Serikali ni ya nini basi?


Mzee MKJJ unatafuta article ya kuandika jumatano ijayo nini 🙂?
 
Mzee MKJJ unatafuta article ya kuandika jumatano ijayo nini 🙂?

Hapana (ingawa sifuti kabisa uwezekano wa kufanya hivyo baadaye). Hata hivyo kwangu niko interested zaidi na falsafa nzima na nadharia ya seriikali:

a. Serikali ni nini?
b. Serikali ina umuhimu gani katika maendeleo ya mtu mmoja mmoja na jamii nzima?
c. Serikali bora inatambulikanaje?
d. Je ni lazima kuwa na serikali ya kidemokrasia ili tuwe na maendeleo?
e. Je vyama vya siasa ni muhimu katika ufanisi wa utendaji kazi wa serikali?
f. Je serikali inaweza kuondolewa kwa nguvu na ni sababu gani zinaweza kuruhusu hiilo kutokea?
g. Je serikali ili kuhakikisha inaendellea kuwepo inayo haki ya kutumia nguvu kuzima jaribio lolote la kuiondoa?
h. Je mfumo wa kutumia kura ndio mfumo mzuri zaidi wa kubadilisha serikali?
i. Je Chama cha kisiasa chaweza kuanzisha ambacho hakina lengo la kushika serikali? yaani kiwe na lengo la kuwa mpinzani tu?

KIMSINGI, serikali ni yanini basi?

et cetera....
 
Que.Kati ya mtu masikini na mtu tajiri ni nani anaihitaji serikali zaidi?

Ans.Government is of the people, by the people, and for the people (rich or poor)

Que.Nani anafaidika zaidi na uwepo wa serikali, maskini au tajiri?

Ans.wote...wanafaidika sawa......

Mhh! Sikujua kama na humu JF namo-mna 'Friendly Firing',nilithani ni kule Afghanistan,basra tu.....
 
 
 
Ukiona au kusikia yanayoendelea Somalia, Iraq, Afghanistan, China, USA, Libya, Tanzania, Zimbabwe, DRC,....utapata tafsiri na maana nyingi za SERIKALI. Utaona pia nani wanafaidika na uwepo/kutokuwepo kwa serikali.
 
Wildcard, hebu fafanua kwa kutumia mifano ya hizo nchi ulizozitaja; una maana gani?
 


ni maswali ambayo hakuna mtu mwenye kuweza kuchambua moja baada ya jingine...?
 
Wildcard, hebu fafanua kwa kutumia mifano ya hizo nchi ulizozitaja; una maana gani?

Mzee,
Nimekuonyesha tu neno Serikali lilivyo pana na gumu kulieleza. Cha msingi ni kwamba zote hizo nilizokutajia ni serikali ingawa zinatofautiana sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…