Serikali na CCM, Wameamua kuwahudumia Watanzania na sio kupambana na Wanaharakati wa matusi au wale we ngine wakutukana

Serikali na CCM, Wameamua kuwahudumia Watanzania na sio kupambana na Wanaharakati wa matusi au wale we ngine wakutukana

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2013
Posts
2,255
Reaction score
1,565
Serikali ya awamu ya Sita ina jukumu la kubwa la kuwaletea Watanzania Maendeleo, ustawi bora wa Maisha, huduma za Kijamii bora na usawa kwa kila Mtanzania.

Kuna kelele nyingi na matusi toka kwa Wanaharakati ambao lengo lao kila mmoja anajua kuwa si jema, si kwamba Serikali ya awamu ya sita, si kwamba Wakurugenzi zaidi ya 180 au Wakuu wa Wilaya wanashindwa kujibu, Serikali na Watumishi wake wamechagua kuwatumikia Watanzania ili kutimiza Ilani ya Chama waliyoinadi 2020.

CCM ina Vijana, akina Mama na Wazee wenye weredi, busara na Wasomi ambao katika nyakati ambapo vyama vingine vimechagua kueneza uongo, ubaguzi na matusi, CCM wamechagua kuisimamia Serikali kuhakikisha inawatumikia Watanzania.

Katika yote, Watanzania wanaoishi Mjini na Vijijini wanaona mambo makubwa yanaendelea

1.Barabara zinavyojengwa huko Kigoma, Katavi, Rukwa, Rombo, etc - leo hakuna mkoa ambao haujaungwa na mtandao wa lami

2.Shule mpya za kisasa za Secondary kwa Wasichana kila mkoa zinavyojengwa.

3. Ujenzi wa Madarasa, Matundu ya vyoo kwa kila shule ya Secondary na Msingi.

4.Ujenzi mpya wa na ukarabati wa nyumba za Walimu

5.Ujenzi wa mabweni kwa Shule za Secondary.

6. Ujenzi na ukarabati wa Hospital za Kanda , Wilaya, Vituo vya Afya Zahanati etc

7..SGR, kupandisha madaraja kwa Watumish etc etc

Anyway.. kura hazipigwi X,

Mwenyezi Mungu ibariki Tanzania

Mwenyezi Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMh. Samia Suluhu Hassan
 
Back
Top Bottom