kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Mpira ni pesa, kutunza uwanja wa mpira na miundombinu yake ni ghali sana, lakini hata gharama za kuendesha timu na kuandaa mechi ni kubwa sana. Mpira wetu umekuwa sana, unakusanya wachezaji wakubwa wa nchi mbalimbali. Kutokana na ukweli huu hata Watanzania wanaotaka kwenda kuangalia mpira wameongezeka sana.
kautafiti kangu nilikokafanya kutokana na kuingia viwanjani kila wakati kwa muda mrefu kanaonyesha kuwa, watu waonaojisaidia haja kubwa sehemu za haja ndogo na kuharibu miundombinu ya uwanjani wengi wao wanatoka miongoni mwa watazamaji wa viingilio vya chini sana vya 2000 na 3000 au walioingia bure kabisa.
Hawa ni watazamaji ambao ama wanajutia hela yao waliyotoa, hawana nauli ya kurudia, au hawana hela ya kula baada ya mechi kwisha. Hawa ni wale ambao ni rahisi kung'oa koki au Bomba au sinki au balbu au chochote wakauze huko mtaani.
Kiingilio cha sh. 3000 hii ni sawa na 1 US Dollar, duniani hakuna mpira huo. Kiingilio kidogo kinavuta watu wengi wenye uwezo wa kuharibu miundombinu ya uwanjani na kuongeza gharama za uendeshaji kwa bei ya hasara kwa serikali, TFF, timu husika na wadau wengine.
Kiingilio kisiwe chini ya 3-5 US dollar, yaani kati ya Sh. 10,000 na 15,000. Viingilio hivi vitaendana na mabadiliko ya mpira kwenye nchi yetu.