Serikali: Nyumba za kupanga - chanzo cha mapato kilichosahaulika

JeanPrierre

Member
Joined
Feb 4, 2012
Posts
91
Reaction score
30
Ndugu wa JF, wafanyakazi serikalini na sector binafsi ukiachilia mbali wafanyabiashara watakuwa wanajua maumivu wanayoyapata kwenye makato ya mshahara (yaani PAY AS YOU EARN). Lakini hii sector "nyumba za kupanga" naona imesahaulika kabisa wakati ingeweza kuchangia kiasi kikubwa kwenye pato la Taifa. Kitu ambacho kimenifanya hadi niandike thread hii ni baada ya kulipa kodi ya nyumba laki 9 kwa miezi 6 kwa mwenye. Nafikiri mtakubalina nami kuwa hizi hela mwenye nyumba hatoi rist ya kuwa amepokea hela na ambayo pia ingeonyesha kuwa kuna kiasi fulani kinaenda Serikalini.

My take:
Hii ni biashara kama biashara zingine, kwa hiyo ni muhimukuwa na kiasi ambacho kinaenda serikalini. Ni muda mwafaka kwa Serikali kuanzisha mkakati wa kuweza kukusanya mapato kwenye hizi nyumba za kupanga. Lakini vile vile wapangaji tungeshirikiana kutoa taarifa ili tuweze kujenga nchi yetu.

Nawasilisha!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Reactions: BAK

Naona unataka kutukasirisha wengi hapo kwenye red nadhani ulikuwa unamaanisha risiti ... mimi katika maisha yangu niliyowahi panga ghetto nikiwa secondary school nilikuwa nikilipa na kupokea risiti Arusha mwenye nyumba alikuwa mchaga na ni msahaulifu asipokupa risiti na siku zikapita hujadai risiti basi ujue next month utalipa twice au uhame na hata sasa hivi nalipa pango kwenye office yangu na risiti napata kwa kiasi unachotoa wewe ni lazima upewe risiti na withholding taxi on rent either ulipe wewe au umlipie huyo mwenye nyumba kama hujalipa au kupokea risiti ni upendo wako tu na ni kosa pesa nyingi sana umelipa.

Katika nchi hii hakuna kitu kilichosahaulika watu wanakwepa kwepa tu. hata mpangangaji wetu wa magogogni halipi pale ni bure kama unavyotaka white house pangeleta pato kubwa sana.
 
wazo lako la kutaka serikali ikusanye kodi ni zuri lakini utekelezaji wake unahitaji umakini, weledi na miundo mbinu ya kimfumo kuweza kukusanya hiyo kodi.Kwanza makazi/nyumba nyingi hazijasajiliwa kwa maana ya kutambulika wamiliki hili ni tatizo kubwa..Kama zingekuwa zinatambulika wamiliki wake kwenye mfumo na kodi kukusanya ingekuwa rahisi kidogo.Na kwa hali ya sasa ilivyo kama wenye nyumba wakibanwa walipe kodi tambua wazi kabisa kwamba hiyo kodi utalipa wewe mpangaji mwenye nyumba watapandisha kodi ya nyumba kwa kufidia hiyo kodi wanayotakiwa kulipa.Na bado wanaweza wakakupandishia kodi na wasilipe serikalini hicho walichotakiwa kulipa kutokana na udhaifu wa mfumo.Hivyo basi kwa hali sasa ilivyo ni vyema serikali isikimbilie kukusanya kodi kwa pesa ya pango, zaidi wakikite kwenye kuweka mfumo na miundo itayowezesha kutambulika kwa wamiliki na baadae ndo waanze kukusanya kodi.
 
Serikali yoyote corrupt haiwezi kukusanya kodi,,,

Wengi wa wamiliki wa hizo nyumba ni wafanyakazi wa serikarini na mashirika mengine makubwa ya serikali ikiwemo TRA,, so hawawezi kupitisha sheria itayowabana,,,,

But hii inshu ni noma kweli, maana kodi ya nyumba Dar es salaam zinapoelekea ni balaaaa,,, kila siku zinapanda
 

Sorry, nilitaka kumaanisha risiti, nlakini nashukuru kwa sababu umeelewa nilichokuwa namaanisha. Niseme tu kuwa kama wapo wanaotoa risiti basi ni wachache lakini kwa ujumla wengi hawatoi. Labda tu kama wengine walivyo changia nafikiri kikwazo kikuu ni kutambulika kwa hawa wamiliki na kukosekana kwa sheria inayosimamia hizi biashara. Kungekuwa na sheria inayosimamia nafikiri kila kitu kingekuwa kimeainishwa husuani tax na kiwango cha kodi na wasingekuwa wanapandisha kodi kiholela. Kwahiyo hakuna haja ya kuogopa kama hiyo Tax mpangaji au mmiliki ndo atalipa.
 
Mwenyewe unaweza kudhani una wazo zuuuuuuri na kujishebedua hapa jamvini bila kuangalia msingi wa kodi ni nini na nani hulipa kodi husika. Kama ulishani suala hilo litampunguzia mapato mwenye nyumba unajidanganya na jealous zako. Mwenye nyumba atakachofanya ni [(900,000 X 18) / 100] + 900,000 = 1, 062,000

Mara serikali itakaposikiliza maoni yako, hiyo ndio itakuwa kodi yako mpya.
 
Jan makamba alikua na hoja binafsi juu ya nyumba za kupanga bungeni sijui imeishia wapi?
 
 
Lengo hasa ni nini?
Kuongeza mapato ya serikali? Kupunguza mapato ya mwenye nyumba? au kuongeza gharama za kupangisha nyumba?

Serikali ina majukumu mengi kwa wananchi ambayo haiyatekelzi ipasavyo. Wananchi kwa kiasi kikubwa wanavumulia mapungufu hayo ya serikali. Ndio maana serikali nayo inafumbia macho mambo fulanifulani kama haya.

Tukitaka kwenda haki bin haki, itakayoumia ni serikali or more correctly chama tawala, kwa sababu wananchi wameshazoea kufanya mambo yao in a particular way. Kubadilisha ghafla kuna gharama zake...
 
Kodi inaweza kulipiwa iwapo kila mlipa kodi anafaidika. kwa mfano kama wewe ni mfanya kazi, ukionyesha risiti ya kodi ya nyumba unayolipa, na wewe unapunguziwa makato ya kodi kwenye mshahara. mwenye nyumba vilevile anapunguziwa kodi kwenye gharama zake mbali mbali anazolipia kama maji, umeme, ukarabati na kadhalika. kwa kufanya hivyo kila mtu anapata unafuu.
 


Target hapa ni kuongeza pato la serikali, impact kwa hawa wengine inategemea ni jinsi gani sheria ingekuwa inaelekeza. Mie siyo mtaalamu sana wa uchumi kaini niliona kuwa hii sector isiyo tambulika pengine ingeweza kuchangia kiasi flani. Tatizo siyo kwenye nyumba tu za kupanga lakini hata biashara nyingi hawatoi risiti kwahiyo sidhani kama hata wakaguzi kutoka TRA wagawanapata exact figure. Chukulia mfano kwenye biashara nyingi kariakoo, unakuta kuna bei mbili (kama utahitaji au hautahitaji risiti). Vitu kama hivi ndo ninavyomaanisha.
 
Uko sawa mkuu. Serekali ina makengeza, hailioni hiyo sekta vizuri


Ila laki tisa ni kidogo tu kwa miezi sita. Wenzio wanalipa m hadi nane kwa kipindi hicho na sarkali bado haiwaoni na hao wakalipe kodi
 
Makamba aliaachana nayo baada ya kugundua ata yeye na dingi ni Malandlord hapa town who pays nothing to the government but earns outrageous amount of monies through rents.
Jan makamba alikua na hoja binafsi juu ya nyumba za kupanga bungeni sijui imeishia wapi?
 
Uko sawa mkuu. Serekali ina makengeza, hailioni hiyo sekta vizuri


Ila laki tisa ni kidogo tu kwa miezi sita. Wenzio wanalipa m hadi nane kwa kipindi hicho na sarkali bado haiwaoni na hao wakalipe kodi


Ni kweli mkuu, lakini unapanga sehemu kulingana na kipato chako. Lakini cha muhimu ni kiasi flani kiende serikalini. Haingii akili waendelee tu kutegemea mishahara ya wafanyakazi. Kwa wenzetu kila unaponunua kitu lazima upewe risiti.

Lakini haitoshi tu kwamba hela ikusanywe (say bil moja ) harafu VAsco anatumia bil 3 kwenda kupiga pic na .................
 
Biashara ya nyumba na upangishaji nchi hii ni holela mno na wanaonufaika ni wenye nyumba,wapangaji ni kama slave tu.Mimi nilidhani huyu mama aliyetoka Habitat angeweza kubadilisha mambo haya kama vile kodi kulipwa kwa mwezi kame wenzetu wa kenya na kadhalika,lakini naye ni walewale.
 
Nilikuwa nasema hili jambo sasa mwaka wa nne sijui Serikali imelichunia. Licha ya kuwa ni chanzo kikubwa cha kodi vile vile ni chanzo kikubwa cha kuanguka kwa sarafu yetu. Kodi Dar zinalipwa kwa dollar!!!!! sasa unadhani shillingi itasalimika kweli? Kodi inalipwa kwa pound au Euro but sio Tshs. Watu wanakodisha nyumba hawalipi kodi sasa unategemea nini? But sio la kushangaza kwasababu wapo wakubwa pengine wanafaidika na hilo. Mnajisumbua bure hakuna kitakachobadilika hapo.
 
Ungeishauri kwanza serikali ituhakikishie ajira,kati ya watu milion 40 tanzania angalau watu milioni 10 wawe wameajiriwa na serikali pamoja na sector binafsi....then washauri huo unyonyaji.
 
Kama serikali ina njaa ya mapato itoe kipaumbele kwenye udhibiti wa vyanzo rasmi vilivyopo. Hili la nyumba kwa sasa waliache kama lilivyo.

Makamba kabla hajaelewa vizuri siasa alinza kuliongea ongea hili, baada ya kulielewa kwa undani ameacha nalo...
 
Niliwahi kuwauliza watu wa TRA wakati wa miaka 50 ya uhuru namna gani wanakusanya kodi za nyumba jamaa aliyekuwepo alijigamba hakuna mtu anayekwepa kulipa kodi ila ukweli hii sekta inabidi walipe kodi wakianza kulipa kodi itakuwa na unafuu kwa wapangaji kwani hawa watu wanajipandishia kodi wanavyojisikia lakini sasa hivi kuna nyumba zinapangishwa kwa dola kuanzia 1500 na kuendelea.
Kulipa kodi ni wajibu wetu badala ya kukaa na kuangaishana na watu wa kipato cha chini hii kodi ingechangia kwa kiasi kikubwa ikiwemo kutoa ruzuku kwa vifaa vya ujenzi ili watu wengi wamudu kujenga nyumba zao
 
Ungeishauri kwanza serikali ituhakikishie ajira,kati ya watu milion 40 tanzania angalau watu milioni 10 wawe wameajiriwa na serikali pamoja na sector binafsi....then washauri huo unyonyaji.

Nakubaliana na maoni yako lakini nafikiri suala na ajira ni sensitivu zaidi kwa maana vijana wengi wanaomaliza hawana uhakika wa kupata kazi. Moja ya sababu kuu nafikiri ni kukosekana kwa viwanda ambavyo vingeweza kuajiri hata vijana waliomaliza veta tu. Nafikiri ni hoja ambayo inahitaji mjadala mpana zaidi na ambayo inahitaji fani mbali mbali. Kwa mfano sioni sababu ya kwanini tunashindwa kuzalisha chuma chetu wenyewe wakati kipo tu aridhini na tuendelee kuagiza kutoka nchi za nje. Lakini hata kwa kiasi hiki tunachoagiza hakuna quality control ya kutosha inayofanywa na kupelekea ghorofa nyingi kuanguka. Nchi nyingi zilizoendelea km Germany, France na hata hapa karibu S.A zimeendelea kwa sababu ya kuzalisha chuma. Chuma ndo kila kitu katika ukuaji wa viwanda na ambavyo vinatoa ajira nyingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…