Ndugu zangu,
Kwenye The Citizen la leo kuna makala ndefu ya Bernard Mapalala. Huyu ni Kaka na mwafamilia mwenzangu kwenye tasnia ya habari.
Mapalala ameanza kujenga hoja yake kwa kuiwekea nguzo za mwandishi Martin Meredith ( The State Of Africa). Bahati nzuri nami ninacho kitabu cha mwandishi huyo na nimekisoma.
Ufananisho wa Nigeria na hoja iliyo mezani kwetu juu ya Katiba na Muundo wa Serikali haungiliani. Ni vitu viwili tofauti. Sisi hatuna Igbo wala Biafra.
Lakini, ukiacha hilo. Ndugu yangu Bernard anahangaika pia na utambulisho wetu. Naamini anajua, lakini anashindwa kuweka wazi sisi ni nani na tumetoka wapi. Anataka hata tuukane Utanganyila wetu.
Bernard anaongea lugha ile ya Waziri Mkuu Pinda Bungeni aliposema kuwa ' Zanzibar Si Nchi'. Baadae ikaonekana kuwa ' Zanzibar Ni Nchi'.
Mapalala nae anataka tuamini kuwa hakujawahi kuwepo Tanganyika kwa kuwa anaandika;
" There was a Tanganyikan State, but there was no Tanganyikan Nation".
Ni yale yale ya ' Zanzibar si nchi ni dola!'. Unawezaje kuwa na dola bila kuwa na nchi?
Na Mapalala huyu katika andiko lake hili refu amejikita katika kutuonyesha hatari ya kuwa na Serikali Tatu na hata kuwepo Tanganyika bila yeye mwenyewe, mahali popote pale, kutueleza wazi anasimamia katika muundo gani wa Serikali.
Nadhani Mapalala angefanya hivyo, na kutueleza ni kwanini tufuate mfumo anaodhani yeye unatufaa, iwe Serikali Moja au Mbili, Ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Jumapili Njema.
http://mjengwablog.com