Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Uchunguzi : Wakati Serikali ikikuza sekta ya viwanda ili kupunguza tatizo la ajira nchini, ukuaji wa sekta hiyo umechangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa ajira za muda na za kudumu. Ajira hizi zimekuwa hazina ubaguzi wa jinsi kwa jicho la nje, japo kwa jicho la ndani yapo mengi yanayoendelea.
Licha ya jitihada hizo, hali sio rafiki kutokana na mazingira ambayo yamekuwa yakiwazunguka Wanawake katika baadhi ya viwanda, kuanzia vidogo, vya kati na vikubwa. Mazingira hayo yamekuwa mwiba mkali kwa Wanawake wengi wanaotamani kufanya kazi viwandani.
Katika viwanda vilivyopo Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani, kumekuwepo na viashiria vya mazingira ya rushwa ya ngono. Mazingira hayo yamekuwa kizingiti kikubwa kwa Wanawake wengi wanaofanya kazi viwandani kukivuka.
Visa vingi vimeshuhudiwa kwenye viwanda vya nguo, rasta na vinginevyo, ambavyo waajiriwa wengi ni Wanawake. Katika viwanda hivyo, ‘supervisor’ na watendaji wengine wenye mamlaka, wamekuwa mstari wa mbele kuomba na kushawishi rushwa ya ngono kutoka kwa Wanawake.
Kwa namna mazingira ya upatikanaji wa ajira yalivyo nchini, rushwa hiyo inatajwa kuwa kama ‘leseni’ ya kupata kazi au mikataba kwenye kiwanda, huku wengine wakiitumia kama kigezo kwa mfanyakazi wa kike kupandishwa cheo.
Zaidi ya viwanda 30 vilivyoko Dar es Salaam na Pwani, rushwa hiyo ya ngono imekuwa kama jambo la kawaida.
Hata Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO), kinakiri wazi kupokea kesi mbalimbali za rushwa ya ngono.
Jambo la kushangaza na kustaajabisha, kesi hizi za visa vya rushwa ya ngono kwenye viwanda vingi, zimekuwa hazifiki kwenye mamlaka husika, ambapo pia wanaodai kukumbwa na kadhia hiyo, wamekuwa wakihofia kufukuzwa kazi.
Pendekezo
Kwa mazingira yaliyopo kwa sasa, ni muhimu Serikali ikaunda kikosi kazi maalumu ambacho kitafanya uchunguzi wa kina kwenye viwanda, kumulika mazingira yaliyopo, hususani katika eneo la rushwa ya ngono, ili iweze kuweka mipango mizuri zaidi ya kisera na kuhakikisha utekelezaji wake.