SoC01 Serikali, Umma na utawala bora

SoC01 Serikali, Umma na utawala bora

Stories of Change - 2021 Competition

Jo Africa Tz

Member
Joined
Jul 23, 2019
Posts
10
Reaction score
10
Mara nyingi hutokea kwamba umma mkubwa unatupita sisi na una hamu zaidi ya kusonga mbele hatua moja na kwamba juu ya yote hayo viongozi wetu hawafaulu kuwa viongozi wa umma mkubwa bali wanafuata kama mkia baadhi ya watu walio nyuma kwa fikra, wakiyaleta maoni ya watu wale na, zaidi ya hayo, kufanya makosa ya kuyafikiria maoni hayo kama ni ya umma mkubwa.

Yachukue maoni ya umma na yakusanye pamoja, halafu nenda kwa umma, yashikilie maoni hayo na uyatekeleze, ili upate kuunda maoni sahihi ya uongozi. Hii ndio njia ya msingi ya uongozi.

Katika kazi zote za vitendo za serikali, uongozi ulio sahihi ni lazima "kutoka kwa umma, kurejea kwa umma". Hii ina maana kwamba: chukua fikra za umma (fikra zilizotawanyika na zisizo na mpango) na zikusanye (kwa kupitia mwenendo wa kufanya uchunguzi juu yake na kuzigeuza kuwa zilizokusanyika pamoja na zenye mpango) halafu nenda kwa umma na uzitapakaze na kuzifahamisha fikra hizi mpaka umma wazikubali kama ni zao, wazikamate barabara na wazigeuze na kuzitumia katika vitendo, na pima usahihi wa fikra hizi katika vitendo hivyo.

Tena kwa mara nyingine kusanya fikra kutoka kwa umma na kwa mara nyingine nenda kwa umma ili fikra zile zishikiliwe na kutekelezwa. Na kadhalika, tena na tena, kama damu inavyozunguka mwilini bila ya mwisho, na kwa namna hiyo fikra hizo zitazidi usahihi wake, zitazidi kuwa na uhai na zitazidi kukuzwa kwa kila mzunguko. Hii ndiyo nadharia ya Kimarx kuhusu ujuzi.

Inatuwajibikia tuende kwa umma na tusome kutoka kwao, tuyakusanye maarifa yao kwa kanuni na njia bora zenye mpango zaidi, baadaye tuueleze umma mambo haya kwa kupitia uenezi siasa miongoni mwao, na tuwatolee mwito wa kuzitumia kanuni na njia hizi katika kutanzua matatizo yao na kuwasaidia kupata ukombozi na furaha.

Kuna watu katika idara za uongozi katika baadhi ya mwahala ambao wanafikiria kwamba inatosha kwa viongozi peke yao kujua siasa za chama na kwamba hapana haja ya kuufanya umma wazijue. Hii ni mojawapo ya sababu za msingi kwa nini baadhi ya kazi zetu haziwezi kufanya vyema.

Katika mavugu vugu yote ya umma ni lazima tufanye uchunguzi na uchambuzi wa msingi kuhusu idadi ya watu wanaounga mkono kwa dhati, wanaopinga na walioko kati kati na tusikate shauri juu ya matatizo kwa kuzingatia fikra zetu tu na bila ya msingi.

Umma katika mwahala po pote pale kwa kawaida huwa umegawika sehemu tatu:

1. Wale ambao kwa kulinganishwa na wengine wana harakati.
2. Wale ambao wako kati kati.
3. Wale ambao kwa kulinganishwa wako nyuma.

Kwa hivyo, ni lazima viongozi wawe na ustadi wa kuwaunga wale wachache wenye bidii kuwa uti wa mgongo wa uongozi na kuwategemea watu hawa katika kuinua daraja ya wale walio kati kati na kuwavuta wale walio nyuma.

Kuwa hodari katika kuzigeuza siasa za chama kuwa vitendo vya umma, kuwa hodari katika kuwafanya si makada wanaoongoza peke yao bali vile vile umma mkubwa kufahamu na kuelewa vilivyo kila vugu vugu na kila jihadi tunayoianzisha. Huu ndio ustadi wa uongozi unaotokana na Umarx-lenin. Vile vile huu ndio mstari wa mpambanuo kuonesha tuko upande wa makosa au la katika kazi yetu.

Kikundi cha uongozi hata kikiwa na bidii vipi, shuguli zake zitaishia kuwa jitihada za watu wachache zisizoleta maana isipokuwa shuguli hizo zichanganywe na shuguli za umma mkubwa. Kwa upande mwingine, ikiwa ni umma mkubwa tu ndio uliojishughulisha bila ya kuwa na kikindi madhubuti cha uongozi kinachozipanga vyema shuguli zao, shuguli hizo haziwezi kuendelezwa kwa muda mrefu, au kupelekwa mbele katika njia inayofaa, au kunyanyuliwa kuendea daraja ya juu.

Nyenendo za uchumi zifanywazo na umma, maslahi ya umma, maarifa na hisia za umma, yote haya ni mambo ambayo makada wanaoongoza lazima wayaangalie daima.

Tuangalie sana suala la maisha ya umma, kutoka matatizo ya ardhi, makazi na kazi mpaka matatizo ya kuni, mkaa, mchele, mahindi, mafuta ya kupikia, mboga, sukari, chumvi, maji, umeme, afya, elimu, barabara, ulinzi n.k. Matatizo yote kama haya yanayohusu maisha ya umma lazima yatiwe katika orodha ya mambo ya kuzingatiwa. Lazima tuyajadili matatizo haya, tukate shauri, tuyatekeleze mashauri yetu na tuyakague matokeo yake.

MWISHO:

1. Lazima tuufanye umma utambue kwamba tunawakilisha maslahi yao na kwamba maisha yetu yamefungamana na maisha yao.

2. Lazima tuufanye umma - kutokana na mambo haya - ufahamu kazi kubwa zaidi tulizoziweka, yaani kazi za vita vya kimapinduzi, na kwa njia hii, umma utaunga mkono mapinduzi, na kuyaeneza mapinduzi nchini kote, umma utaitikia mwito wetu wa kisiasa na utapigania ushindi wa mapinduzi mpaka mwisho.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom