Serikali msifumbie macho uzandiki huu: Upotoshwaji kuhusu nacte-baraza la mitihani

nyiondo

Senior Member
Joined
Jan 14, 2013
Posts
149
Reaction score
24
Kwa muda mrefu sasa katika nchi ya Tanzania kumekuwepo na wazandiki ambao wanasambaza uongo na uzushi kuwa mitihani inasahihishwa kidini. Wazandiki hawa wanazusha kuwa, watu wa dini fulani 'wanafelishwa' na watu wa dini fulani 'wanafaulishwa'. Je wazandiki hawa wanataka kumdanganya nani kuwa nchi ya Tanzania na Watanzania ni wafuasi wa dini mbili pekee?

Nauita uzandiki na uzushi kwa sababu ni uongo. Ningetarajia wafanye utafiti ili watueleze namna NACTE wanavyosahihisha mitihani na hivyo kututhibitishis madai yao. HAWAFANYI HIVYO....NA SERIKALI INAWAACHA WAUPOTOSHE UMMA. NAISIKITIKIA NCHI YANGU TANZANIA...MAMBO KAMA HAYA YA UONGO, UZUSHI, HILA NA UPUMBAVU NDIO YANAYOSABABISHA DAMU KUMWAGIKA....SERIKALI CHUKUENI HATUA.

Mimi nimefanya utafiti ili kujua mitihani inasahihishwaje hapo NECTA. Kama ninasema uongo wadau wanaohusisha na fani hii wanisahihishe. Lakini kwa jinsi mambo yanavyofanywa - hakuna hata nukta moja inayowezesha udini kujipenyeza. Ni haki tu ndiyo inatawala. Kama hujui - ni hujui; kama unajua - unajua.
i) Kwanza tukianza na watahiniwa - kila mwanafunzi hupewa namba yake ya utambulisho. Katika karatasi zake za mtihani hakuna mahali popote ambapo panaandikwa jina lake. Ni namba tu....mfano STI2013/T.210.
ii) Wasahihishaji ni walimu wanaoteuliwa kutokana na taaluma zao. Huwezi kutafuta mwalimu 'kilaza' akasahihishe mitihani. Walimu hawa wanachaguliwa huko mashuleni (nadhani wanachaguliwa na maafisa elimu?). Walimu hawa kama walivyoajiriwa bila ubaguzi wa kidini - hupata nafasi ya kwenda kusahihisha mitiha i bila kuwepo ubaguzi wa dini zao.
iii) Usahihishaji hufanywa kwa JOPO. Jopo ni idadi ya watu wapatao kumi na kuendelea au zaidi au pungufu. Walimu hawa wanakaa kuzunguka meza moja. Mezani panajazwa karatasi za mitihani. Walimu wanasahihisha mitihani ikiwa na namba za mitihani na sio majina ya wanafunzi.
iv) Wasahihishaji wanasahihisha swali moja - wakilimaliza ndio wote wanahamia kwenye swali jingine. Wanaanza na swali la kwanza....linasahihishwa likiisha wanaingia swali la pili hadi mwisho. Je hapa ni nani atamfelisha nani? kwa kumjuaje?
v) Baada ya kukamilisha usahihishaji na kuandika alama za kila swali kwenye ukurasa wa juu (wale waliopitia elimu ya msingi, sekondari, na vyuo...wanaelewa karatasi za mitihani ninazozizungumzia). Alama zinajumlishwa na kumfanya mwanafunzi mwenye namba xyz ana jumla ya alama 75%
vi) Ndipo hatua ya kuoanisha majina na namba za mitihani inafanyika. Hapa ndipo wanaingiza majina ya watahiniwa kwenye namba zao ambazo ndizo walizozitumia katika usahihishwaji. NIAMBIENI 'WAZANDIKI' HUO UDINI KATIKA USAHIHISHAJI NA UFAULUJI UNAKUJAJE?
Vii) Baada ya matokeo kutoka - kuna nafasi ya kukata rufaa kupinga matokeo. Kama kawaida jina la mtahiniwa halitumiki ila namba yake. Akishakata rufaa mtihani wake unasahihishwa na jopo maalumu la wasahihishaji ili kuona alionewa au hakuonewa. Niambieni wazandiki????
____________________________________________________________________________________________
Kwa hiyo kinachofanyika sasa kwa hawa wazandiki ni kupandikiza sumu ili jamii isiyojua ukweli huu idanganyike. Serikali timizeni wajibu wenu kukemea UPUMBAVU wa aina hii. Huu ni upumbavu kwa kuwa, ingalikuwa ni UJINGA...mtu angeuliza na kuelimishwa na hivyo angefahamu mitihani inasahihishwaje. Kuna wakati eti walitaka kwenda kung'oa katiba wa NACTE Joyce Ndalichako...huu ni wendawazimu. Joyce anaratibu shughuli za baraza na wala sio sehemu ya wasahihishaji wa mitihani. Mitihani inasahihishwa na walimu ambao ndio wanawafundisha wanafunzi masomo mbalimbali. Kama kuna dosari zozote NACTE zishughulikiwe ili kuweka mazingira ya kazi huru na ya haki.... hakuna UDINI!

Wazandiki hawa wanatumia sababu ya udini ili kudanganya wajinga...wajinga ndio waliwao! Mimi nina ndugu zangu ambao wanasoma kwenye shule fulanifulani (za kidini). Mimi nasoma serikalini. Tunapokutana kwenye group discussion hawa wenzangu hawajui mambo mengi... sielewi kwamba huko shuleni kwao wanakazaniwa elimu ya dini tu? au kama na elimu ya dunia wanapewa - je walimu wao 'wamefuzu' barabara kufundisha masomo hayo? Jamani tusidanganyane... kama huna mwalimu 'bora' usidhani utapata wanafunzi bora. Hapana! Wataishia kufeli tu.

Wito: Serikali acheni kukaa kimya. Waziri mwenye dhamana na eneo hili auelimishe umma kuhusu namna usahihishwaji unavyofanyika NACTE. Kila Mtanzania akiujua ukweli - hao 'wazandiki' watashikwa na aibu. Kila mtu ATAWAZOMEA kwa kupandikiza chuki, fitna, na uasi katika jamii. Penye ukweli uongo hujitenga. WAELIMISHENI....
 
Serikali inayoongozwa na mwislamu mwenye lengo la eti kuwainua waislamu kutoka kwenye hali ya kufikirika itawezaje kufanya utafiti wa kupata ukweli wa jambo!!!! Kwa taarifa yako mambo yote hayo yana baraka za kiongozi mkuu pale magogoni.
 
Waongeze bidii na umakini katika masomo ili kupata matokeo mazuri na kufaulu.
 
nyiondo,

..hata mimi nimeyasoma malalamiko ya Waislamu kuhusu necta ktk gazeti la an-nuur.

..nadhani wanacholalamika ni jinsi madaraja/alama zinavyopangwa. kwamba mwaka mmoja C inaweza kuwa anaanzia 61, halafu mwaka mwingine ikawa inaanzia 71. sina uhakika lakini nadhani hicho ndicho wanachokilalamikia.

..sasa wanadai kuna kamati ambayo inahusika na kupanga madaraja/alama mwaka hadi mwaka. wanadai eti kamati hiyo imejaa Wakristo na hivyo wanahisi kwamba Wakristo hao huwafanyia hujuma watahiniwa Wakiislamu.

..naweza kuwa nimekosea, lakini nimejitahidi kueleza kadiri nilivyoelewa kile kilichoandikwa ktk gazeti la an-nuur.

cc: Kichuguu, Zakumi, Mohamed Said, Mzee Mwanakijiji , zomba, Ritz
 
Last edited by a moderator:
Wanaposahisha hawatambui jina la mtu kwani kinachoandkwa ni namba ya mtihani ya mtahiniwa.
.Je? Namba za watahiniwa zinatolewa kulingana na dini ya mtu kiasi kwamba msahishaji ajue dini ya mtu?

.Je wanao husika kusahisha ni watu wa dini moja pekee na je wanakuwa pekee yao?

.kama ipo ipo tu! Na kama m2 hawezi ni hawez tu!

.kudhiirisha ukilaza wa watu fulan we anza kuangalia wanasayansi wa dunia hii ni wa2 wa dn gan.
.Je? Nao walifanya uonevu kama huu unao daiwa na vilaza hawa?
.Ebu angalia vitabu vingi kuanzia madiscover hadi mapablisher kama utawakuta vilaza hawa hata kidogo.
. MI NAWASHAURI WAACHE KUPAPALIKA KWANI ILISHAKUJULIKANA UWEZO WAO TANGU KUUMBWA KWA DUNIA.
 
NECTA na NACTE ni bodies mbili za elimu tofauti kabisa
 
waislam muda mrefu wamekuwa wakilalamika kuhusu necta na kuonesha waziwazi kutokuwa imani na baraza hili lakini kabla hatujawaita wadini na wanakazania sana elimu ya dini hebu kwanza tuangalie udhaifu wa hii necta uliojitokeza ktk kupanga matokeo hasa ya somo la islamic uliotokea mwaka jana.Maswali mengi unaweza ukajiuliza kuwa ni kweli kwamba necta walikuwa hawana taarifa juu ya mabadiliko yaliyotokea ktk mfumo wa utungaji wa somo hili? Na kama ilikuwa na taarifa inaoneka ni jinsi gani mambo ya muhimu hasa ya waislam kutopewa kipaombele mpaka kufikia necta kukiri na kuona kuna makosa yaliyotoke ktk kupanga madaraja.
Mambo kama haya yanawafanya waislam kuwa na mashaka na hili baraza.
 
nyiondo, ulifanya utafiti NECTA au NACTE? Utafiti makini unaondoa dhana kama hii:
(nadhani wanachaguliwa na maafisa elimu?)

vi) Ndipo hatua ya kuoanisha majina
na namba za mitihani inafanyika.
Hapa ndipo wanaingiza majina ya
watahiniwa kwenye namba zao
ambazo ndizo walizozitumia katika
usahihishwaji.

Uchakachuaji unaweza kuaminika kutokuwepo kama namba zitatumika mwanzo mpaka mwisho wa huo mchakato.
...kuna nafasi ya kukata rufaa...
Si kila mtahiniwa atauweza mchakato wake.!
 
Last edited by a moderator:

hii umeandika mwenyewe au umeandikiwa?
Dogo kama hujui yanayoendelea NECTA ni bora ujikalie kimya. kuna ujinga mkubwa sana unaenlea pale na ndio maana Mh Nasari alikuwa anapeleka hoja binafsi kuhusu NETA. Wala usikae ukafiiri watu husema bila kuwa na vividy evidence. Nakushauri ufanye utafiti wa kinachosemwa kabla ya kuurupuka kuandika.
 
Hujielewe mara NECTA mara NACTE, hebu kaa chini ujue unazungumzia nini ili nije kuchangia
 
Pamoja na kasoro zilizopo NECTA,hakuna suala la udini.Hoja za waislam ni za kitoto na ni kwa sababu ya kukosa elimu.Hawa jamaa wanapoteza muda kwenye madrasa halafu wakifeli wana kuja na hoja km hizo.Mtoa mada sahihisha sio NACTE ni NECTA.
 
Hoja za kina Ponda na mohamed said ni MFU
cc zomba n co.
 
Last edited by a moderator:
kwa kweli ndugu zangu waislamu kazeni buti, hakuna kipanga anayeweza kufanywa kilaza, kipanga ni kipanga na kilaza ni kilaza tu, hakuna udini wala ndumba.
 
kwahyo hawa wa2 uliowatag ndo walalamikaji na watetezi au wanaumuhimu gani ktk uzi huu?
 
kaka unaelewa maana ya standardization?B kikawaida inaanzia 61 bt inabadlka kulingana na ufaulu wa wanafunzi...wakifaulu wengi inapandishwa na wakifeli wengi inashushwa na hyo ni ki2 ya kawaida sana...
 
naamini islamic knowledge inasahishwa na waislam japo sina uhakika alafu ni upumbavu kukomalia somo ambalo ata vyuo vikuu hawalihesabu ktk kudahili wanafunzi...mbona hamlalamiki mmeonewa kwenye physics,maths au geog?nyie mmekomalia elimu akhera pekee...badilikeni.
 
naamini kipanga haitaji bible/islam knowledge ili afaulu....yale masomo yake 7 ya msingi plus ya combination yanatosha sana...
 
Samahani wajumbe,
namaanisha necta...... Mitihani ya kidato cha nne/sita
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…