Serikali tuvilinde viwanda vyetu vya sukari

Magane

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2011
Posts
202
Reaction score
57
Baba wa taifa aliwahi kuishauri serikali kwamba bidhaa zinazotoka nje zitozwe kodi ili kuvilinda viwanda vyetu. Aliendelea kusema kwamba serikali ispotoza kodi bidha hizi kutoka nje zitauzwa kwa bei ya chini na hivyo kupelekea kufa kwa viwanda vyetu vya ndani. Uzalishaji wa sukari nchini wa viwanda vyetu bado haviweza kuzalisha sukari ya kutosheleza soko nchini nahivyo serikali kulazimika kutoa vibali vya kuingiza sukari tani 80,000.Lakini kwa bahati mbaya fursa hii imetumika vibaya na watu wasio waaminifu na kuingiza sukari nchini tani 200,000 ambayo inasemeka ni ya daraja la chini na na haitozwi kodi na hivyo inauzwa kwa bei poa na kuifanya sukari yetu kushindwa kuuzika. Tunaiomba serikali kwanza iwachukulie hatua kali wale wote walioruhusu kuingiza sukari nchini zaidi yale iliyoruhusiwa na serikali pia wadhibiti uingizaji horera wa sukari nchini.Sisi tulio ndani ya sekta ya sukari tunakabiliwa na hatari ya kukosa mishahara kwani sukari ndiyo tegemeo letu na vile vile wawekezaji wanaweza kuamua kuondoka na matokeo yakawa mabaya zaidi.Tuaiomba serikali ilinde viwanda vyetu vya sukari.
 

Kumbe unalilia tumbo lako, mi nilidhani uzalendo umekujaa! vipi kuhusu sisi tusiokuwa na uwezo, hauoni bei ya bidhaa inapokuwa juuuu sisi tunashindwa kujikimu!!!! Viwanda vya ndani viangalie mbinu bora za biashara zitazowafanya wahimili ushindani! Sisi wadanganyika hatuoni manufaa yanayoletwa na hao unaowaita wawwekezaji!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…