Serikali tupia jicho Mfumuko wa maghala au Magodown maeneo mbalimbali nchini unapelekea mfumuko wa bei za bidhaa

Serikali tupia jicho Mfumuko wa maghala au Magodown maeneo mbalimbali nchini unapelekea mfumuko wa bei za bidhaa

Neek

Member
Joined
Oct 1, 2019
Posts
75
Reaction score
86
Pamoja na kwamba ukuaji na ueneaji wa Magodown ni ishara ya ukuaji wa shughuli za kiuchumi na uongezekaji wa vipato na ukusanyaji kodi kwa Serikali lakini usiporatibiwa vizuri unaweza kuleta ugumu na ukali wa maisha kwa wananchi na pia unaweza ukapunguza kwa asilimia kubwa ukusanyaji wa kodi hasa ile kodi inayopatikana kutokana na mtu anaponunua bidhaa maana mfumuko wa bei unaweza ukapelekea kupunguza wanunuzi wa bidhaa ambao ndio wengi zaidi na hivyo kupunguza kodi

Mfumuko huu unasabaishwa na baadhi ya wamiliki wengi wa Magodown(maghala) wasio na nia njema ambao huzinunua kwa wingi kutoka viwandani au nje ya nchi na kuzitoa kidogo kidogo kwa wahitaji ili zionekane Upatikanaji wake ni ADIMU au Mgumu Mwisho wa siku bei yake inapanda sana, Sasa naiomba Serikali iangalie sana kama je kuna mbinu chafu za wamiliki wa maghala au Je wanashirikiana na Makampuni yanayozalisha kupunguza uzalishaji kwa makusudi ili mfumuko wa bei utokee.

ASANTENI.
 
Sikubaliani na wewe, maghala yana kua mengi kutokana na shortage of storage facilities. Na kwa taarifa yako ma godown mengi siku hizi ni matupu hayana kitu.
 
Sikubaliani na wewe, maghala yana kua mengi kutokana na shortage of storage facilities. Na kwa taarifa yako ma godown mengi siku hizi ni matupu hayana kitu.
si kila ghala linahifadhi bidhaa zilizokosa storage facilities
 
Back
Top Bottom