Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Mamlaka waliyo nayo wakuu wa mikoa, wilaya na Mawaziri kuamuru polisi kukamata watu au kuanzisha kesi hayapaswi kuwepo kabisa katika nchi inayoitwa ya kidemokrasia.
Huenda utaratibu huu ulifahaa wakati wa Nyerere kutokana na hali ya kisiasa na idadi ndogo ya watu wakati huo ila utaratibu huu haukapaswa kuendelea kuanzia utawala wa Mwinyi, wakati huu ndio haufai kabisa kwa sababu ya mabadiliko makubwa zaidi ya kisiasa na ongezeko la idadi ya watu.
Leo katika mfumo wa vyama vingi unapompa mkuu wa mkoa, wa wilaya au Waziri ambao ni makada wa chama tawala mamlaka ya kukamata watu utahakikisha vipi hawayatumii mamlaka hayo vibaya kisiasa?
Leo hii unapompa mkuu wa wilaya mamlaka hayo juu ya wilaya yenye watu zaidi ya milioni moja atayatumia vipi mamlaka hayo wakati hata watu wa mtaa wake tu walio wengi hawafahamiani?