Kwa muda mrefu sasa katika nchi ya Tanzania kumekuwepo na wazandiki ambao wanasambaza uongo na uzushi kuwa mitihani inasahihishwa kidini. Wazandiki hawa wanazusha kuwa, watu wa dini fulani 'wanafelishwa' na watu wa dini fulani 'wanafaulishwa'. Je wazandiki hawa wanataka kumdanganya nani kuwa nchi ya Tanzania na Watanzania ni wafuasi wa dini mbili pekee?
Nauita uzandiki na uzushi kwa sababu ni uongo. Ningetarajia wafanye utafiti ili watueleze namna NACTE wanavyosahihisha mitihani na hivyo kututhibitishis madai yao. HAWAFANYI HIVYO....NA SERIKALI INAWAACHA WAUPOTOSHE UMMA. NAISIKITIKIA NCHI YANGU TANZANIA...MAMBO KAMA HAYA YA UONGO, UZUSHI, HILA NA UPUMBAVU NDIO YANAYOSABABISHA DAMU KUMWAGIKA....SERIKALI CHUKUENI HATUA.
Mimi nimefanya utafiti ili kujua mitihani inasahihishwaje hapo NECTA. Kama ninasema uongo wadau wanaohusisha na fani hii wanisahihishe. Lakini kwa jinsi mambo yanavyofanywa - hakuna hata nukta moja inayowezesha udini kujipenyeza. Ni haki tu ndiyo inatawala. Kama hujui - ni hujui; kama unajua - unajua.
i) Kwanza tukianza na watahiniwa - kila mwanafunzi hupewa namba yake ya utambulisho. Katika karatasi zake za mtihani hakuna mahali popote ambapo panaandikwa jina lake. Ni namba tu....mfano STI2013/T.210.
ii) Wasahihishaji ni walimu wanaoteuliwa kutokana na taaluma zao. Huwezi kutafuta mwalimu 'kilaza' akasahihishe mitihani. Walimu hawa wanachaguliwa huko mashuleni (nadhani wanachaguliwa na maafisa elimu?). Walimu hawa kama walivyoajiriwa bila ubaguzi wa kidini - hupata nafasi ya kwenda kusahihisha mitiha i bila kuwepo ubaguzi wa dini zao.
iii) Usahihishaji hufanywa kwa JOPO. Jopo ni idadi ya watu wapatao kumi na kuendelea au zaidi au pungufu. Walimu hawa wanakaa kuzunguka meza moja. Mezani panajazwa karatasi za mitihani. Walimu wanasahihisha mitihani ikiwa na namba za mitihani na sio majina ya wanafunzi.
iv) Wasahihishaji wanasahihisha swali moja - wakilimaliza ndio wote wanahamia kwenye swali jingine. Wanaanza na swali la kwanza....linasahihishwa likiisha wanaingia swali la pili hadi mwisho. Je hapa ni nani atamfelisha nani? kwa kumjuaje?
v) Baada ya kukamilisha usahihishaji na kuandika alama za kila swali kwenye ukurasa wa juu (wale waliopitia elimu ya msingi, sekondari, na vyuo...wanaelewa karatasi za mitihani ninazozizungumzia). Alama zinajumlishwa na kumfanya mwanafunzi mwenye namba xyz ana jumla ya alama 75%
vi) Ndipo hatua ya kuoanisha majina na namba za mitihani inafanyika. Hapa ndipo wanaingiza majina ya watahiniwa kwenye namba zao ambazo ndizo walizozitumia katika usahihishwaji. NIAMBIENI 'WAZANDIKI' HUO UDINI KATIKA USAHIHISHAJI NA UFAULUJI UNAKUJAJE?
Vii) Baada ya matokeo kutoka - kuna nafasi ya kukata rufaa kupinga matokeo. Kama kawaida jina la mtahiniwa halitumiki ila namba yake. Akishakata rufaa mtihani wake unasahihishwa na jopo maalumu la wasahihishaji ili kuona alionewa au hakuonewa. Niambieni wazandiki????
____________________________________________________________________________________________
Kwa hiyo kinachofanyika sasa kwa hawa wazandiki ni kupandikiza sumu ili jamii isiyojua ukweli huu idanganyike. Serikali timizeni wajibu wenu kukemea UPUMBAVU wa aina hii. Huu ni upumbavu kwa kuwa, ingalikuwa ni UJINGA...mtu angeuliza na kuelimishwa na hivyo angefahamu mitihani inasahihishwaje. Kuna wakati eti walitaka kwenda kung'oa katiba wa NACTE Joyce Ndalichako...huu ni wendawazimu. Joyce anaratibu shughuli za baraza na wala sio sehemu ya wasahihishaji wa mitihani. Mitihani inasahihishwa na walimu ambao ndio wanawafundisha wanafunzi masomo mbalimbali. Kama kuna dosari zozote NACTE zishughulikiwe ili kuweka mazingira ya kazi huru na ya haki.... hakuna UDINI!
Wazandiki hawa wanatumia sababu ya udini ili kudanganya wajinga...wajinga ndio waliwao! Mimi nina ndugu zangu ambao wanasoma kwenye shule fulanifulani (za kidini). Mimi nasoma serikalini. Tunapokutana kwenye group discussion hawa wenzangu hawajui mambo mengi... sielewi kwamba huko shuleni kwao wanakazaniwa elimu ya dini tu? au kama na elimu ya dunia wanapewa - je walimu wao 'wamefuzu' barabara kufundisha masomo hayo? Jamani tusidanganyane... kama huna mwalimu 'bora' usidhani utapata wanafunzi bora. Hapana! Wataishia kufeli tu.
Wito: Serikali acheni kukaa kimya. Waziri mwenye dhamana na eneo hili auelimishe umma kuhusu namna usahihishwaji unavyofanyika NACTE. Kila Mtanzania akiujua ukweli - hao 'wazandiki' watashikwa na aibu. Kila mtu ATAWAZOMEA kwa kupandikiza chuki, fitna, na uasi katika jamii. Penye ukweli uongo hujitenga. WAELIMISHENI....