Serikali sikivu ya CCM hili la Elimu ya juu hamlioni?

Serikali sikivu ya CCM hili la Elimu ya juu hamlioni?

Lulyeho

Member
Joined
Jun 16, 2013
Posts
52
Reaction score
7
Wakuu,

Wanafunzi wanaosoma vyuo vya elimu ya juu nchini (University & University Colleges) wameanza mafunzo yao ya vitendo (Teaching Practice & Practical Training) tangu jumatatu ya tarehe 14/7/14 lakini hawajapata posho zao ambazo kimsingi ndio huwasaidia kwa chakula na malazi wawapo katika vituo vyao vya kazi.

Kinachosikitisha ni kuwa (kama wanavyodai wao wanafunzi) utaratibu wa mwaka huu walilazimishwa kwenda nje ya mikoa yao kwa madai ya kuwa wanapata posho hizo!

Wanafunzi hao wamekuwa wakipokea ahadi hewa kutoka serikalini kuwa watalipwa siku chache zijazo tangu vyuo vyao havijafungwa mpaka sasa ambapo hakuna chochote kilichofanywa na Serikali hii!

Madai ya kwamba serikali haina pesa yamezagaa kwa wanafunzi hao ambao tunawaona wakitaabika katika vituo vyao walipopelekwa na kuwakatisha tamaa kama pesa hiyo inaweza kupatikana ndani yakipindi kifupi kijacho.

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma walijaribu kujikusanya maeneo ya Bodi ya Mikopo huko Dar lakini walikipata cha mtema kuni kutoka kwa askari waliovalia kivita.

Mimi najiuliza usikivu wa serikali uko wapi? na kama ni sikivu kwa nini na hili la wanafunzi wa elimu ya juu msilisikie? Kumbukeni hao ndo wapiga kura wenu mwakani mkiwakorofisha watawanyima kura na kuangukia pua.

Wasaidieni watoto wa wapiga kura wenu wanakufa njaa!

 
Nyinyi wanachuo si mnajifanyaga mnaipenda ccm leo mnalia nini tulieni iwanyooshe! mtajiuza sana mwaka huu mpaka mjue ccm ni adui namba moja kwa watu.
 
nyinyi wanachuo si mnajifanyaga mnaipenda ccm leo mnalia nini tulieni iwanyooshe! Mtajiuza sana mwaka huu mpaka mjue ccm ni adui namba moja kwa watu.

tuwe na subira hera itafika tu kwawakati.
 
Back
Top Bottom