Serikali mtambue kuwa warabu sio wahisani wazuri

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
16,871
Reaction score
39,881
Naona baada ya kukataliwa kupewa mikopo na misaada,. Sasa mnakimbilia kujipeleka Kwa warabu

Nawakumbusha warubu sio wahisani wazuri kama wazungu

Mzungu anatoa misaada mingi na masharti machache kama democrasia, haki za binadamu, kutunza mazingira n. K

Sasa huko Kwa mwarabu mtaishia kupewa tende, alkasusi, na vikoi
 
Simba akikosa Simba hakikosa nyama ula majani.
 
tushapokea gari zetu mbili alf wao wanachukua Dar nzima na watu wake🤣🤣🤣
 
Waarabu ndio waliouziwa bandari kwa hiyo nilitegemea kuwaona kipindi hiki kutumika sana kwenye maswala ya diplomasia.

Lakini tukiangalia kuhusu misaada basi Waarabu hawajawahi kutupa msaada wowote wa maana na wabinafsi sana.

Hata ukiangalia kwenye mataifa ya waarabu wenzao ambao walikutwa na majanga yaliyohitaji kutolewa msaada tuliona waarabu wakiwa nyuma na mataifa ya Ulaya ndio yaliyokuwa kinara kutoa misaada.

Sasa kama tu waarabu wenzao waifanyiwa undava, sisi ni nani tujione special mbele ya muarabu?

Mwaka jana gazeti la Citizen liliandika habari iliyosema Tanzania na Kenya ni miongoni mwa nchi kumi zinazopokea nusu ya misaada inayotolewa na nchi za Ulaya kuja Afrika.

Wafadhili wakuu ni World Bank na nchi wanachama wake hao ndio tunaowategemea miaka yote kwenye misaada na mikopo.
 
Kizimkazi katuponza kwakweli
 
Kule kwa Traore wamegonga mwamba.
 
Pale mwenye njaa akijitapa kumshibisha mwenye njaa mwenzake
 
Sikio la kufa halisikii dawa....
 
Kwani, kuna wahisani wazuri? Dawa siyo ubaya au uzuri wa wahisani bali kuacha kutegemea hisani wakati tunazo raslimali nyingi tena za thamani.
 
Kwani, kuna wahisani wazuri? Dawa siyo ubaya au uzuri wa wahisani bali kuacha kutegemea hisani wakati tunazo raslimali nyingi tena za thamani.
Acha maneno ya siasa hakuna mwenye akili za utilize hizo Rasimali.
Madini wanachimba wazungu
Bandari mmeuzia waarabu
Utalii mmewapa UAE

Hapa serikali inategemea Kodi za mama ntilie kuendesha nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…