introvert
JF-Expert Member
- Sep 21, 2010
- 1,372
- 2,420
WanaJF,
Bila kuandika mengi, ombi kwa Serikali ni kupumzisha ndugu zetu kwa heshima na kwa utaratibu unaoeleweka na kwa uwazi.
Kwa sasa Serikali imeamua kutumia "HERD IMMUNITY" kama njia ya kupambana na huu ugonjwa. Hii ni kutokana na kauli ya Rais alipozungumza na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, matendo ya Serikali kusisitiza kazi ziendelee kama maBar, Ibada, usafiri wa umma, n.k. na sasa kauli ya Waziri Kigwangala.
Njia hii inayotumiwa inatabiriwa kuwa na vifo vingi na kwa utaratibu wa sasa ni Serikali inayozika miili ya wanaopeteza maisha. Iwapo vifo vitakua vingi kama inavyotabiriwa, maombi kwa Serikali ni kuandaa utaratibu wa wazi na unaoeleweka wa kuzika wale wote watakaopeteza maisha.
Hakuna sababu yoyote ya kuficha vifo au kuzika kwa usiri usiku.
Kila mkoa, hata wilaya, itenge maeneo kuhakikisha kuna nafasi ya kutosha ya kuzika na utaratibu uwekwe wazi wa jinsi ya kuzika.
Serikali imechagua njia hatari ya HERD IMMUNITY basi wale watakaopeteza maisha wazikwe kwa heshima.
Mwisho, kwa namna yoyote ile, lazima wale waliofanya maamuzi wawe RESPONSIBLE and ACCOUNTABLE.