Serikali, tumieni nafasi hii ya ongezeko kubwa la makusanyo ya Kodi, na nafasi ya Mhe. Jakaya kikwete kama mwenyekiti jukwaa la elimu Duniani

Serikali, tumieni nafasi hii ya ongezeko kubwa la makusanyo ya Kodi, na nafasi ya Mhe. Jakaya kikwete kama mwenyekiti jukwaa la elimu Duniani

Joan lewis

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2019
Posts
993
Reaction score
1,463
Wasalaam, Wana jukwaa. Kufuatia hiki kizungumkuti Cha Idadi kubwa ya waalimu wasio na ajira hata kuelekea kuunda chama chao, huku kukiwa na Idadi kubwa ya upungufu wa waalimu kwa mashule mengi yaliyojengwa Kila Kona ambapo inatajwa upungufu huo ni 276,000 na walioko Mtaani 146,000 🙃🙃.

Tumieni nafasi hii mnayotangaza Kila miezi mitatu kuwa makusanyo ya Kodi yanaongezeka mpk 200% sometimes, (NETO wakimnukuu Mhe Rais samia kwamba ajira zinatolewa kwa hesabu ya ratio inayopigwa kulingana na ongezeko la makusanyo ya Kodi) {wage load}

kadhalika na nafasi ya Mhe. Jakaya mrisho kikwete kama mwenyekiti jukwaa la elimu Duniani (mwafrika wa kwanza kukalia kiti hicho) kuondoa hili Dubwana linalofukuta maana fursa na wakati havidumu milele.

Hata kama hili tatizo lilianza awamu za kabla nashauri Liangaliwe. Dawa ya kidonda ni kukiosha na kufunga sio kukipaka mafuta.

Wasalaam.
 
Wasalaam, Wana jukwaa. Kufuatia hiki kizungumkuti Cha Idadi kubwa ya waalimu wasio na ajira hata kuelekea kuunda chama chao, huku Idadi ya upungufu wa waalimu kwa mashule mengi yaliyojengwa Kila Kona ambapo inatajwa upungufu huo ni 176,000 🙃🙃 nchini.

Tumieni nafasi hii mnayotangaza Kila miezi mitatu kuwa makusanyo ya Kodi yanaongezeka mpk 200% sometimes, (NETO wakimnukuu Mhe Rais samia kwamba ajira zinatolewa kwa hesabu ya ratio inayopigwa kulingana na ongezeko la makusanyo ya Kodi) pia nafasi ya Mhe. Jakaya mrisho kikwete kama mwenyekiti jukwaa la elimu Duniani (mwafrika wa kwanza kukalia kiti hicho) kuondoa hili Dubwana linalofukuta maana fursa na wakati havidumu milele.

Hata kama hili tatizo lilianza awamu za kabla nashauri Liangaliwe. Dawa ya kidonda ni kukiosha na kufunga sio kukipaka mafuta.

Wasalaam.
Elimu inayotolewa Tanzania ni Elimu duni ambayo ukikosa ajira Tanzania hauwezi kujaribu fursa katika soko la dunia.
 
Elimu inayotolewa Tanzania ni Elimu duni ambayo ukikosa ajira Tanzania hauwezi kujaribu fursa katika soko la dunia.
Sawa mkuu Dr. Haya ila ndio tunasema hazijakosekana Wala sio kwamba hazihitajiki ilah ni maamuzi ya wafanya maamuzi.

Juzi Kuna mkoa nasikia shule Ina mwalimu Mmoja na asipokuwepo inabidi mwenyekiti wa Kijiji akashinde shule kuchunga wanafunzi. Ratio ya Idadi ya wanafunzi kwa mwalimu Mmoja iliyopendekezwa na Shirika la Elimu Duniani na pia walioleta hii formal education, inaonesha kwa Idadi ya waalimu waliopo sasa wanahitajika 276, 000 kufikia huo uwiano. Ila ndio mpaka mapenzi ya wafanya maamuzi.
 
Back
Top Bottom