Serikali msizime mitambo ya kuzalisha umeme

Basi uzieni majirani, ila muwe macho mkileta mchezo wa umeme kukatika bila sababu yenye vigezo mtashtakiwa kimataifa.
 
Nimemsikia Waziri wa Nishati Bw. Biteko akisema Serikali imelazimika kuzima mitambo ya kuzalisha umeme kwenye bwawa la Mwl Nyerere kwa kuwa matumizi ya umeme nchini ni madogo kuliko uzalishaji.
Ingekua January kasema haya kama naona ambavyo angeitwa mhujumu uchumi na mpiga dili!! Ila kwa Biteko watu kimyaaaaa.
 
Sidhani km uwingi wa umeme ni sababu ya kuzimwa. Nilivyosikia ni kuwa mitambo yote 8 ya uzalishaji hayajakamilika. Umeme ni bidhaa ungeweza kuuzwa nje ya nchi
Kasikilize tena taarifa ya waziri wa Nishati Bw. Biteko
 
washushe bei ya unit tufunge AC mpaka chooni wataona matumizi ya umeme yatakavyopanda.
mpaka chipsi zege zitapikwa kwa majiko ya umeme.
 
Nilishangaa sana kusikia waziri anasema umeme unazalishwa ni mwingi kuliko matumizi.Nikamkumbuka trump aliposema Africa ni shithole country
 

Bei ipo juu kwa sababu ya umeme wa gesi asilia iko juu. Hao wawauzie south africa huo. Sisi tubaki na huu wa mabwawa ambao ni zaidi pia ya mahitaji kwa sasa. Tutumie ya bwawa la Rufiji tupumzishe vile vinu vingine ili kuvifanyia ukarabati pia kupunguza tope ktk mabwawa ya zamani. Bei itashuka. Vinginevyo wapandishe kima cha tarrif 4 kutoka 75 units mpaka 250 tuweze kutumia umeme kupikia.
 
Turudishe mpango wa kuunganisha umeme kwa elfu 27, tuongeze bei ya umeme kwa unit moja kwa shs 20, mapato ya tanesco yataongezeka kwa 20%. Hii itaongeza uwezo wa shirika kuwahudumia wananchi
 
Serikali ingeshusha bei ya umeme mapato yake yangekuwa sana sababu ya kuchochewa kwa shuguli za kiuchumi. Badala ya kuuza Unit moja 360 wauze 150-200.
 
Siasa za umeme hazitakaa ziishe nchi hii.
 
Hii nchi jamani..!
 
Mtauzaje wakati bado hamna umeme wa kuwatosheleza MAHITAJI mkuu?
Mamlaka zinasema tunazalisha mwingi kuliko mahitaji, kama ni kweli.... badala ya kuuza nje mbona tunazima mitambo?
 
Mamlaka zinasema tunazalisha mwingi kuliko mahitaji, kama ni kweli.... badala ya kuuza nje mbona tunazima mitambo?
Hii nchi ina vituko Sana, na kwanini bei ya unit moja ya umeme ibakie ileile ya kipindi cha ukame na wakati sasa hivi wanasema Wana umeme ambao hawajui pa kupeleka? Tusidanganyane bado umeme ni tatizo nchini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…