Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Huu utaratibu wa wageni kutakiwa kujiandikishaa kwenye kitabu vya wageni vinavyofanana na vitabu vya mahudhurio ya wanafunzi kwenye hoteli, lodge na guest ni wa kijima au kishamba sana na umepitwa na wakati. Ni utaratibu mbovu kwa usalama na usiri wa mteja. Hii ndio sababu mojwapo inayopelekea watu wengi kutopenda kujiandikisha au kuweka taarifa za uongo kwenye hivyo vitabu.
Kwenye nyumba za wageni zitumike kadi/karatasi maalum za kujiandikisha ambazo unaweka taarifa ya mteja mmoja tu kwa ukurasa mmoja au vitabu vyenye ukarasa mmoja kwa mteja mmoja na risiti za malipo, Sio hayo mavitabu ambayo ukurasa mmoja unakuta wanajiorodhesha watu thelathini na taarifa zao zote muhimu.