Inafahamika kuwa tume ya wataalamu iliyoteuliwa kushauri kuhusiana na ugonjwa huu ilitoa mapendekezo yake.
Inafahamika kuwa % kubwa ya mapendekezo ya tume hiyo yamepokelewa na yako katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
Hata hivyo katika yote, mawili haya yangalipo yakielea angani yakiendelea kupelekea wagonjwa na vifo zaidi ambavyo aghalabu vingeweza kuepukika:
1. Kutokutolewa takwimu za ugonjwa kinyume cha mapendekezo ya tume.
2. Kukosekana kwa usimamizi kuhakikisha utekelezaji kwa yaliyopitishwa.
#1 - Inapelekea maeneo yaliyoathirika zaidi kwa hatua stahiki za tahadhari kutokufahamika.
#2 - Mikusanyiko inaendelea pasipokuwa na tahadhali za msingi kuchukuliwa.
Wizara ya afya na hasa serikali hamuwezi kujivua lawama kwa mwendelezo wa hali hatarishi zinazoendelea.
Pana maisha mengi yanapotea hali ambayo ingeweza kuzuilika.
Ifahamike serikali ina wajibu mkubwa wa kuwahami wananchi wake dhidi ya majanga likiwamo hili.