sallim bakari
New Member
- Oct 6, 2016
- 2
- 0
TANZANIA TUITAKAYO
Tanzania tuitakayo ni ile ambayo itabana mianya ya rushwa, Rushwa ni tishio kubwa kwa uwajibikaji na utawala bora. Serikali inapaswa kuchukua hatua madhubuti kupambana na rushwa kwa kuweka mifumo ya udhibiti, kukuza uwazi, na kuwachukulia hatua wale wanaojihusisha na vitendo vya rushwa. Pia mianya ya rushwa ikibanwa serikali itaweza kusimamia haki na usawa katika jamii. Itapaswa kuhakikisha kuwa sheria zinafanyiwa kazi, na kwamba hakuna mtu au kundi la watu linalopewa faida au unyanyasaji. Serikali itapaswa kuchukua hatua dhidi ya ubaguzi na kutetea haki za makundi yote ya jamii, ikiwa ni pamoja na wanawake, watoto, wazee, watu wenye ulemavu, na wachache. Hivyo mianya ya rushwa izuiwe kwa nguvu zote haki na usawa katika jamii itapatikana.
Tanzania tuitakayo ni ile ambayo katika suala la uwekezaji, wawekezaji wanatakiwa watufate sio sisi kuwafuata ili waje kuwekeza, hapa ni pale tutakapo weka sheria zinazo mlinda mwekezaji na zitakazo mpa maslahi makubwa mwananchi,uwekezaji unalenga pia maslahi ya nchi na mwanachi kwa ujumla hivyo uwekezaji unatakiwa kuleta matokeo chanya kwa Mwananchi. Usalama wa Nchi unatakiwa kuwa wa hali ya juu sana hivyo kuvutia wawekezaji, mwekezaji anatafuta Nchi ambayo ina usalama wa kutosha na sera nzuri za uwekezaji ambazo hazimbani yeye, pia mikataba inayo sainiwa iwe ya uwazi na ukweli hii inatokana na ukweli kwamba mikataba mingi ambayo imesainiwa mingi ilionekana haikua wazi hivyo ikailetea shida Nchi. Hivyo katika uwekezaji mzuri wa serikali inaweza kusaidia kuzuia migogoro na vurugu kwa kuwezesha njia za amani za kushughulikia malalamiko ya wananchi. Kusikilizwa na kushirikishwa katika mchakato wa maamuzi kunaweza kupunguza tamaa na kusaidia kujenga jamii yenye utulivu.
Tanzania tuitakayo ni ile ambayo tutaweka mitaala ambayo ina mfanya mwanafunzi kuwa mbunifu na sio yule anye kalili, hapa ni kubadilisha sera ya elimu iwe ya kujitegemea na sio ya kuajiliwa yaani kuwe na vyuo vikuu ambavyo kama ni cha Madini ni madini tuu, umeme ni umeme tu, hapa naangalia vyuo kama cha kilimo, Madini, Ufugaji, Umeme, Uvuvi, Misitu, Ualimu, Utabibu, na kisichanganye corse kiwe kinahusu corse moja tuu. Na kianzie certificate mpaka Degree. Katika kuandaa mitaala ya elimu ya kujitegemea ni kumwandaa mwanafunzi akimaliza shule akafanye kile alichosomea bila kuajiliwa, kwa mfano kilimo, mwanafunzi akimaliza aweze kuendeleza kile alichosoma hapa ni kuwezeshwa na kwenda mikoa ya kilimo na kufanya kilimo sio kusuburi ajira ambayo ataisubiri kwa muda mrefu, lakini akiwezeshwa na kwenda kufanya kilimo basi atatoa elimu kwa wengine huko aliko sio mpaka afisa kilimo aje.
Tanzania tuitakayo ni ile ambayo tutaweka viwanda Nchi nzima vidogo vya kati na vikubwa kwa kila mkoa. Sekta ya Viwanda ni muhimu katika kukuza uchumi wa nchi na kuboresha maisha ya watanzania, pia ni muhimu kuhakikisha tunapata soko la uhakika la malighafi zinazopatikana nchini, kutoa ajira kwa wananchi na kuongeza mapato ya serikali pamoja na fedha za kigeni. Sekta ya viwanda ndio chimbuko la maendeleo ya nchi mbalimbali na ni mhimili mkuu wa kutegemewa katika kuongeza thamani ya malighafi tulizo nazo. Hivyo basi Tanzania tuitakayo ni ile ambayo itakuwa na viwanda vidogo, vya kati na vikubwa kwasababu sekta ya viwanda inakuza uchumi na kuboresha maisha ya watanzania, na pia ili Tanzania ipenye katika soko la Afrika mashariki na lile la Jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika (SADC) ni kuhakikisha sekta ya viwanda inakua na uzalishaji unaongezeka kufikia asilimia 50.
Tanzania tuitakayo ni ile ambayo itakua na uwajibikaji mkubwa, mkuu wa mkoa afanye kazi ionekane na waziri awajibike kwa kutoa matokeo chanya ya kazi aliyo kabidhiwa. Hapa atupe majibu yanayoeleweka la sivyo abadilishwe na akabidhiwe mwingine, pale mtu anapoteuliwa anatoa na ahadi zake mwisho wa mwaka analeta mrejesho wakile alicho ahidi. Pia serikali inayowajibika inajumuisha kutoa taarifa kwa namna iliyo wazi, kuruhusu wananchi kuhoji na kuomba maelezo ya ziada, kuwa tayari kuwajibika na kuchukua hatua stahiki kwa vitendo vyake na kukubali kuwajibishwa. Viongozi wa serikali wanapaswa kuwa na uwajibikaji kwa vitendo vyao na kuzingatia misingi ya uadilifu na maadili. Wanapaswa kufuata taratibu za kisheria na kufanya maamuzi yanayotumikia maslahi ya umma badala ya maslahi yao binafsi.
Tanzania tuitakayo ni ile ambayo itaboresha sekta ya Usafirishaji; usafiri ni muhimu kwa ajili ya kukuza mawasiliano, biashara, ukuaji wa uchumi na ajira.Katika masuala ya usafiri, tunatakiwa tuimalishe usafiri wa treni , na nzuri ni zile treni za umeme ambazo zinakwenda kasi, hizi ziunganishe mikoa mitano mikubwa mbayo ni Dar Es Salaam, Mwanza , Mbeya na Dodoma na Morogoro, na mikoa mingine ya Kimkakati ya uchumi ni Iringa, Ruvuma, Mtwara, Lindi, Kigoma, Kilimanjaro, Kagera, Tanga na Mara.
Tanzania tuitakayo ni ile ambayo itaweza kuwekeza katika suala la afya, hapa ni kuboresha vituo vyote vya afya kuanzia ngazi ya kitongoji, kijiji, kata wilaya, mkoani mpaka kitaifa. hivyo Serikali inapaswa kujenga zahanati, vituo vya afya na hosptitali kubwa kila wilaya na kuhakikisha huduma inapatikana masaa ishirini na nne, pia serikali inapaswa kujenga hospitali za rufaa kila mkoa na ziwe na huduma za kibingwa, hivyo kutasaidia kupunguza shida kwa wananchi kusafiri umbali mrefu kufata huduma za kibingwa. Pia sio tu kujenga hospitali bali kuhakikisha dawa zinapatikana na wadumu wa afya wanaajiliwa wa kutosha,
Tanzania tuitakayo ni ile ambayo katika suala la michezo tunatakiwa tuwe na viwanja vya mpira vyenye hazi kama cha Benjamini Mkapa kilichopo Dar es Salaam, kila mkoa kujengwe kiwanja cha hazi hio. Pia tuimalishe vipaji vya ndani kuanzia shuleni, kwa kila shule kuwe na somo maalumu kuhusu michezo ambapo ni kuimalisha michezo ya UMITASHUNTA na UMISETA, baada ya hapo tuwe na Academy za kukuzia vipaji katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Arusha, Mwanza, mbeya na Dodoma, hizi ziwe shule zilizo kamilika kutoka elimu ya kawaida mpaka michezo kama vile Makongo. Katika hizi sehemu za academy za kuendeleza vipaji kila mwaka timu za ndani nilazima wakatafute vipaji ndani ya hizi academy, na iwe ni lazima mana tunakuwa tumewekeza kwa kiwango cha juu, nafikiri ndani ya miaka mitano mpaka kumi matokeo halisi ya uwekezaji huu utaleta majibu chanya. Pia tuzipe motisha timu zetu za ndani maana nyingi hazina uwezo wa kujiendesha hapa ni uwekezaji ambapo mwekezaji yoyote akitaka kuwekeza katika timu yoyote hapa Nchini asiwekewe vikwazo vikamfanya ashindwe kuwekeza.
Kwa kuhitimisha serikali tuitakayo ni ile itakayoweza kutambua kuwa mahitaji muhimu ya wananchi ni afya, elimu, maji, usafiri, na nishati. Huduma hizi ziweze kupatikana kwa usawa na kwa viwango vinavyostahili na serikali iweke mfumo wa kusimamia ubora na kuboresha huduma hizo kila baada ya mwaka mmoja, huduma hizi ziwekewe mifumo ili kuhakikisha zinatolewa kwa viwango vinavyostahili.

Upvote
2