serikali tatu ndio chaguo la wengi

ansebaluu

Member
Joined
Aug 15, 2013
Posts
21
Reaction score
9
Baada ya bunge la katiba kuteuliwa kumekuepo na minongono na maneno ya hapa na pale kuhusu muundo Wa serikali uliopendekezwa kwenye rasimu. Baada ya maoni kukusanywa na tume imeonekana watanzania wengi kutaka serikali tatu. Badala ya watu kushauri mfumo uwo uweje ili uwe imara kumetokea watu wanataka kutuaminisha kuwa wanajua sana eti wao kama wasomi ndo wanajaribu kuwaonesha watanzania mfumo unaofaa.! Walikua wapi wakati Wa kukusanya maoni? Mimi nafikiri kama tunataka tuwe na katiba nzuri inayokubalika na wote tukubali maoni ya wananchi yaliyo kwenye rasimu.
 
hakuna cha serikali tatu wala nini, msimamo ni serikali mbili, jiandaeni kisaikolojia............
 
hakuna cha serikali tatu wala nini, msimamo ni serikali mbili, jiandaeni kisaikolojia............
Hata mimi ni muumini wa serikali Mbili. Na watanzania wengi pia wanaamini hivyo. Ila walikuja kupotoshwa tu hapa kati na CHADEMA
 
mimi seeikali mojarra AMA pita chiming muungano. tanganyika kwanza
 
Hata mimi ni muumini wa serikali Mbili. Na watanzania wengi pia wanaamini hivyo. Ila walikuja kupotoshwa tu hapa kati na CHADEMA

Serikali mbili zipi hizo, nitajie kwa majina, maana mi sielewi Nchi mbili zilizoungana zitakuwaje na serikali 2?! Muundo gani utatumika kuwa fair kwa serikali 2!?!!
 
Unaumwa wewe hembu nenda zanzibar kama utapata ardhi au cheo serikalini lakini huku bara wamefanya kwao

Hatuangalii kupata vyeo tunajali/tunaangalia maslahi ya wananchi wanyonge.Tafutaga vyeo kwa mtindo mwngine sio huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…