Serikali Tatu ni Mwafaka, siyo hasi ni chanya- Sehemu II

Serikali Tatu ni Mwafaka, siyo hasi ni chanya- Sehemu II

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Tumeona katika sehemu ya kwanzakwamba hofu walizo nazo wenzetu kuhusu uwepo wa Serikali tatu ni zakibinafsi na kimaslahi zaidi na hazina mashiko wala ithibati kwa kuwa jambo lenyewe halijaanza na ndiyo kwanza linapangwa kuanza.
Kama kweli bado tunaenzi fikra na mawazo ya waasisi wa Muungano wa Tanzania, hususan katika kuwa na muungano mkubwa zaidi wa eneo hili la Afrika lazima nchi yetu itwae uongozi wa kidira na kifikra hapa Afrika.
Ili kuwa na uwezo wa kuongoza na Afrika nzima kukubali kutufuata ni lazima tuwe kielelezo na mfano wa kuigwa na wengine katika mipango, uamuzi na utekelezaji wa wajibu na majukumu yetu ya kimaendeleo kwanza. Kisha lazima tuachane na ubinafsi wa kinchi na kuichukulia Afrika yote kama kitu kimoja.
Afrika Kusini ilianza vyema kwa kuja na wazo la NEPAD wakati wa enzi za mheshimiwa Thabo Mbeki, lakini alirithiwa pengine na watu ambao walikuwa hawakuwa katikamtazamo na msimamo wao juu ya Umoja wa Afrika na ambao matatizo ya ndani yamewashughulisha zaidi kuliko wazo kuu la kuwa na Afrika iliyoungana. Inawezekana kabisa uzuliwaji na ufuatiliaji wa wazo la NEPAD ilitakiwa ufanzwe na Tanzania, nchi yenye uzoefu wa kutosha lakini tukaiachia fursa hiyo ya kuongoza Afrika. Kwa haraka haraka ningelishauri ili Tanzania kuiongoza Afrika ipo haja ya kuwa na timu maalumu ya wasomi kutokavyuo mbalimbali ambao watafanya kazi kama tangi la fikra kuhusu namna ya kuwezesha kupatikana kwa muungano mkubwa zaiidi na Umoja wa Afrika. Kazi ya tangi hili lafikra itakuwa ni kushughulikia tu masuala yanayokwamisha upatikanaji wa Umoja wa Afrika na kutoa uongozi kwa Afrika, hususan katika kukwepa mambo yatakayofanya nchi nyengine zisitake kuwa sehemu ya muunganowetu.
Tanzania imekaa mahali ambapo uamuzi na mipango yake ya kiuchumi inabidi kuoanishwa na ile ya nchi zinazoizunguka. Wakati haujapita, hatua za dharura zikitekelezwa mara moja bado upo uwezekano wa angalau kuiaminisha Burundi, Rwanda, Congo, Malawi na Zambia kwamba sisi ndiyo tunaostahili kuwa washirika wao wakubwa. Dawa ya hili ni kufanya uamuzi unaodhihirisha kuwa sisi tutapata na wao watapata (win-win decision).
Faida za Serikali tatu na kuongezeka kwa Serikali katika muungano kila nchi inapojiunga ni pamoja na nchi zinazojiunga kuwa na uhakika kwamba mali zao asili zitatumika kufaa eneo lao kwanza na siyo vinginevyo; Muundo wa Serikali tatu utazivutia Serikali nyingine nyingi jirani Afrika kujiunga na muungano huo; Nchi husika kuwa huru kulinda utamaduni, desturi na imani zao bilakuingiliwa na wabia wengine kwenye muungano, mathalan, Zanzibar kulinda hadhi yake kama nchi ya Kiislamu kutokana na idadi ya waumini huko kuwa wengi; Nchi husika kuchagua kipaumbele chake bila kuingiliwa na wengine, mathalan, Zanzibar inaweza kuiga kuwa kama Cape Verde au Dubai au Hongkong au Singapore ya pande hizi za Afrika;
Nchi kuwa huru katika kuchagua wabia wake wa kimaendeleo, marafiki na washirika wake katika masuala yake ya kiuchumi na kimaendeleo. Madai ya gharama kama nilivyogusia awali, hayana uzito wowote kwani huwezi kuweka gharama kwenye kiu na njaa ya watu kuwa huru kupanga, kuamua na kutekeleza mambo yao wenywe; utawala wa sheria, haki na demokrasia pana na ya kina.
Ni dhahiri kwamba hasara kubwa zaidi siyo nyingine ila ni ile ya kukimbiwa na nchi ambazo zingeweza kuwa sehemu ya muungano husika; Gharama kubwa kwa upande wetu hivi sasa ni upacha wa viongozi wa kuteuliwa hususan wakuu wa mikoa na wakuuwa wilaya. Muungano unaweza kuimarishwa kwa kuondokana na wakuu wa wilaya na wenzi wao na kuwa na mkuu wa mkoa wa kuchaguliwa na watumishi wa umma wanaostahili katika mfumo wa vyama vingi. Mfumo wa Serikali tatu utasaidia sana kupunguza urasimu katika utendaji wa kila nchihusika na vilevile kupunguza gharama za pamoja kwa shughuli husika kufanywa kipamoja na kwa gharama ileile;
Ushindani utapunguza gharama katika kupata vyama na viongozi bora kutokana na mazao ya ufanifu na ufanisi katika menejimenti binafsi na ile ya umma;
Nchi na watu kujikita katika kile wanachoweza kufanya vizuri zaidi kutaboresha utendaji kazi na kuongeza tija katika kila eneo mbia la muungano.
Huu siyo wakati wa kutetea na kung’ang’ania uwepo wa Serikali mbili katika muungano wa Tanzania au ule mkubwa utakaokuja hapo baadaye. Huu ni wakati wa kwenda kwingineko duniani kujifunza njia bora za kuendesha Serikali huru mbili au zaidi chini ya Serikali moja kuu ya shirikisho au muungano.
Nchi zinazofuata zina mifano mizuri kwa mibaya kuhusu muundo wa muungano au sh irikisho unaotufaa: Ujerumani, Afrika Kusini, Brazil, India, Nigeria na Urusi ambako tunaweza kwenda kujifunza na kuhakikisha Katiba yetu inayoandikwa hivi itakuwa na tamko linalodhihirisha na kupambanua bila kuficha kuwa muungano au shirikisho letu ni la nchi zinazoungana pamoja, lakini kila moja ikiwa na Serikali yake na Serikali ya muungano itakuwa ikifanya kazi kwa mujibu wa kile kilichokubaliwa kufanyiwa na Serikali hiyo na nchi washirika au wabia wa Muungano iwe ni wawili au zaidi.

CHANZO: MWANANCHI
 
Back
Top Bottom