Georgewashington
New Member
- Feb 23, 2013
- 4
- 0
SERIKALI NUNUA KIWANJA KIDOGO CHENYE RUTUBA KULIKO KIKUBWA KISICHO NA RUTUBA KWANI GHARAMA HUTOIWEZA.
Wajomba nami leo wacha nimwage cheche zangu kwa hili serikali imekosea ila siilaumu ijipange upya tuu ndo kuangalia nini chanzo.
Ninasikitika sana lakini kwa sababu haina jinsi inabidi nikubali tuu na kisha nicheke japo kidogo. Kwa nini hawa wahusika hawawajibishwi, hadi inafikia tunafika kiwango hiki. Takwimu hadi leo sijaziamini ila inabidi nikubali tuu kuwa katika kila wanafunzi 100 basi sitini ni maziro. Ikimaanisha katika kila wanafunzi mia waliofanya mtiani wa kidato cha nne, sitini kati yao hawakuwa na uwezo wa kufanya mtihani huo. Tulikuwa tukisikia kuwa shule za kusini zinafeli au shule za serikali zinafeli haya yote yamekuwa ni tabia sasa na hakuna ufuatiliaji wowote ule. Sasa ugonjwa ushaambukiza na kwingine hivyo dawa sijui itakuwaje maana chanjo hamukutoa kwa waathirika wa miaka iliyopita.
Serikali inapanga 20% ya bajeti au mijihela kwa ajili ya masuala ya kielimu ila wanafunzi wanapata mabuyu au wanataga. Inasikitisha ila inafurahisha kwa upande mwingine kwamba serikali badala ya kuangalia Quality yenyewe inaangalia Quantity nikimaanisha badala ya kuangalia viwango au elimu bora wao wanaangalia idadi. Hii ni sawa na kununua eneo kubwa unaloambiwa halifai kwa kilimo na kuliacha eneo dogo lenye kina aina ya mahitaji kwa ajili ya matokeo mazuri au kilimo bora.
Ifikie wakati sasa walimu wanapotoa hoja zao wasikilizwe. Haiwezekani kuwa mwalimu analalamika na maisha pia yanamkandamiza, mwenye nyumba anataka kodi, watoto walipiwe ada, bado hajaumwa nk. Kisha anapoteza muda wake ili aweze kuongea na wewe kisha unayachukulia malalamiko yakekirahisi rahisi tuu na kuyatia kapuni. Maswali yao hayajibiwi, matakwa yao hayatekelezwi unategemea nini hapo.
Hebu tuchukue mfano mdogo kuwa mimi nimesoma Dar tangu elimu ya msingi hadi namaliza chuo na degree yangu ya ualimu. Nimepigika sana, sina historia ya kuishi nje ya Dar kisha wewe unanipangia kazi Rufiji, Musoma au mikoa mingine ambayo ukitaka mahitaji muhimu basi upoteze siku nzima kuyafuata, kisha unaniacha nijitegemee mwenyewe hapo nitaishi vipi na nikikuambia kuna masuala tuongee husikilizi. Kifuatacho ni kuhamia shule ya private kwa kurudi Dar au kutafuta biashara nifanye kuliko kwenda shule wakati hainisaidii kimaisha. Si kwa wote ila kwa wengi mtu ataangalia maisha yake kwanza haiwezekani yeye aumie kisha awanufaishe wengine hiyo imani tulishaiacha zamani na si utamaduni wetu tena.
Inasikitisha kuwa wanafunzi waliofikia kiwango cha kuingia kidato cha Tano ni asilimia sita 6% au wanafunzi 23,520 na wanafunzi 344230 hawana kiwango. Bora serikali itoe tena matokeo ili wayastandardize au wayasanifishe walau B iwe A, C iwe B na kadhalika lakini kwa hili sijui wapi tunaenda. Inaniuma sana nikifikiria hasa kuwa kuna kundi kubwa sana ambalo halina tena muelekeo wowote hususani wenzangu na mimi wasio na uwezo wa kifedha wa kurudia mitihani au kwenda private schools.
Kwa form four wapya muda munao na jitahidini kujipanga kaka yenu hapa Malaptop nawatakia maandalizi mema muda bado munao.