweli!
 
Iuzeni tu nchi na watu wake maana mnatwambia Tozo ndo itajenga madarasa,Zahanati,vituo vya afya nk,sasa hivi mmekopa tena kwa kazi hiyo hiyo shenzi nyie!
 
Mwambie huyo mkinga wa Njombe atuambie hayo madarasa yapo wilaya zipi,tarafa zipi ,mkoa upi
Unashinda dukani,hujui hata mtaani kwako kuna shule ngapi,mikutano huhudhurii unataka nani aje kwako kukuhabarisha?

Si una diwani na watendaji waulize..ila mimi kwa kuwa ni mfuatiliaji na shughuli zangu zinanipa nafasi naona kinachoendelea.
 
Kwa hiyo sio corona tena ni madarasa?

Sio kuwapa relief watu wa utalii, kuwapa subsidy na mambo kama hayo kumbe walikopa kwa mgongo sa covid halafu wanafanyia shughuli nyingine?

Sasa hela hiyo tumepewa kununua madawa, pesa ya kununulia tutatoa wapi?
 
Unajenga madarasa huku waalimu hawana nyumba za kuishi na ni wachache. Yaani Tanzania tuna kazi mbeleni. Tunaigiza kila kitu.
 
Mfadhiri gani anayekubali kutoa Mkopo kwa ajiri ya Corona, Mkopo huo huo utumike kwa shughuli nyingi ya Umeme, barabara.
hakuna Mahusiano yeyote kati ya Corona Na Umeme, barabara

Hii Serikali imeanza kusema Uongo
Uhusiano upo,tumia akili hizo ni pesa za kuchenjua uchumi anaepanga vipaombele ni aliyechukua mkopo..
 
Mambo ya ajabu kabisa kuwahi kutokea! Yani pesa yote hio ndio ikajenge madarasa 1000 tu? These guys must be kidding us!

Kama tozo ya 50B inajenga madarasa 500+ hio trillion 1.2 ndio ijenge madarasa 1000 tu? Kazi ipo kwa kweli!
Na wewe Acha kuropoka serikali imeainisha maeneo ya kupelekwa pesa hapo juu kwenye taarifa yake, kwenye madarasa wamesema watajenga 1000.. na pesa nyingine itaenda sekta tajwa hapo juu..

Acheni umaskini Til.1.2 sio pesa nyingi,miradi ya maji 4 tuu hiyo pesa inakata.
 
Sio Pesa nyingi kwa nani? We unayo hio hela?
 
Mama yenu katika ubora wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…