Serikali punguzeni gharama za kuingiza umeme ili mkusanye kodi

Oppomall

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2017
Posts
3,683
Reaction score
3,966
Salaam wakuu,

Nijielekeze kwenye hoja.

Serikali ilikuja na Mpango mzuri sana wa kukusanya kodi za majengo kupitia matumizi ya Umeme (Luku)
Ulikuwa ni mpango mzuri sana kwakua hakuna mtu anayeweza kukwepa kutumia umeme na hakuna anaeweza kuacha kununua umeme for a life time.

Hata kama akinunua mara moja wa mwaka mzima malimbikizo yake atayakuta tu.

Sasa changamoto imekuja baada ya Serikali kupandisha kodi kutoka ile 27,000 ya zamani hadi 350,000/=
Kwanza hii gharama haijaangazia vipato vya wananchi na haijalenga kuwasaidia walipa kodi.

Pili,imewafanya Wananchi wengi kughaili ama kuchelewa kuingiza umeme maana hapo utakuta kuna gharama zingine kama nguzo kwa walio mbali, ufundi,wiring,vifaa vya ndani nk.

Hao wananchi wanapoacha kuingiza umeme ama kuchelewa ifahamike kuwa Majengo yao yanakaa bila kulipia kodi na Serikali inapata hasara,aidha wengine wanaenda mbali zaidi wanachukua Umeme wa jua kutoka Makampuni ya kukopesha kisha wanalipa kidogo kidogo,suala la kodi halipo tena hapo.

Ushauri wangu, litizameni hili kwa manufaa na maslahi mapana ya Taifa letu.

Nawasilisha.
 
Hakuna gharama zilizopanda,
Pili, kusema kweli tusipende vya bure, unajenga nyumba ya 20M ila hutaki kulipa 350k ya umeme, unataka hizo nguzo, nyaya na vitu ka hivyo nani alipe? Sometimes kama taifa tunazidi kulilia viti vya bure,
Watu wanataka Elimu bure, maji bure, Afya bure, nk,
Swali tutaendeshaje ? Wakati kiukweli kabisa wengi wetu tu wakwepaji wakubwa wa kodi ? Lipa tu bana kelele zisiwe nyingi,
 
Umeshaona Serikali inapoteza kiasi gani kwakua nyumba nyingi haziingizwa ymeme badala yake wamejielekeza kutumia sola?
Hizo nguzo bado wananchi wananunua.
Ukijiingiza kwenye biashara usiogope kufikisha huduma kwa watu ili uanze kuvuna.
Kwanza hizo ni huduma kwa wananchi wala siyo anasa,kwa serikali bunifu itasambaza bila kuwaza cost ili ianze kuchuma
 
Pamoja na 27,000 watu Wameshindwa kuweka umeme kisa wiring.

Serikali wekeni Nguvu kwenye viwanda na Biashara achana na watu binafsi ambae hana pesa alale Giza.
 
Nikilipa hiyo nguzo akija kuvuta mwingine nanufaika nayo au atapewa umeme bure tu? Kama umesema kitu ni mali yako acha nilipie ninachotumia mimi. Nguzo ni mali ya tanesco na itaunganisha wateja wengi japo uliyeilipia ni mmoja. Tuwe kama wa minara ya simu, sogeza huduma karibu yeye alipie matumizi yake
 
Moja kati ya vitu nitakavyokimbia ni TANESCo better kua na solar unauhakika nao kuliko hii kitu ni pasua kichwa sn
 
Hakuna gharama zilizopanda,
Pili, kusema kweli tusipende vya bure, unajenga nyumba ya 20M ila hutaki kulipa 350k ya umeme, unataka hizo nguzo, nyaya na vitu ka hivyo nani alipe? Sometimes kama taifa tunazidi kulilia viti vya bure,
Watu wanataka Elimu bure, maji bure, Afya bure, nk,
Swali tutaendeshaje ? Wakati kiukweli kabisa wengi wetu tu wakwepaji wakubwa wa kodi ? Lipa tu bana kelele zisiwe nyingi,
Mkuu sio kila mtu anae jenga basi anapesa wengine ndio hivyo tia maji tia maji.

Halafu mtoa mada hajasema bure, kasema zipunguzwe.
 
Yan mkuu, hio bei hapo ya 350k imepunguzwa toka 800k, bado mnataka ipungue tena,
Wabongo tusizoee tabia ya kulia lia sanaaa,
 
Umeshaona Serikali inapoteza kiasi gani kwakua nyumba nyingi haziingizwa ymeme badala yake wamejielekeza kutumia sola?
Hizo nguzo bado wananchi wananunua.
Ukijiingiza kwenye biashara usiogope kufikisha huduma kwa watu ili uanze kuvuna.
Kwanza hizo ni huduma kwa wananchi wala siyo anasa,kwa serikali bunifu itasambaza bila kuwaza cost ili ianze kuchuma
Sasa unadhani anaetumia solar anajikomesha au anakomesha tanesco?? Maeneo ya vijijini bado ni 27000 kama hawaingizi umeme ni tatizo jingine na mjini ni 321000 sasa umejenga nyumba kuanzia mil 10 kwenda juu unataka umeme wa 27k?? Hata circuit breaker na main circuit yako tu ni ghali kuliko hiyo.. Na hao wa nguzo wana option mbili wasubiri mradi uwafikie au kama unahela ulipe.. Umejenga nyumba ya mil 30 then hutaki kulipa 500k sababu ya umeme na nguzo unakuwa haupo serious.
 
Salaam wakuu,

Nijielekeze kwenye hoja.

Serikali ilikuja na Mpango mzuri sana wa kukusanya kodi za majengo kupitia matumizi ya Umeme (Luku)
Ulikuwa ni mpango mzuri sana kwakua hakuna mtu anayeweza kukwepa kutumia umeme na hakuna anaeweza kuacha kununua umeme for a life time.

Hata kama akinunua mara moja wa mwaka mzima malimbikizo yake atayakuta tu.

Sasa changamoto imekuja baada ya Serikali kupandisha kodi kutoka ile 27,000 ya zamani hadi 350,000/=
Kwanza hii gharama haijaangazia vipato vya wananchi na haijalenga kuwasaidia walipa kodi.

Pili,imewafanya Wananchi wengi kughaili ama kuchelewa kuingiza umeme maana hapo utakuta kuna gharama zingine kama nguzo kwa walio mbali, ufundi,wiring,vifaa vya ndani nk.

Hao wananchi wanapoacha kuingiza umeme ama kuchelewa ifahamike kuwa Majengo yao yanakaa bila kulipia kodi na Serikali inapata hasara,aidha wengine wanaenda mbali zaidi wanachukua Umeme wa jua kutoka Makampuni ya kukopesha kisha wanalipa kidogo kidogo,suala la kodi halipo tena hapo.

Ushauri wangu, litizameni hili kwa manufaa na maslahi mapana ya Taifa letu.

Nawasilisha.
Mimi ni mmojawapo niliyeghairi, mbaya zaidi nauziwa nguzo 2 kisa umbali na bado inabaki mali ya TANESCO, wateja wengine wataunganishiwa bure bila gharama ya nguzo kupitia nilizopigiwa mimi bei. Hii tanzania ni uwanja wa fujo.
 
Sasa unadhani anaetumia solar anajikomesha au anakomesha tanesco?? Maeneo ya vijijini bado ni 27000 kama hawaingizi umeme ni tatizo jingine na mjini ni 321000 sasa umejenga nyumba kuanzia mil 10 kwenda juu unataka umeme wa 27k?? Hata circuit breaker na main circuit yako tu ni ghali kuliko hiyo.. Na hao wa nguzo wana option mbili wasubiri mradi uwafikie au kama unahela ulipe.. Umejenga nyumba ya mil 30 then hutaki kulipa 500k sababu ya umeme na nguzo unakuwa haupo serious.
Mbona mwingine akija anaunganishiwa bila kulipia nguzo nilizolipia mimi? Hatusemi iwe 27 bali iwe cost hata ya usafiri na posho za waliofikisha mzgo na si kuwapigia gharama za nguzo.
 
Madhara ya kazi kumilikiwa na taasisi Moja ndiyo haya Sasa ubunifu hamna. tanesco yanajinenepea tu na vitambi vya vilibatumbo.kwanza Kwa Sasa kutokana na mradi wa JNHEPP kukamilika ilitakiwa watu waunganishiwe bure na wangepata wateja wengi na wangepata faida nyingi kupitia mteja anaponunua umeme.huyu aliyeshauri huduma ya uunganishwaji wa umeme uwe 321000 ndani ya mita 15 ni juha kwelikweli.
 
Pamoja na 27,000 watu Wameshindwa kuweka umeme kisa wiring.

Serikali wekeni Nguvu kwenye viwanda na Biashara achana na watu binafsi ambae hana pesa alale Giza.
Siyo kweli, serikali inafanya upumbavu wa hali ya juu kwenye suala la umeme, labda watu wanaoishi mijini ndiyo hawana changamoto ya kupata umeme, lakini vijijini ni shida sana. Hivi mwananchi wa kawaida unamwambia kuwa ikizidi nguzo tatu basi huo unahesabiwa kama mradi... Na inakuwa ngumu mtu kupata umeme... Mdau mleta mada ameshauri vizuri sana hapo juu sema basi tu
 
Tukiongea kuhusu vijijini bado serikali ina miradi ya kupeleka umeme vijiji,ambayo kimsingi mwaka uliopita wa fedha unatakiwa ukamilike,kwa ile hoja kwamba miondombinu ya nguzo haijafika maeneo mengi,pili kuna miradi ya vitongoji na mitaa kwa maeneo ambayo miradi ya umeme haijafika, halafu pia swala la wiring ya umeme hakuna sheria inayokwambia fanya wiring nyumba nzima,unaweza kufanya hata chumba kimoja,kwa ajili ya kupokea umeme, ifike point tuone umeme muhimu kama unavyoeka milango yako ya ndani kwenye nyumba yako.
 
Mh Bata mzinga sijakuelewa vizuri, ila nikisema vibaya unisamehe natanguliza. Kwenye suala la umeme vijijini serikali inafanya usanii na uhuni wa hali ya juu. Hii ni pengine kuwa wanachukulia suala la umeme kama anasa. Lakini wanasahau kuwa umeme ni huduma muhimu sana na si anasa tena, pia umeme ni biashara umeme ni mtaji nk.... Lakini utasikia hawana nguzo utadhani nguzo zinatengenezwa mbinguni... Tanesco wanafel sana
 
Mkuu natanguliza samahani pia kwako,na pia itakuwa busara kutoa neno Mh kwangu,naongea kama mdau kwenye sekta umeme, hasa hasa kwa maeneo hayo hayo uliyosema ya vijijini,kwenye miradi mingi inayotekelezwa kwa sasa ya kupeleka umeme vijijini TANESCO wanahusika kama wadau kwenye usimamizi,ila miondombinu yote ya kupeleka umeme vijijini wanapewa makampuni binafsi, hii ina maana kutoa huo ukakasi ambao unaosema,
 
Back
Top Bottom