Serikali na Dhana Potofu kwamba Wawekezaji lazima Watoke Nje Tu!

Serikali na Dhana Potofu kwamba Wawekezaji lazima Watoke Nje Tu!

MwanaHaki

R I P
Joined
Oct 17, 2006
Posts
2,401
Reaction score
707
KWA TAKRIBAN miongo miwili sasa, serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia kitengo cha Tanzania Investment Centre (TIC) pamoja na asasi nyingine, imekuwa ikiweka mkazo na jitihada kubwa za kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji, wawekezaji ambao ni raia wa nje, hususan watu weupe - wazungu!

TIC ilipoanzishwa ilijikosha kwa kusema kwamba inamkaribisha mwekezaji yeyote, awe wa ndani au nje. Lakini kadri siku zilivyosonga mbele dhamira yake halisi ilizidi kujitokeza; Wazungu tu!

Hivyo basi, kutokana na sera hii, Rais amekuwa akisafiri mara kwa mara nje ya nchi kwenye nchi mbalimbali zilizoendelea barani Ulaya na Marekani akifanya kazi ya Ubalozi wa Kiuchumi, kazi ambayo aliibuni akiwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kiasi cha kuwashangaza wadau wa uchumi na diplomasia hapa nchini na kuhoji: Rais amesahau kwamba yeye ni Kiongozi wa Nchi?

Wadau wengine wamekwenda mbele zaidi na kusema kwamba Rais ameidhalilisha Taasisi ya Urais, kwani Rais ni Taasisi, si mtu binafsi.

"Rais anapashwa kukumbushwa kwamba alipaswa kuikabidhi sera ya Economic Diplomacy au kuunda taasisi ambayo ingefanya kazi hiyo chini ya ofisi yake, jambo ambalo lingemwezesha kujiepusha na tuhuma nzito wa matumizi mabaya ya ofisi yake, ikiwa ni pamoja na matumizi yasiyo ya msingi ya fedha nyingi ambazo mara nyingi huwa hazina maelezo na wala matumizi yake hayakaguliwi.

"Yote hayo ni tisa. Kumi ni pale rais anapoandamana na maswahiba wenzake akitumia chombo cha serikali, Ndege ya Rais, watu ambao hawajahakikiwa, hawajachunguzwa wala kuidhinishwa na Idara ya Usalama wa Taifa, Kitengo cha Usalama wa Rais.

"Unajua, ndege hii ilinunuliwa kwa mabilioni ya fedha na kilichomo ndani yake ni siri ya taifa. Sasa iwapo mmoja wa watu hao angekuwa gaidi au jasusi, angeweza kuuza siri za ndege hiyo, jambo ambalo lingeweza kuhatarisha usalama wa ndege hiyo na hata Rais mwenyewe. Sisi tunajiuliza anawaamini kiasi gani watu hao kiasi cha kuwapa nafasi kubwa namna hiyo?

"Kama mjuavyo, ndege hiyo ni ndogo, kwa hiyo unakuta watu wachache, 5 hadi 7 wanapanda ndege hiyo, waliobaki, 70 na ushee wanapanda ndege za mashirika ya nje, Business au First Class!

"Sisi hatuna chuki na Rais wetu. Tunampenda. Lakini tunajiuliza iwapo kasi hii ya kutafuta wawekezaji hawa wa nje imezaa au itazaa matunda," kilisema chanzo chetu.

----------------

Hii ni sehemu ya kwanza ya makala haya. Usikose kusoma sehemu ya pili na ya mwisho ya sehemu hii muda si mrefu ujao.
 
Moderator

Nadhani bora niufute huu uzi kwani, licha ya kupitiwa na zaidi ya watu 450, hakuna hata mmoja aliyetoa hoja, kuunga mkono, kuupinga au kutoa ushauri.

Ushauri wako?
 
Last edited by a moderator:
Moderator

Nadhani bora niufute huu uzi kwani, licha ya kupitiwa na zaidi ya watu 450, hakuna hata mmoja aliyetoa hoja, kuunga mkono, kuupinga au kutoa ushauri.

Ushauri wako?

naona mkuu umeamua kumuongelea rais na kuacha dhumuni la huu uzi. ungeongelea nini kifanyike ili na sisi watz tuwekeze kwenye nchi yetu kuliko kuongelea mambo ya rais ambayo ila mtu anayajua na kuyakemea pia.. nadhani ndio maana hukupata wachangiaji mkuu..
 
mimi nadhani ameongelea zaidi udhaifu wa taasisi ya urais, ''tumefika hapa tulipo kwa sababu ya UDHAIFU wa JK, na upuuzi wa CCM'' JJ Mnyika akiwa bungeni.
 
MwanaHaki mkuu, umenifurahisha saana! Lol

Hizo likes si ni dalili kuwa imeungwa mkono tayari?! Wengine huwa ni wasomaji tu wala hawachangii. Na jukwaa hili I think linaongoza kwa kusomwa na guests kuliko hata members or members ambao husoma kama guests or whatever (kama sikosei).

Kwamba unataka ifutwe? Iachwe bana! Hata hivyo wacha tusubiri pengine Moderator atakua na ushauri kama ulivyo omba.
 
Moderator
Nadhani bora niufute huu uzi kwani, licha ya kupitiwa na zaidi ya watu 450, hakuna hata mmoja aliyetoa hoja, kuunga mkono, kuupinga au kutoa ushauri.
Ushauri wako?
MwanaHaki fuata maoni na ushauri wa Dada AshaDii. JF-Members wako addicted na appetite ya mambo mengine kabisa tofauti na uchumi, biashara na uwekezaji. Ushahidi uko mwingi. Anza kwa kurejea ule uzi wetu wa kutoweka kwa huduma za umma, gonga kaangalie kama hata hao walionakiliwa kwenye mada, ambao ni mabingwa wa kusema Bungeni na majukwaani kama wamejishughulisha kwa kuchangia chochote! Mengine tunaweka JF kwa ajiri ya wepesi wa rejea, free archive na kumbukumbu.
 
AshaDii

Kwa kuwa mumeamua kuchangia, Moderator hataufuta uzi huu. Sasa kazi imeanza rasmi. Ngoja nivute pumzi. 🙂
 
Last edited by a moderator:
naona mkuu umeamua kumuongelea rais na kuacha dhumuni la huu uzi. ungeongelea nini kifanyike ili na sisi watz tuwekeze kwenye nchi yetu kuliko kuongelea mambo ya rais ambayo ila mtu anayajua na kuyakemea pia.. nadhani ndio maana hukupata wachangiaji mkuu..

ndeticia

Rais ndiye kiongozi wa "Serikali", kwa hiyo serikali inapokuwa na dhana potofu ambayo "wawekezaji" lazima watoke nje ya nchi tu, hapo ndipo utata unapoanzia.

Kwa kukujibu, hebu jiulize: Ni changamoto zipi zinazotufanya sisi Watanzania tushindwe kufikiria kwamba sisi ndio wenye mamlaka na nafasi kubwa zaidi ya kuwa wawekezaji kuliko kuwasubiri hao wageni? Kwa nini tushindwe kulima shamba letu wenyewe na badala yake tusubiri wageni waje kutulimia, wavune kisha waondoke zao na kutuachia mabua tu?

Orodhesha hapa hizo changamoto, tuzijadili moja baada ya nyingine.

Asante.
 
MwanaHaki fuata maoni na ushauri wa Dada AshaDii. JF-Members wako addicted na appetite ya mambo mengine kabisa tofauti na uchumi, biashara na uwekezaji. Ushahidi uko mwingi. Anza kwa kurejea ule uzi wetu wa kutoweka kwa huduma za umma, gonga kaangalie kama hata hao walionakiliwa kwenye mada, ambao ni mabingwa wa kusema Bungeni na majukwaani kama wamejishughulisha kwa kuchangia chochote! Mengine tunaweka JF kwa ajiri ya wepesi wa rejea, free archive na kumbukumbu.
Ericus Kimasha

Usemayo ni kweli. Huu utegemezi wa "nje" unatugharimu. Hebu ona, vitu kama vitanda vya hospitali tunasubiri tuletewe - vya mitumba - kutoka nje (Marekani na Ulaya), wakati vimetengenezwa kwa mabomba yaliyokunjwa tu! Kama ni magurudumu mbona yapo hapa kibao?

Ati tunataka uwekezaji na misaada kwenye huduma za afya; nani atujengee hospitali wakati udongo tunao na tunaweza kuchoma matofali ya udongo? Kwani madirisha lazima yawe ya aluminium? Mbona mbao zipo kibao? Au ni zile zinazouzwa nje ya nchi kila uchao?
 
Last edited by a moderator:
Wakuu naunga mkono hoja, Msisahau hata hao makuwadi wa wawekezaji wa nje husema siku zote kuwa "wawekezaji siyo lazima watoke nje, hata wa ndani ruksa". Tena watetea hoja yao kwa kusema ili kuwavutia wawekezaji wa ndani wamemshushia hata ile threshold ya kupata incentives- sijui kama hii inatosha na sijui kama kweli mazingira ya wawekezaji wandani ni rafiki kwa kiasi kinachoongelewa - wenye taarifa na hayo watatuambia.Mimi nina moja tu ambalo mpaka kesho sijalielewa. Kwa wale wafuatiliaji wa mambo haya watakumbuka miaka ya 90 tulipoanzisha Investment Promotion Centre - [IPC], pamoja na mambo mengine tulitenga kwa uwazi maeneo ambayo ni mtanzania tu anaweza kuwekeza -[sijui kama tunakumbuka?] kama siajakosea eneo moja wapo lilikuwa ni mighahawa(restaurants). kwa maana kuwa hatuhitaji mwezaji kutoka ughaibuni aje kuanzisha mghahawa kariakoo - hilo tunaeza sisi tena vizuri na hatutaki uje umbane yule mswahili anayetutengenezea ile pilau tuanyoipendandaga, kisa una pesa ma mtaji unaokublika na viwango vya uwekezaji. Mantiki hii ni wazi nampaka leo sijaelewa nani alitudanganya tukafuta hiki kipengele. Matokeo yake ni wazi mchina anauza vijiko na sahani kariakoo naye mwekezaji.
Wakuu nawasilisha hoja
 
Moderator

Nadhani bora niufute huu uzi kwani, licha ya kupitiwa na zaidi ya watu 450, hakuna hata mmoja aliyetoa hoja, kuunga mkono, kuupinga au kutoa ushauri.

Ushauri wako?

Mkuu nina muda sijapita mitaa hii, mimi pia kuna kipindi-siyo mara moja nilijiuliza kama hapa ni kwa great thinkers. kwa muda mrefu unaona mada ambayo ungefikiri inafikirisha na hivyo hapa kuwa jukwaa sahihi lakini watu wanafungua wanafunga. Niseme nimerudi na kukuta mada nyingi moto- usifute mkuu tupo kuchangia
 
Poverty is an attitude. It is expensive to be poor. Tusipobadili attitude zetu tutaendelea kuwa under developed maana hatutakaa tuwe na confidence kufanya chochote kila siku tutakuja na majina mazuri ya kujustify utegemezi kama investors etc huku tukidhani kuwa investor quality au attribute ya kwanza ni uwe mweupe, umetoka ulaya, Asia au America kama sivyo basi hata wakenya na wanyarwanda tusingewaita wahamuaji haramu tungewaita investors tu! Kwani wana tofauti gani na hawa wengine weupe? Lakini kwakuhusudu tuko tayari tuambiwe vyakufanya na weupe tukiwaingiza mpaka vyumbani lakini ole wetu awe ngozi nyeusi weeee; huyo ni ama tapeli, mhamiaji, jambazi etc!
 
Back
Top Bottom