Serikali Uganda yaweka sheria kali kuwabana wasanii wa muziki, marufuku kulewa, kuvaa mlege/nguo fupi jukwaani

Serikali Uganda yaweka sheria kali kuwabana wasanii wa muziki, marufuku kulewa, kuvaa mlege/nguo fupi jukwaani

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798
Serikali ya Uganda kupitia Wizara ya Utamaduni na Sanaa imetangaza sheria mpya zenye lengo la kuwabana wasanii, ili kulinda maadili na sanaa kwa ujumla.

Sheria hizo ambazo zimetangazwa wiki iliyopita, zinaeleza kuwa msanii yeyote hawezi kwenda nje ya nchi hiyo kutumbuiza bila kibali .

Moja ya sheria mpya, ni kwamba Msanii yeyote wa muziki hatakiwi kupanda jukwaani akiwa amevaa nguo fupi au mlegezo.

Sheria nyingine, msanii hataruhusiwa kupanda jukwaani kutumbuiza akiwa ametumia kinywaji au kilevi chochote.

Mabadiliko hayo pia, yanamtaka kila msanii asajiliwe na haitaruhusiwa wimbo uachiwe bila kukaguliwa na mamlaka husika ya serikali.

1.jpg
2.jpg
3.jpg
4.jpg
 
Back
Top Bottom