BIG X
JF-Expert Member
- Nov 4, 2011
- 777
- 212
Sidhani hawa viongozi wetu wana watoto kwenye hivi vyuo, Yani wapo tayari kununua maelfu ya mabomu kuliko kuwapatia mahitaji hawa wanafunzi wa vyuo. Labda viongozi wetu hawana watoto, sababu hawajui uchungu wa watoto. Kuna maana gani ya kuwa na viongozi wazee kwenye serikali yetu halafu serikali inakosa busara kama uzee ni busara.
Ukiangalia hizo picha hapo hao wanafunzi wamekaa wakijadili matatizo yao ambayo yanawaumiza na wayapeleke panapohusika. Mnapowawekea Askari na vifaa vya hatari nyuma manake ni nini, ni kuwatisha!!. Kama ni kuwatisha basi serikali ijue inakosea sana badala yake mnawajenga ujasiri hawa wanafunzi bila nyie kujua. Baada ya miaka mingi 20-30 taifa litakuwa na watu wenye hasira ambao hawataliheshimu Jeshi la polisi hata kidogo, mnajenga nchi ya watu wenye visasi wakati huo nyinyi viongozi hamtakuwepo, mtakua mmetuachia balaa watanzania. Ndio mnataka tuwakumbuke kwa hayo!!!.
Ni wazazi gani nyie mnaoshindwa kuongea na vijana wenu, mkawasaidia na kuwatatulia shida zao. Mnafikiri mtaiweza nchi kwa kufanya vitisho!!!.
Kama mnawatisha sana wanafunzi miaka nenda rudi na hakuna anayetishika, mambo yanajirudia vilevile. mmeshindwa kuelewa mnatengeneza nchi ya namna gani.
Ni watoto wa masikini ndio wanateseka hivi!!!!.
Mjue tu kila jambo huwa lina mwisho wake.