Serikali sisi wajasiriamali pia ni watanzania msitufanyie hivyo

Dp800

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
1,793
Reaction score
3,709
SALAMU WATANZANIA WENZANGU.
Leo naomba niseme au niishauri serikali yetu. Ni kweli kwamba inatupasa kuiheshimu mamlaka hata Biblia imetuambia hilo, lakini niwakumbushe mlio kwenye mamlaka za juu kwamba nafasi mlizo nazo Mungu ameruhusu muwepo ili muwasaidie walio chini, na unapokua kiongozi jua wewe ni mtumwa wa walio chini yako(unawatumikia),kwa sababu hiyo unatakiwabkujali masilahi yao kwanza. Lakini hapa kwetu mambo ni tofauti, walio juu mmekua mnakakandamiza wanyonge, acheni niseme Mungu hapendi hilo. Mfano ni tangazo la hivi karibuni la mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro kuweka masharti magumu kwa wamiliki magari binafsi kuingia hifadhini, hapo nasema wazi haki haijatendeka. Ushauri wangu kwa serikali ni kwamba wabadilishe mfumo wa hizo leseni ( TALA), Nina uhakika wangeweka kiwango kwa gari, mfano. Kila gari lilipiwe dola 200 kwa mwaka hakuna mtu angekwepa na serikali ingepata mapato mengi zaidi kuliko mfumo kandamizi uliopo sasa wa dola 2000 kwa kampuni. Mwenye gari 200 alipe dola 2000, na mwenye gari moja alipe dola 2000. Hivi mnavyosema watu wajiajiri mmemaanisha au ni lengo lenu kujilimbkizia na kukundamiza wanyonge? Nini kimefichwa nyuma ya jambo hilo?, naomba waziri husika pamoja na serikali yote mheshimiwa JPM muangalie jambo hilo kiundani zaidi. Naamini raisi wetu yuko mstari wa mbele kutetea wanyonge maana kwa kipindi kifupi cha utawala wake tumeona mengi aliyotutendea wanyonge, na ninaamini hili halijui kwa mapana. Nimeona niandike mtandaoni maana sauti zetu wanyonge ni ngumu kufikia sehemu husika. Mimi ni mzalendo mwenye mapenzi na nchi yangu ndio maana nimeamua na Mimi kutoa maoni yangu.
Asanteni na Mungu wetu azidi kuwapa viongozi wetu afya njema na hekima ya kuongoza taifa letu.
AMEN..
Stefano E Makaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…