Serikali: Tunaikabili Corona kisayansi, kiasili. Tumeshatumia bilioni 28 kuukabili ugonjwa huo

Dr Mollel + Dr Dorothy Gwajima = ?
 
Daktari wa meno akikanusha ukweli na kutujaza ujinga
Ajifukize yete mvuke wa joto kali linaloweza kuua virusi tuone kama hataunguua mapafu
Huyu angeishia kuuza dawa za Kimaasai barabarani na sio kuungalia mustakabali wa afya ya Watanzania wote
 
SERIKALI imesema inaendelea na jitihada za kukabili maambukizi mapya ya virusi vya Corona, vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 kwa kutafuta tiba mbadala, huku ikibainisha kuwa licha ya kutumia njia za asili, inaukabili ugonjwa kisayansi pia.
Hao wanasayansi ni akina Mgaya
 
Kumwamini mwana siasa ni kama kirusi kipya kwa sasa labda baadaye tukapowafanyia utafiti
 
Hao wanasayansi ni akina Mgaya
Mahali Waziri hanishawishi ni pale serikali kutoweka wazi uwepo wa ugonjwa huo na tahadhari zake kwa wazi sana. Wamepatiza ugonjwa majina mengi. Ingawa ukisoma kwa kina unatambua kama vile waziri anakubali lakini anaogopa kutamka. Weka wazi, watu wajikinge ili wasiambukize wengine au wasianbukizwe.
Mitaani ukivaa barakoa watu wanakushangaa. Waziri anajua hilo? Amesisitiza wapi uvaaji wa barakoa?
 
Wanakabili corona ipi? Tulishaambiwa haipo sasa wanaikabili ipi?

Wasamehe mkuu, walikuwa wanatuhadaa waliposema Mungu katuponya. Walikuwa wanakwepa kuchukua hatua ambazo zingeathiri nyanja za kimaisha. Waliogopa athari nyingine wakataka tusiogope ugonjwa unaweza kuua!! Focus yao haikuwa kuokoa maisha bali uchumi, uchaguzi nk.

Angalau sasa wanakiri kuwa kuna tatizo. Tuchukue hatua!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…